Wanawake stress nyingine tunazitafuta

Wanawake stress nyingine tunazitafuta

Mmekaa sitting room mnaangalia taarifa ya habari, simu ya mr inaita, anaamka anachukua simu, ameamua kuongelea chumbani. Baada ya maongezi anarudi anakukuta mwanamke umeumuka kama umetiwa hamira, aliyepiga simu ni nani?

Kama ungetakiwa kumjua au kujua wanayoongea asingeenda chumbani, yeye ni mtu mzima anahitaji privacy yake. Kama anataka kukopa hela je?

Mimi ninaamini kama katika wote amenichagua mimi, hata akitoka wala sina wasiwasi ninajua atarudi. Simu ikipigwa ninampelekea kama yuko mbali, hata kama caller’s name ni Joyce siulizi kwani mwenye pete ya ndoa ni mimi.

Uache kulala usingizi wako mzuri unamsubiri mtu ambae yuko kwenye bata lake huko au ndiyo anashughulikia ada za watoto. Mradi tu awe na adabu ya kunijulisha kuwa atachelewa.
Leo ndio nimeelewa kwa nini Asprin upendo wake kwako hua hauchuji.
Yaani wanawake wote wangekua na akili kama zako hii dunia ingekuwa ni sehemu salama sana kwa ustawi wa maendeleo ya watu wake.
 
Mimi ninaamini kama katika wote amenichagua mimi, hata akitoka wala sina wasiwasi ninajua atarudi. Simu ikipigwa ninampelekea kama yuko mbali, hata kama caller’s name ni Joyce siulizi kwani mwenye pete ya ndoa ni mimi
Wadada na wanawake wengi wenye maono kama haya walifariki kwenye vita ya maji maji, ile ya muhenga Kinjekitile "Bokero" Ngwale. (RIP). Wachache sana waliobaki wakamalizwa wakati wa vita ya Uganda, ile ya Nduli Idd Amin Dada. Wewe umetokea wapi? 😛 😎
 
Nikwambie kitu hata ukimbana mwanamme akiamua kuchepuka atachepuka tu,atafanya yake mchana wa jua kali halafu saa kum na mbili yuko home, pia nadhani hadi mtu kuchepuka anakuwa kadhamiria toka moyoni mwake, hivyo bwana mie sihangaikagi kwa kweli
Ndiyo sasa kinachotakiwa ni kukemea tabia ya uchepukaji kwenye ndoa hizi kauli ndo zinawafanya waendelee kuchepuka niamini mimi
 
Hakuna anayetaka kushindana ila tatizo wanaume mnadhani ndoa bora ni ile ambayo mwanaume anafanya makosa kwa makusudi kila siku akitegemea mke wake atamsamehe na atamvumilia na mwanamke hafanyi makosa hata siku moja ndo ndoa mnazotaka hizo
Uangalie na vitu vya kuviita makosa. Yeye kaongea na simu chemba basi nawewe kesho unalipiza. Yeye last week karudi home saa 5 usiku nawe wasema week hii ni zamu yako. Hii mentality hii...tatizo ni kwamba hakuna trust. Humuamini...ndio maana. Be confident wewe ndio mwenye nyumba usibabaishwe na wapangaji. Hivi nyie mngekuwa wanaume mngeoa kweli?
 
Leo ndio nimeelewa kwa nini Asprin upendo wake kwako hua hauchuji.
Yaani wanawake wote wangekua na akili kama zako hii dunia ingekuwa ni sehemu salama sana kwa ustawi wa maendeleo ya watu wake.
Kwa kuwaacha mchepuke kwa uhuru ai ndiyo?
 
Shida sio makosa, usikae hapo nyuma kufuatilia hatua za mume. Umeagwa kwa amani mtu kaenda job, katoka lunch mmebonga. Yuko kijiwe na wana umeagwa na unahudumiwa freshi.

Sasa kazi ya kuanza kufukunyua simu ya mume bila ridhaa yake au kwa kificho ndio linalosemwa hapa ni kujitaftia matatizo bila sababu.

Na labda nikusaidie mume wa kukusujudia kama mtoto hayupo. Labda awe hajiwezi kiuchumi na hana nguvu za kiume sawasawa. Otherwise tafta hela ukamate boya umhudumie.
Nawashangaa sana hawa viumbe. You are right bro
 
Mmekaa sitting room mnaangalia taarifa ya habari, simu ya mr inaita, anaamka anachukua simu, ameamua kuongelea chumbani. Baada ya maongezi anarudi anakukuta mwanamke umeumuka kama umetiwa hamira, aliyepiga simu ni nani?

Kama ungetakiwa kumjua au kujua wanayoongea asingeenda chumbani, yeye ni mtu mzima anahitaji privacy yake. Kama anataka kukopa hela je?

Mimi ninaamini kama katika wote amenichagua mimi, hata akitoka wala sina wasiwasi ninajua atarudi. Simu ikipigwa ninampelekea kama yuko mbali, hata kama caller’s name ni Joyce siulizi kwani mwenye pete ya ndoa ni mimi.

Uache kulala usingizi wako mzuri unamsubiri mtu ambae yuko kwenye bata lake huko au ndiyo anashughulikia ada za watoto. Mradi tu awe na adabu ya kunijulisha kuwa atachelewa.
Akili kubwa,...ila umesahau kitu ki1...mwanamke mwenye akili tena wala haulizi maswal meng,anatafta ki ben10 cha kumpunguza ny.ege
 
Uangalie na vitu vya kuviita makosa. Yeye kaongea na simu chemba basi nawewe kesho unalipiza. Yeye last week karudi home saa 5 usiku nawe wasema week hii ni zamu yako. Hii mentality hii...tatizo ni kwamba hakuna trust. Humuamini...ndio maana. Be confident wewe ndio mwenye nyumba usibabaishwe na wapangaji. Hivi nyie mngekuwa wanaume mngeoa kweli?
Daah basi hapa ndo tunaposhindwa kuelewana mimi siyo mtu wa tit for tat yaani eti mwanaume akirudi saa nane na mimi nirudi saa nane akichepuka na mimi nichepuke? Never.

Ninachojaribu kusema hapa ni kwamba anapokosea ni lazima nimkanye kwa ustaarabu kama mke na siyo eti kumkalia kimya eti kwa sababu yeye ni mwanaume mkishapeleka magonjwa kwa wake zenu ndo mnawakumbuka na ndo mnataka kufia mikononi mwao dunia hii
 
Nikwambie kitu hata ukimbana mwanamme akiamua kuchepuka atachepuka tu,atafanya yake mchana wa jua kali halafu saa kum na mbili yuko home, pia nadhani hadi mtu kuchepuka anakuwa kadhamiria toka moyoni mwake, hivyo bwana mie sihangaikagi kwa kweli
Kwamba mtu akichepuka anakuwa kadhamiria toka rohoni hapana, that's not always the case. Muda mwingine anajikuta amechepuka tu kwa kuwa vishawishi vimemzidi nguvu
 
Back
Top Bottom