Wanawake wametugeuza wanaume chanzo cha mapato, ole wetu wallet zisisome

Loading failed

JF-Expert Member
Sep 14, 2023
1,945
5,849
Katika maisha ya sasa kumekua na wanawake wengi sana wasiojielewa kabisa, wanawake wameongezeka na wenye mtazamo hasi wa kuwatizamia wanaume kwenye mahusiano au nje ya mahusiano kama chanzo cha mapato na shida zao binafsi pamoja na huko kwao.

Wanaume tunafahamu wazi kabisa kila mtu atalibeba furushi lake mwenyewe na tusipofanya kazi kwa bidii hakuna kula hakika wala kupata hela, ila inasikitisha sana vijana mwenye maadili na hofu takatifu wanajitoa katika wimbi la kukataa ndoa na punyeto.

hivyo vijana kwa akili zao thabiti na timamu wanaona sasa ni vyema wawe na mwanamke kwenye maisha yao kwa nia nzuri tuu ya kujenga nao maisha kama wake zao ila wanawake hao hao wana waona hao vijana kwa taswira ya source of income kupitia macho yao ya tamaa na ubinafsi mwingi uliojaa katika mioyo yao yenye giza nene.

Vijana wanapambana huku wakiwa na mizigo mikubwa ya kujenga uchumi wao binafsi, kusaidia wazazi wao pamoja na kushiriki kwa moyo katika harakati za kijamii ,hapo hapo wanaona kuzidiwa na majukumu pamoja na kukosekana tulizo la moyo hivyo kwa akili za uanaume anaona nijambo la heri atafute mwanamke kama msaidizi sawa sawa na maandiko matakatifu yanavyo tuelekeza ila kizaa zaa kinakuja mwanamke badala ya kua msaidizi na mke mwema kwake anakuja kum-view mwanaume kama chanzo cha mapato na kumjengea maisha huko kwao sawa sawa na ubinafsi wake.

Wanawake hawana huruma kwa sasa, siyo mishangazi ,siyo single mother, siyo vibinti, wala sio wa mama wake za watu. Wanawake wameweka macho kwenye wallet ya mwanaume, wanawake wameweka macho kwenye kazi ya mwanaume , wanawake wameweka macho kwenye mshahara au kipato cha mwanaume, wanawake hao hao walivyo na roho mbaya natamaa wameweka macho hadi kwenye rasilimali za mwanaume huku wakieleza matatizo kede kede pasi na kufikiria wanaume tuna akili huaga wakati mwingine tuna nyamaza tuu kuepusha shari maisha ya ende.

Kutwa kucha wanawake utakuta wanalilia huduma na kudhibiti vipato vya wanaume, mara kudhibiti ndugu wa mwanaume kwa kuona wataneemeka kwa mapato, utakuta mwanamke anapiga mizinga pasi nakuwaza chochote ,mara utasikia naumwa nipe hela ni ende hospitali, mara mama anaumwa sijui mara anadaiwa kodi, mara vikoba nime cheza majina manne . Sasa kwa haraka haraka kwanini tusiwaone nyie mpo kimaslai na hakuna upendo wowote hapo.

Kama kweli mwanamke unataka ndoa , na kama kweli upo teyari kujenga maisha ya umoja na mazuri na mwanaume wako kwanini usitoeushauri wa jinsi ya kupata fedha na kujenga uchumi imara pamoja bali una mgeuza mwanaume chuma ulete, kwanini mnageuza wanaume kama ni shamba la bibi la kujichumia hela na kufanya anasa zenu huko mkiwa mmesula minywele isiyo na faida inayofika hadi kwenye makalio , kwanini mmekua wa na tamaa mbaya tena zilizo changanyana na uvivu wenu wa kutofanya kazi, kujiendekeza na kukosa kufikirisha akili.

Wanaume wenzangu ukiona upo na mwanamke usijiaminishe sana shauri yenu na waambia sisi washatugeuza chanzo cha mapato yao kupitia mahusiano haya ya kimapenzi au urafiki wa faida sasa shauri yetu, wanawake wameweka macho kwenye wallet wasione mwanaume ana kauchumi imara na ana tanashati kutwa ni kujipitisha maeneo na ikitokea la kutokea ni kumtegea mimba hata isiyo yake ili avune pesa zetu bure bure tuu na kutuacha masikini , wenye msongo wa mawazo na tufe tukachomwe moto

NB: USITURINGISHIE UNAPENDWA, FILISIKA UIJUE TABIA YA MWANAMKE WAKO.
 
We call it life. Ukizaliwa mwanaume tabu tupu. Imagine unatongoza mwanamke anakua yatima muda huo huo. Kila kitu kwake kinaisha na anataka wewe ndio uhudumie. Nipo single kwanza akitokea mwenye kujiweza sawa twende wote
 
Back
Top Bottom