Wanawake stress nyingine tunazitafuta

Wanawake stress nyingine tunazitafuta

Hamna anayefanya kosa makusudi
Kucheat ni bahati mbaya? Kuchat na wanawake tofauti na mkeo kimahaba ni bahati mbaya? Hivi vitu vina process ndo maana tunawashangaa mnavyosemaga ni bahati mbaya

Bahati mbaya maana yake kitu kimetokea ghafla bin vuu siyo utongoze wanawake huko uhonge hadi ukubaliwe mkubaliane kukutana sehemu mfanye yenu halafu useme ni bahati mbaya? Jamani Mungu anawaona mjue
 
hakunaga kitu ka hio
Ndiyo hizo ndiyo ndoa mnazozitaka ila mnashindwa tu kusema mnataka kuoa wanawake ambao hata wakiona mnaingiza vimada ndani ya nyumba yenu wasiulize chochote

Wakae kimya wawasamehe na wawavumilie tu mnataka wanawake kama malaika ambao hawafanyi makosa hata siku moja

Yaani kila unachomwambia anakubali na anatekeleza mara moja bila kupinga wala kuhoji chochote ikitokea kakosea kidogo tu unamtishia kumsaliti au kuoa mwanamke mwingine au kumuacha au unaamua kumpiga

Na ukishamuumiza yeye ndo anakuomba msamaha ndiyo wanawake ambao wanaume wengi wanawataka hao na wanawake wa aina hiyo wanaonekana ndo wife material asipokuwa hivyo anaonekana anapenda haki sawa kushindana na wanaume na hafai kuolewa
 
Hujui kwamba sisi ni wadhaifu. Na pia tunataman??? Mnatakiwa mvumilie na muache kufatilia fatilia mtakufa siku kabla ya zenu
Hiyo dunia unayoiota haipo na haitakuja kuwepo amka tu kwenye hiyo ndoto ndugu yangu yaani huoni hata aibu eti nyie ni wadhaifu ingekuwa hivyo basi Mungu angeshawaruhusu mtende dhambi lakini ndo katukataza wote kutenda dhambi

Halafu mkae mkijua duniani hakuna mkamilifu siyo wanawake siyo wanaume wote tuna mapungufu sasa kaa hapo endelea kudhani wanawake ni malaika hawatakiwi kukosea utadhani shetani huwaga anawatendesha dhambi wanaume tu
 
haiko hivyo...mtu mstaarabu atawajibika kwa makosa yake ila bahati mbaya wanaume wengi wanafeli ha
Basi ndo mkubali sasa kwamba mnafeli na siyo kuendelea kujitutumua na kujiona kuwa mko sahihi eboo
 
What about serial cheaters? Unaitaka ndoa, unampenda sana na ushamwambia hupendi baadhi ya vitu ila wala hana mpango wa kubadilika? Nasema hivyo because nilikaa kwenye ndoa 8 years sijawahi hata siku moja kufungua simu ya mume wangu, wala hajawahi hata kunipa simu nipige picha hata za matukio ya kawaida... but here I am, no husband 😀😀. Of course his LOSS! but my point ishuwa najiambia kama ningekuwa namkagua ama namfanyia vurugu kidogo labda angeogopa, or maybe ningejua mapema wapinzani wangu! Nimekuja kushtuka wameshazaa watoto wawili uhawara uliokubuhu ndio wanakumbuka kuoana.😀
Dah pole sana mkuu, hilo ni pigo takatifu. Kama bomu basi Hiroshima
 
mwili mmoja kitandani tu
Aisee nimeitafuta hiyo sehemu palipoandikwa watakuwa mwili mmoja kitandani tu nimeikosa hebu nisaidie basi imeandikwa wapi yaani kitabu gani sura ya ngapi na mstari wa ngapi?
 
What about serial cheaters? Unaitaka ndoa, unampenda sana na ushamwambia hupendi baadhi ya vitu ila wala hana mpango wa kubadilika? Nasema hivyo because nilikaa kwenye ndoa 8 years sijawahi hata siku moja kufungua simu ya mume wangu, wala hajawahi hata kunipa simu nipige picha hata za matukio ya kawaida... but here I am, no husband 😀😀. Of course his LOSS! but my point ishuwa najiambia kama ningekuwa namkagua ama namfanyia vurugu kidogo labda angeogopa, or maybe ningejua mapema wapinzani wangu! Nimekuja kushtuka wameshazaa watoto wawili uhawara uliokubuhu ndio wanakumbuka kuoana.😀
Huyo mjuba kweli alikuwa serial kabisa, yani kama silaha ni lethal weapon. Sema tuongee yote ila mapenzi ya kibongo bila u FBI ni kitendawili.
Dont ever love blindly in.Tz
 
Mimi nadhani sky ameshazeeka
Ndio maana Hata caller ya Joyce hamaindi
Hivi angekuwa na mwaka katika ndoa na kitumbo kimejaa simu ikaita caller ni Joyce naamini angelia Hadi kujifungua
Ukifikia level ya uzee wivu unapungua
Unaona "hakuna jipya tena".
 
Back
Top Bottom