Wanawake ukimpenda mwanaume unafanyaje hadi uwe naye?

Wanawake ukimpenda mwanaume unafanyaje hadi uwe naye?

Mmhh mimi kwa kweli kumpenda mwanaume kiasi hicho hapana na hata ikitokea siwezi kumuonesha. Wanaume wenyewe ndiyo hawa wengi umalaya tu.

Wewe utampenda na utafanya kila njia kumuonesha ajue kuwa unampenda mwenzako ataona hiyo ndiyo fursa ya kula tunda kimasihara. Wenyewe wanasemaga "ng'ombe kajipeleka machinjioni" sijui "mbuzi kafia kwa muuza supu" na ujinga mwingine kibao.
Kweli unataka kuniambia hujakutana na mtu unlliemzimia unazingua, jamii unayojichanganya nayo hakuna vijana wenye kuuteka moyo wako,
 
Hii mbinu unayompa, ataliwa kimasihara na ataachwa tu.
Njia yoyote atakayotumia ataliwa kimasihara kwa kuwa yeye ndiyo aliejipeleka hapo ni kama anafanya gambling kuna kupata au kukosa,
 
Zipo tamaduni nyingine nyingi tu zinazomgandamiza mwanamke
Hujaelewa nilichoandika!Nazungumzia mila kumgandamiza mwanamke na wakati huohuo hiyo mila kupendwa na kulindwa kwa nguvu zote na mwanamke huyohuyo
 
Kweli unataka kuniambia hujakutana na mtu unlliemzimia unazingua, jamii unayojichanganya nayo hakuna vijana wenye kuuteka moyo wako,
Hakuna aise nikiwaza wanaume wengi wa kiafrika walivyo na imani za kijinga huwa nakosa hizo nguvu za kupenda hivyo
 
Sidhani kama tunaipenda wala kuilinda basi tu jamii inatulazimisha
Mnaipenda kwa sababu mngekuwa hamuipendi mngekuwa mmeshaanza kuipinga kama mlivyopinga mila nyingine mbaya na mkafanikiwa
 
Sasa ukimpenda unabaki unaumia tu?

Kwani hujaonaga wanaume wanatongoza lakini akakutumia tu.

Hizo ni risk tu za maisha.

Yupo mwanaume alitongozwa na wapo kwenye ndoa mpaka leo.

Mi naona Kama umependa you try to ukitolewa nje yote maisha tu...
Huo ni mtazamo wangu tu mwisho wa siku maisha yako ni vile wewe umeamua yawe. Kwa upande wangu mimi siwezi kutongoza mwanaume, kwa sababu kama ananipenda angenitongoza kwa vile hajanitongoza maana yake hajanipenda.
 
Duuu

Malipo tena...!!!!! Yes huwezi kosa anayekupenda but mtima wako unaona haujigusi

It just happened tu nilijikuta nampenda tu toka nilivomtia machoni.....kuna siku akapiga simu....nilitetemeka sana....ha ha ha ha

Kuna siku akatuma sms.....nilivoona jina lake.....nilirukaruka, nikajigaraza kitandani bila kuisoma.....ha ha ha ha ha ha ha.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] nakuelewa vizuri sana, wengi tunapitia hii hali ila [emoji40][emoji40][emoji40]
 
Habari?

Umemwona mwanaume umempenda na unatamani awe mpenzi wako lakini yeye hana hata dalili ya kukutongoza , je ni sahihi kumtongoza? Au huwa mnafanyaje hadi ajue kuwa unampenda?

Asante.
Ukimuona tena jaribu kumuangalia straight ndani ya macho yake (usimlegezee macho, atakutamani tu).
mkikutanisha macho zaidi ya mara moja onyesha tabasamu la kweli(wanaume tunapenda vitu real), kuna kitu kitajengeka kwake.
Macho hayadanganyi, Automatic feeling zitaanza kujijenga zenyewe. Then mwambie do me a favor please
mfano: simu yangu inasumbua network, nisaidie kutatua.(Hata kama hana utaalam huo, automatic atajajaribu kukusaidia, Hiyo ni ishara nzuri hisia zake pia ziko na wewe).
Based from my experience
 
Mnaipenda kwa sababu mngekuwa hamuipendi mngekuwa mmeshaanza kuipinga kama mlivyopinga mila nyingine mbaya na mkafanikiwa
Mila zipi ambazo tumefanikiwa kuzipinga mkuu? Maana hadi leo mwanamke akifikisha miaka 28 hajaolewa jamii inaanza kujiuliza, tofauti na mwanaume, au mwanamke akiwa single mother jamii inamshambulia, lakini single father inamuacha!

Kwamba hizo nyingine nazo tunazipenda
 
Unakunywa kinywaji gani?
Mimi mwenyewe kuna kipindi nakuwa busy hasa.

Hata kula nakosa mda mpaka nasahau lakini siwezi kosa dakika moja ya kuwasiliana na babe.

Na yeye pia hivo hivo.

[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Kuna siku alivunja glasses [emoji483] alikuwa kaenda kununua glass sasa ile haraka ya kuwahi kuwasiliana na mie haraka haraka ya kushusha mizigo kwenye gari akavunja glass.

Mbaya zaidi ile siku nilijifanya kummind kachelewa kunijibu akanipigia picha ujue ninevunja glass kwa ajili yako we mtoto?

Mapenzi ni mazuri sana.
Umeona eeh!?!!
Yaani lazima mtu atapata tu Muda akutafute hata Kama ni muda kidogo Sana.

Amu story yako tamu,natamani uendelee[emoji23][emoji23][emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Natoa siri ya kambi.

Taka msaada kwake, midogo midogo yote ambayo unajua any stranger can try to help you.

Kama unamfaa, week haiishi usha tongozwa.
Mkuu kweli umetoa siri mojawapo ya kambi, nyingine usizitoe hiyo itamtosha!
 
Mila zipi ambazo tumefanikiwa kuzipinga mkuu? Maana hadi leo mwanamke akifikisha miaka 28 hajaolewa jamii inaanza kujiuliza, tofauti na mwanaume, au mwanamke akiwa single mother jamii inamshambulia, lakini single father inamuacha!

Kwamba hizo nyingine nazo tunazipenda
Mmefanikiwa kupinga mila na tamaduni mbaya dhidi ya mwanamke kama vile ukeketaji,mwanamke kunyimwa haki ya kusoma,mwanamke kunyimwa haki ya kuwa kiongozi,mwanamke kuolewa kwa nguvu,mwanamke kuolewa akiwa mdogo na kadhalika na sasa hivi mpo kwenye vita ya haki sawa
 
Natoa siri ya kambi.

Taka msaada kwake, midogo midogo yote ambayo unajua any stranger can try to help you.

Kama unamfaa, week haiishi usha tongozwa.
[emoji23][emoji23][emoji23]

Kuna mmoja alininunulia msosi njiani tulikuwa tunasafiri,, mwisho wa safari ikabidi nichukue # tu,

[emoji395]
 
Mmefanikiwa kupinga mila na tamaduni mbaya dhidi ya mwanamke kama vile ukeketaji,mwanamke kunyimwa haki ya kusoma,mwanamke kunyimwa haki ya kuwa kiongozi,mwanamke kuolewa kwa nguvu,mwanamke kuolewa akiwa mdogo na kadhalika na sasa hivi mpo kwenye vita ya haki sawa
Basi bado sana aise
Africa mwanamke bado anakandamizwa na bado hajafanikiwa kuchomoka
 
Back
Top Bottom