Mkereketwa_Huyu
JF-Expert Member
- Feb 19, 2011
- 10,590
- 7,951
Safi sana hii
Kwa kuongezea tu, niliwahi kumuuliza mke wangu kwa nini alikuwa hapendi kunisalimu wakati nilikuwa ninamuheshimu na kumsalimu kama wanawake wengine, akanishangaza kwa kusema eti alikuwa anaogopa nitamchunia na kama angenitongoza mimi ningemuona yeye kuwa malaya na alishazoea mchezo wa kutongoza wanaume. Akanishangaza zaidi kwa kuniambia kuwa aliwakataa wanaume wawili kwani alihisi iko siku nitamuoa au kutoka naye na alishamuomba Mungu niende kumtongoza, kwa kweli niliumia sana alivyoniambia hivi. Samahani ila ilinibidi nilie kidogo lakini si mbele yake, nililenda chooni. Nilimuhurumia sana mke wangu kwa kuwa jasiri wa kukaa na maumivu ya kunipenda wakati mwenzake sikuwa na hili wala lile juu yake, wanawake jamani msijiumize mioyo, jitokezeni kutongoza wanaume. Kuna wanaume wengine hawajuwi kutongoza kwani kutongoza si kila mtu anajuwa.