Wanawake wasomi wana changamoto gani kwenye ndoa?

Nasikia siku hizi kuna vijana wanaoa vyeti ? Bila shaka hili huwa unalisikia.

Naomba ulitolee ufafanuzi kidogo.
Kwa uelewa wangu...wanatafuta mwenza wa kusaidiana kuendesha maisha....
Mwenza atakaye kubalika kwenye jamii vizuri....

Pamoja na yote tukubali ukweli...wanawake wengi sasa wanapata nafasi ya kwenda vyuoni...sio kitu kibaya.

Tunakuja kuharibu pale...kwenye kujua nafasi ya mwanamke ndani ya NDOA....
 
Nenda....ila utarudi tu
Lazima nirudi tangu nikaiacha furaha yangu. Ila itifaki za zamu lazima zizingatiwe, siku ya leo ilikuwa yako ila sababu kulala sebuleni siwezi, acha nimzawadie mwenzako, kisha nitaifidia hii kwako baada ya kukaa kama kamati.
 
Huwezi amini katika kile nilichokiandika nikiwa nime relax mno, na hapa nina kinywaji murua kiitwacho "al Qasus" taratiibu.

Wanangu watasoma ila nitawapa na ile Elimu ambayo mashuleni na vyuoni hawaipati. Yaani nitawatoa tongo tongo.

Vipi lakini mzime weye.....!??
Na mimi naomba niagizie "al Qasus" nazipenda sana.

Tabia ya mtu hauhusiani na Usomi.
 
Kwa uelewa wangu...wanatafuta mwenza wa kusaidiana kuendesha maisha....
Mwenza atakaye kubalika kwenye jamii vizuri....

Pamoja na yote tukubali ukweli...wanawake wengi sasa wanapata nafasi ya kwenda vyuoni...sio kitu kibaya.

Tunakuja kuharibu pale...kwenye kujua nafasi ya mwanamke ndani ya NDOA....
Ngoja nimalizie al Qasus nije kusema jambo juu ya haya uliyo yaandika. Ikitokea nimesahau, basi ni juu yako unikumbushe.

Ahsante.
 
Wasalaam wanajukwaa hili pendwa.

Niende moja kwa moja kwenye swali, naomba kwa wazoefu ambao mmeoa wanawake wasomi kuanzia shahada ya kwanza (Bachelor's degree) kuendelea, wana changamoto gani hasa kulinganisha na hawa wenye elimu chini ya hapo kwenye ndoa?
Nachojua mwanamke akiwa na pesa plus usomi huwa anaoa, kuwa makini usiolewe
 
Na mimi naomba niagizie "al Qasus" nazipenda sana.

Tabia ya mtu hauhusiani na Usomi.
Usijali wewe tena, nakuletea.

Elimu huwa zina wa shape sana watu. Ndiyo wale waliofaidika na Elimu zama za kale, walikuwa wanasema hivi :

"Sisi tulikuwa tunajifunza Elimu miezi miwili na tunajifunza adabu (Tabia njema) miezi mitatu". Ukitafakari kwa makini maneno haya,kwa thamani yake yanafaa kuandikwa kwa wino wa dhahabu na sherehe yake kujaza vitabu kwa vitabu.

Narudi....
 
Wasalaam wanajukwaa hili pendwa.

Niende moja kwa moja kwenye swali, naomba kwa wazoefu ambao mmeoa wanawake wasomi kuanzia shahada ya kwanza (Bachelor's degree) kuendelea, wana changamoto gani hasa kulinganisha na hawa wenye elimu chini ya hapo kwenye ndoa?

Naomba nikujibu kama ifuatavyo....
Changamoto za wanawake karibu wote zinataka kufanana, na hii haijalishi kama umeoa mwenye vyeti ama asie na vyeti.
Tabia njema ya mke ama mke kuitambua wajibu wake/nafasi yake kwa mume wake, haijawahi kujalisha kama ana vyeti ama hana vyeti.
Kimsingi mume ni mume tu, na wajibu wa mume utapaki kuwa palepale pasipo kujalisha kama mke anamiliki vyeti ama lah.
 
Ujuaji mwingi. Halaf wanataka equal powers kwenye mahusiano.
Samahani mkuu, kama unamaanisha mahusiano ni sawa.
Lakini kwenye ndoa kamwe hakuna equallity, bali mume ni kichwa cha nyumba and mume na mke kila mmoja anapaswa kuwajibika na kuitambua nafasi yake katika ndoa
 
Kwa kutumia ndoa yako kama mfano. Why unapinga hili? Explain
Naomba uniulize swali, ingawa sipo hapa kuisemea ndoa yangu mkuu.
On top of that, kwanza una mke..??
Maana nisije nikajikuta nabishana na hewa hapa....
 
Mama yangu alikua na diploma ya ualimu.. baada hakuishi Miaka mingi na baba yangu..na akiwa na watoto watatu.. baba yangu alimshawishi Mama yangu akasome Degree Kama baba yangu alivyosoma...baba akabaki na watoto Mama akaenda kusoma degree.

hakuogopa Kwamba watalingana elimu au kipato.. Mungu akurehem baba yangu ..hakika Ulifanya vyema...

Nawashangaa vijana wasiojua nafasi zaidi Kama wanaume kuanza kuwaponda waliosoma..

KILA mtu na amchangue amtakae...na atakae ridhika nae regardless of ELimu.
 
By the way....
Vijana mmekua laini na dhaifu sana hata kwa wanawake, na hii imepelekea kushindwa kusimama kidete kama wanaume na kufikia kujiliza hovyo Hadi kusingizia vyeti vya wanawake vinavyo wapa hofu.
Ebu acheni uvivu, punguzeni unyonge na hofu. Simameni na mtambue nafasi zenu ndani ya ndoa please.....
 
Mama yangu alikua na diploma ya ualimu.. baada hakuishi Miaka mingi na baba yangu..na akiwa na watoto watatu.. baba yangu alimshawishi Mama yangu akasome Degree Kama baba yangu alivyosoma...baba akabaki na watoto Mama akaenda kusoma degree.

hakuogopa Kwamba watalingana elimu au kipato.. Mungu akurehem baba yangu ..hakika Ulifanya vyema...

Nawashangaa vijana wasiojua nafasi zaidi Kama wanaume kuanza kuwaponda waliosoma..

KILA mtu na amchangue amtakae...na atakae ridhika nae regardless of ELimu.
Your Dad is pretty smart.
 
Wasalaam wanajukwaa hili pendwa.

Niende moja kwa moja kwenye swali, naomba kwa wazoefu ambao mmeoa wanawake wasomi kuanzia shahada ya kwanza (Bachelor's degree) kuendelea, wana changamoto gani hasa kulinganisha na hawa wenye elimu chini ya hapo kwenye ndoa?
Nadhani badala yakuwaona kama changamoto waone kama backup kwako yakukufikisha kwenye malengo yako. Think positive. Msikilize mwanasaikolojia unaweza kujifunza jambo.

Wengi wao sio submissive 100% vyeti vyao huwaongezea options ktk maisha. Ndoa hudumu zaidi pale mwanamke asipokuwa na options nyingi hasa hasa za kiuchumi, wanawake huolewa for security reasons.

Unafahamu kuwa asilimia kubwa ya wanawake huolewa na wanaume wasiowapenda? Wengi huolewa na best option aliyokuwa nayo kwa wakati husika. Ukitaka kuwa na ndoa yenye furaha hakikisha mwanamke anakuhitaji zaidi wewe na sio vinginevyo.
 
Back
Top Bottom