Wanawake wengi hawapendi, bali wanatafuta 'sponsor' kwa kigezo cha mahusiano

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,399
40,305
Nimepata uzoefu huu, kupitia mazingira mbalimbali ya kimahusiano. Kila niliyekuwa nakutana naye, awe ameajiriwa, amejiajiri, yuko chuo, au hana ajira; wote wanaomba fedha za matumizi pamoja na gharama za kuendesha maisha yao.

Unaweza kushangaa mtu ameajiriwa au amejiajiri na ana kipato kizuri tu, lakini mwisho wa siku atataka akubane wewe mwanaume kwa kila kitu. Wakati katika mahusiano kila mmoja ananufaika na uwepo wa mwenzie, mbali na kumtolea gundu la kutokuwa kwenye mahusiano.

Sasa, najiuliza ni nini maana ya mapenzi; Ikiwa, wao wanawatumia wanaume kama wafadhili wa maisha yao, kwa kigezo cha kuwa kwenye mahusiano?

Hii hali imesababisha wadada wengi kutokuolewa, kutokana na kuendekeza mambo ya kumtumia mwanaume kama mfadhili wa kutimiza malengo yao ya kiuchumi.
 
Ni kweli kwa mfano mimi moyo wangu umebutuliwa mno napenda mtu akiwa ananitunza,ila wale wanaoanzaanza ndo hukopa hadi vikoba walee wawapendao kwa dhati....mi nakumbuka nishawahi kujipa bill kabisa ya kumjazia mafuta gari yake kwa mshahara wangu wa ualimu:p:p😂
Kama uko hivyo kweli, najua wewe ni waifu matirio
 
Nimepata uzoefu huu, kupitia mazingira mbalimbali ya kimahusiano. Kila niliyekuwa nakutana naye, awe ameajiriwa, amejiajiri, yuko chuo, au hana ajira; wote wanaomba fedha za matumizi pamoja na gharama za kuendesha maisha yao.

Unaweza kushangaa mtu ameajiriwa au amejiajiri na ana kipato kizuri tu, lakini mwisho wa siku atataka akubane wewe mwanaume kwa kila kitu. Wakati katika mahusiano kila mmoja ananufaika na uwepo wa mwenzie, mbali na kumtolea gundu la kutokuwa kwenye mahusiano.

Sasa, najiuliza ni nini maana ya mapenzi; Ikiwa, wao wanawatumia wanaume kama wafadhili wa maisha yao, kwa kigezo cha kuwa kwenye mahusiano?

Hii hali imesababisha wadada wengi kutokuolewa, kutokana na kuendekeza mambo ya kumtumia mwanaume kama mfadhili wa kutimiza malengo yao ya kiuchumi.
Wenyewe wanadai kwamba wao wako Kwa ajiri ya kuhudumiwa.

Ukiwauliza wao wana mhudumia nini mwanaume?Watakujibu sex
 
Back
Top Bottom