Sitombeza aliyechagua kujifungua kwa upasuaji. Jamani kama si mvumilivu wa maumivu yale maumivu ya uchungu yanaweza kukupa ukichaa wa muda. Hayaelezeki kwa lugha rahisi. Kuna wengine uchungu unazidi hata siku tatu. Sijui hata wanawezaje maana masaa 8 tu kwangu yalikuwa ni mziki. Anayechagua upasuaji kukwepa shurba za kupush ni haki yake, tena tushukuru kuwa kachagua kuzaa maana wengine wanazisitisha zikiwa changa. Mtoto aje kwa njia ya kawaida au upasuaji bado ni mtoto, isitoshe hakuna tuzo za aliyezaa kwa njia ya kawaida.