Wanawake: Ukimpenda mwanaume mtongoze

Wanawake: Ukimpenda mwanaume mtongoze

Nimeipenda hii uliweza kusoma alama za mrembo kukuzimia kila alipokuona.


Haikuwa ngumu kwangu kumsoma mke wangu kwani nilihisi kitu hicho maana kila aliponiona lazima aligeuka na kuniangalia ila nikimpa macho anakuwa na haibu.
 
Mapenzi ya mwanamke kumtongoza mwanaune huwa Hayadumu hata siku mojaaa...!!
 
Wanasema upendo una nguvu kama moto, una uwezo wa kumbadirisha mtu
 
Bad idea ever..... Wasichana zaidi ya 5 wamenitongoza directly from secondary school up to now bt wote hao mimi nimecheza nao tu nimewaacha tena sikudumu nao kwa muda mrefu.... Bora tu mfumo baba wa sisi kuwatongoza uendelee, utaishia kumuumiza na kutokumpenda..
 
Hivi kwanini mwanamke akimpenda mwanaume anapata shida sana ataanzaje kumwambia, mwanamke kikawaida akimpenda mwanaume anamuonesha 'signals' ishara ila ukiiona mwanaume haelekei kuja kukutongoza mfuate, anza kutongoza!

Na nyie wanawake pia mmeumba na hisia tena kali kuliko za mwanaume, ukimpenda mwanaume na kumuonesha ishara na kuona haelekei mfuate mtongoze!

Mimi hadi kuandika hii post kwa hili group ni mtoto wa kiume ambaye tangu utotoni hadi sasa hivi kote niliko pita nimekutana na wanawake wengi waliotokea kunipenda, baadhi walijitoa muhanga kuja kunitongoza kama 20% ila 80% walio baki waliishia kunionesha signal na kushindwa kunifuata.

Alafu wanawake mnanichekeshaga sana mkitokea kumpenda mwanaume na kushindwa kumwambia moja kwa moja utasikia, Bariki una macho mazuri, sijui una kifua, utasikia umependeza hata kama umevaa magunia, utasikia una akili hata kama ulipata division 0, yani atakupa sifa za kila aina na nyingine unakuwa hata hauna ila anakusifia tu ili apate attention yako kwake na ni sub conscious mind, anaweza fanya hivyo bila kugundua kama anafanya.

Wanawake mnanichekeshaga sana aisee Dah! Kwa ushauri wangu kwenu wanawake, ukimpenda mwanaume go straight mtongoze mwambie nakupenda, usianze kuzunguka zunguka na nyie pia mliumbwa na emotion tena kali kushinda hata zetu wanaume.
Duh pole kwa kula tongozo mkuu
 
Kwani wanawake wankupenda wewe au kitu chako, mwanume huwa anapenda mwanamke nje kwanza, mwanamke anapenda mwanaume ndani yaani uwe na kitu fulani kama ni pesa, kipaji au hata roho yake lakini sio housing yako, ila sisi wanaume tunataka housing kwanza. Hivyo ukiona mwanamke kakupenda ujue sio hauzing yako. Mwanaume kamili haangalii shepu ya mwili au sura yake, utaja liwa kiboga na wanaume wenzio kisa unasubiri kupendwa na mwanamke
 
Kwa kuongezea tu, niliwahi kumuuliza mke wangu kwa nini alikuwa hapendi kunisalimu wakati nilikuwa ninamuheshimu na kumsalimu kama wanawake wengine, akanishangaza kwa kusema eti alikuwa anaogopa nitamchunia na kama angenitongoza mimi ningemuona yeye kuwa malaya na alishazoea mchezo wa kutongoza wanaume. Akanishangaza zaidi kwa kuniambia kuwa aliwakataa wanaume wawili kwani alihisi iko siku nitamuoa au kutoka naye na alishamuomba Mungu niende kumtongoza, kwa kweli niliumia sana alivyoniambia hivi. Samahani ila ilinibidi nilie kidogo lakini si mbele yake, nililenda chooni. Nilimuhurumia sana mke wangu kwa kuwa jasiri wa kukaa na maumivu ya kunipenda wakati mwenzake sikuwa na hili wala lile juu yake, wanawake jamani msijiumize mioyo, jitokezeni kutongoza wanaume. Kuna wanaume wengine hawajuwi kutongoza kwani kutongoza si kila mtu anajuwa.
hadi nimetokwa na Machozi ya furaha.... Mungu awabariki
 
Wapuuzi tu wakitutongoza tukiwakubalia kifuatacho kizinga dadeki
 
Back
Top Bottom