Wanawake stress nyingine tunazitafuta

Wanawake stress nyingine tunazitafuta

haya mambo ni mepesi sana ukiwa na moyo kwa kujituliza nafsi yako na ukiwa na uhakika kuwa u chaguo lake
 
Dada kuna michepuko haina adabu inatafuta hadi namba za mke na kumletea ubabe kuna mfano mmoja niliambiwa siku hiyo mke wa mtu amekaa ametulia zake ghafla namba ngeni inapiga kupokea kidada kinajitambulisha kama mchepuko wa mume wake halafu kwa kejeli kinasema eti "nina mimba ya mume wako" yule mke alitumia busara sana kumjibu akamuuliza kwa upole tu "kwani yeye mwenyewe umeshamwambia?" eti kakajibu "ndiyo anajua" mke akamwambia "sasa kama yeye tayari umeshamwambia anajua mimi unaniambia ili nifanyeje?" kenyewe kakaona aibu kakakata simu hii michepuko saa nyingine ndo ina kiherehere cha kutafuta namba za wake haya unakuta mume alikuwa anaficha ila mchepuko ukafichua hapo mke afanyeje jamani?
mimi kama naibu katibu wa chama cha michepuko Tanzania nitamkanya kwa kivunja katiba ya chama
 
Sasa kama kashapigwa chini tufanyeje, ni kumuombea pepo tu maana ni mwanamke wa shoka!
hapana kwa kweli hata Mungu alisema usimuache mwenzio akateketea kwa kutenda dhambi unatakiwa umkanye kile kitendo cha kumkanya tu umeshapata thawabu usimlazimishe aache wewe mkanye tu halafu yeye ndo ataamua afuate ushauri wako au auache

Sasa nashangaa wanawake wanaodhani kukalia kimya maovu ya waume zao eti ndivyo Mungu anavyotaka kwani waume zao siyo watu? My friend I will speak even if I see a text saying 'hi' as long as it is from a woman I will talk oooo chaeee
 
mimi kama naibu katibu wa chama cha michepuko Tanzania nitamkanya kwa kivunja katiba ya chama
Ah mimi ndo maana siwalaumu wale wanawake wa tit for tat japo mimi siwezi kuna wanawake wengine mume akimwaga ugali yeye anamwaga mboga mume akinywa beer yeye anakunywa wine na wapo ambao hizo mbinu zinafanikiwa mume ndo anaishia kuumia
 
Ah mimi ndo maana siwalaumu wale wanawake wa tit for tat japo mimi siwezi kuna wanawake wengine mume akimwaga ugali yeye anamwaga mboga mume akinywa beer yeye anakunywa wine na wapo ambao hizo mbinu zinafanikiwa mume ndo anaishia kuumia
We kwa lawama hizi unaachaje kuwa tit for tat! sema approach tu zinatofautiana ila kununa nuna haikwepeki kama paka wa kirusi!
 
Back
Top Bottom