Wanawake wanavyoivaa Mikenge kwenye ndoa………! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake wanavyoivaa Mikenge kwenye ndoa………!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Mar 27, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Mar 27, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ngoja leo niyadadavue makosa yanayofanywa na wanawake wengi pale wanapoamua ni nani wa kuoana naye:

  1. Kosa la kwanza, unaolewa na mtu ambaye unajua kabisa ni dhaifu na mkorofi, ukitarajia kwamba ataondoa kasoro zake akiwa ndani ya ndoa. Hili ni kosa kubwa. Kama huna furaha sasa na mtu kabla hujaoana naye, usikubali kuingia huo mkenge. Huwezi kutegemea mtu kuadilika aiwa ndani ya ndoa.

  2. Kosa la pili, unaolewa na mtu asiye sahihi kwa sababu ya msisimko wa mwili kimapenzi lakini si kwa sababu ya tabia zake. Kuwa mwangalifu na neno "Nakupenda" neno hili mara nyingi maana yake ni "Nina uchu nawe." Ndiyo amevutiwa nawekimaumbile, lakini undani wa tabia yake unaujua? Hapa kuna mambo manne… Kwanza, Je anapenda kutomfanyia binadamu mwenzie mabaya kama ambavyo yeye hataki kufanyiwa? Pili, anaishi vipi na watu wengine? Anaishi vipi na watu ambao ana uadui nao, Anawasamehe au analipiza visasi? Je anatoa misaada kwa masikini? Tatu, je ni mkweli, anachokisema ndicho anachokifanya? Je anaaminika? Majukumu anayoahidi kuyafanya anayatimiza? Nne, je anajipenda? Je ni mtu ambaye yuko imara kimapenzi au ni mtu wa kuyumbayumba na asiye na msimamo? Sio mtu akishauriwa na marafiki zake au ndugu zake huko, anakuja na maamuzi yasiyo na kichwa wala miguu

  3. Kosa la tatu, unaolewa na mtu ambaye hamna malengo na vipaumbele vya aina moja vya maisha. Je mna utashi wa aina moja? Kwa mfano ni vyema mwanamuziki akaolewa na mwanamuziki mwenzie kwa kuwa anajua mzingira ya kazi ya mwenzie ili kupunguza wivu wa kupindukia usio wa lazima

  4. Kosa la nne, unaolewa na mtu asiye sahihi kwa sababu mnakutana kimwili mapema mno. Kukutana kimwili kabla ya ndoa kunaweza kuleta matatizo makubwa mno. Tendo la ndoa kabla ya ndoa hufunika uwezo wa mtu kufikiri. Mtu anabaki kufaidi na kubaki kujali mapenzi ya kimwili na kusahau kukuna ubongo juu ya mambo mengine. Ni lazima mwanamke akune ubongo ili kujua kama huyo mpenzi anakidhi vigezo vyote vya mume mtarajiwa.

  5. Kosa la tano, unaolewa na mtu ambaye huna msisimko wa kimwili umwonapo. Kuna uwezekano mkubwa mwanamke akavutiwa na mwanaume kwa sababu ya aina ya gari analomiliki. Hapa hakuna msisimko wa kimwili bali mwanamke kavutwa na gari au rasilimali alizo nazo mwanaume huyo.

  6. Kosa la sita, unaolewa na mwanaume anayependa kudhibiti. kuwa na tabia ya kudhibiti wenzako ni ya dalili za mtu jeuri na mwenye kujisikia na mfujaji. Naomba kutofautisha kati ya "kudhibiti" na "kutoa mawazo." Mtu anayekupa mawazo ni kwa faida yako, lakini anayekudhibiti ni kwa faida yake.

  7.
  Kosa la saba, unaolewa na mtu asiye sahihi kwa sababu unakimbia matatizo uliyo nayo. Unaweza kuwa hujaolewa na huna raha wala amani na ukataka kuolewa. Ndo haiwezi kukutatulia matatizo yako binafsi ya kisaikolojia nay a kimapenzi. Badala a kuyapunguza matatizo hayo, ndoa itayaoneza. Kama huna amani na huyafuahii maisha, chukua jukumu la kurekebisha matatizo hayo sasa kabla hujaolewa. Itakuwa ni faida kwako na kwa mmeo mtarajiwa.

  8.
  Kosa la nane, unaolewa na mtu asiya sahihi kwa kuwa yuko ndani ya pembe tatu. Mtu ambaye anaishi na wazazi wake ni moja ya mfano wa mtu anayeishi katika pembe tatu. Watu wengine wanaoweza wakawa wanaishi ndani ya pembe tatu ni kama wanaofanya kazi saa 24! Huyu mtu halali? Watu wengine walio katika pembe tatu ni watu wanaotumia madawa ya kulevya, mtu anayetawaliwa na "hobbie" zake, anapenda sana michezo (Mpira), kuperuzi mitandao ya kijamii na anapenda sana fedha. Hakikisha kwamba wewe na mpenzi wako , nyote hamtawaliwi na pembe tatu. Mtu ambaye anatawaliwa na pembe tatu hawezi kumtimizia mpenzi wake haja ya upendo atakapokuwa anahitaji. Kama mpenzi wako anatawaliwa na pembe tatu kwa kiasi kikubwa, wewe huwezi kuwa kipaumbele chake.
   
 2. Prishaz

  Prishaz JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,928
  Likes Received: 1,461
  Trophy Points: 280
  kwa kuongeza unaolewa na mtu ili mradi na wewe uingie kny ndoa kutokana na msukumo wa kujiona umechelewa unakimbizana na umri! Pressure kutoka kwa ndugu,marafiki walioolewa n.k
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Hiyo namba 7 ndo kosa kubwa maarufu. Kuoa ama kuolewa kwa sababu za kiuchumi, upweke, jina kubwa na kadhalika ni fatal mistake. Sijui kwa nini hatuelewi hii. If u ar not happy with yourself, usitegemee mtu mwingine akufanyie furaha yako.

  Namba tatu ni muhimu pia. Kuna mtu ndoto zake zinazungukia kwa wazazi wake. Kama unataka kupaa zaidi atakuvuta chini. Hawa ni wale wanaume wanaoamini kupata cheo kazini lazima utembee na boss wako, gggrrrhhhh!
   
 4. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na wewe kwa asilimia kadhaa, swali linakuja kwa wale pretenders na ucsahau kua wanaume wamejaliwa kipaji hicho pretending! Mwanzoni mwa mahusiano au wakati wa uchumba anakua m2 safi kabisa yan kasoro zinakua ndogongogo kabisa zinazosolvika LAKINI mnapoingia kwny life comitment yan ndoa kha!hapo ndo utaona true colours,kwa hili unaliongeleaje mkuu?
   
 5. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Nami naongezezea:
  Unaolewa na bishanga kwa kuwa ana bangalo masaki na li mercedes la ukweli (kama langu 600SL).
  Unaolewa na bishanga kwa kuwa baba yake ana jina kubwa mjini Ndulu,Mengi,Bakresa,Zitto Kabwe,Mwanakijiji,Pinda etc.
   
 6. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,125
  Likes Received: 23,734
  Trophy Points: 280
  Shiii..jamani taratibu ati, wengine tunatafuta wachumba humu. Msimwage mboga!.
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  na wewe unajina kubwa???
  Kilo ngapi? Au mls ngapi?

   
 8. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,125
  Likes Received: 23,734
  Trophy Points: 280
  Yegomasika na Ng'wanamalundi ni lipi jina kubwa hapo..
   
 9. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #9
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,765
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  mkuu umenena
   
 10. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #10
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,679
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Swali mkuu, na je kama huyu mwanamke anayeolewa ana tabia kama hizo? Na je wanaume/wanawake ambao wote wako hivyo hawapaswi kuwa na ndoa?
  (Kweli ni maneno mazuri but we all know c watu wote wako hivyo)
   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  Mar 27, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  nawaonea huruma sana walioolewa na mwenye tabia namba 6 na saba...
   
 12. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #12
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,033
  Trophy Points: 280
  hakuna kitu mbaya kama hiyo namba 5.....
  Mtambuzi bana.....
  nini kutushushua watoto wa watu mapema namna hii....a a..

   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  Mar 27, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  hahahah, huyo wa namba tano nahisi akimuona mumewe inabidi ajitoe ufahamu na ajisisimue....sipati picha kunapo 6X6 inakuwaje.......


   
 14. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #14
  Mar 27, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,431
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   
 15. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #15
  Mar 27, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Baba nitampata wapi asiyekuwa na moja wapo ya hayo?
  Na hiyo no 4 hapo inakuwaje?nijirisk kwa kukubali kuuziwa mbuzi kwenye gunia baba?

  Yote ni magumu ila no 6 na 7 ni magumu zaidi!!!!
   
 16. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #16
  Mar 27, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,319
  Likes Received: 2,605
  Trophy Points: 280
  well said!
  binafsi naamini waathirika wakubwa wa mahusiano na ndoa ni wanawake.sababu inayonifanya niamini hivi ni kwa kuwa wao sio waanzilishi wa mahusiano.
   
 17. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #17
  Mar 27, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hili Zaidi yako mtani...!
  mercedesg800.jpg
   
 18. mgeni10

  mgeni10 JF-Expert Member

  #18
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 1,112
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mzee hi kali

  Ni mbaya kuolewa na mtu kwa kutamani kuzaa nae tu, kwa sababu zozote zaidi ya mapenzi ya kweli kwake
   
 19. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #19
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Just lost the direction of your physical address, keep waiting am only around the corner baby!
   
 20. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #20
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  na hapo ndo shida itakapoanza. Hakuna karaha kubwa kuliko zote kwa mwanmke anapogundua akiwa tayari ndani ya ndoa kwamba 'kumbe jamaa yake jongoo hapandi mtungi, mweeeee!".

  Ni heri kujaribu aisee, ili uondokane na risk nyingi!
   
Loading...