Wanawake wengi hawawataki wanaume maskini

Na ukizingatia kwamba zaidi ya watanzania 47m ni masikini, mabinti wengi wataolewa na masikini watake wasitake. Bora wajiandae kisaikolojia tu.
 
Hapo sasa utajua we mwenyewe mkuu! Hujui tu uvumilivu wa kuanza na mtu chini ntajichosha kukuelezea.. magumu anayopitia mtu kumvumilia mwenzie vishawishi anavyovuka mpaka wafikie lengo! Jinsi mtu unavyojikana ili mwende sambamba na huyo masikini… Halafu anajipata anajiona matawi; hivi nilikutanaje kutanaje na hili limwanamke!! Hapa hatuongelei tamaa ya pesa tunaongelea kuanza na mtu chini, kama huwezi kutuliza fahamu vzr unakimbilia tamaa ni ww sasa! Sio kila jambo ni kuhusu tamaa na sio kila mtu ana tamaa..
 
Pata vitu kulingana na uwezo wako , tatizo letu tunataka pisi kali na hatuna kitu mifukoni ndio maana vilio ni vingi.

Huko kyela wamejaa wanawake kibao wala hawachagui na wapo tayari kuanza moja na wewe bwashee
 
Na ukizingatia kwamba zaidi ya watanzania 47m ni masikini, mabinti wengi wataolewa na masikini watake wasitake. Bora wajiandae kisaikolojia tu.
Wengi wataolewa ndio ila kuna pisi hatutakaa tuziguse mjomba, bora tukomae kuzisaka tu.

Ebu fikirai hata wewe hamisa mobeto ni awe mke wa Mjusi Sharobalo !!!!!!!
 
Naona sasa umeanza kuchomoza makucha hadharani na kujikita kwenye ukweli angalau kwa asilimia chache anyway mwanamke ni kiumbe kilichoumbwa kwa njia ya ajabu sana na isiyo eleweka ni ngumu kamwe kwa mwanaume kutambua mwanamke anataka nini hasa kwa nyakati tofauti.
 
Na ukizingatia kwamba zaidi ya watanzania 47m ni masikini, mabinti wengi wataolewa na masikini watake wasitake. Bora wajiandae kisaikolojia tu.
Wenyewe wanelewa hela ilivyokuwa ngumu lakini wanavyoweka demand unaweza sema wao ni foreigners hawajui hali halisi ilivyo nchini.

Wakiwa kwenye peak yao ya umri wanajisahau sana wanajifanya wao ni flagship.

Miaka ikisogea wanaanza kumsumbua Mwamposa.

Unakuta geto limejaa mafuta na maji, huku Mwamposa, kushoto Kuhani Musa, na wengine hata siwajui.

Hii imefanya hadi nikienda kwenye mageto yao huwa najipanga vizuri, nikifika mlangoni sivui viatu nazama navyo ndichi kuepuka kuteleza na mafuta.

Just a precaution isintokee kama ya Kanumba.
 
Ni ukweli wa wazi kabisa , kuna pisi ukikutana nayo , unalinganisha mfuko wako na uzuri na urembo alio nao , kama mtu mwenye busara tu unaona uvunge hata kama umemuelewa .
Pisi za aina hiyo huwa naamua kujenga uhusiano nazo wa kibiashara na siyo upendo kwa masaa machache kulingana na mfuko unapumuaje kisha tunaachana, kusema kwamba niimiliki milele hapo nitakuwa mshirikina kwa kweli!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…