Wanawake stress nyingine tunazitafuta

Wanawake stress nyingine tunazitafuta

Afu unakuta kwenye kibanda umiza wanaume kama wote, mwanamke mmoja tu, kwenye saa tano hivi. Hadi uelewi huyu nae vipi. Kumbe
Ni wivu tu
Ni wivu tu
Hatari sana mpaka unaamua kukatiza mechi na huangalii tena!
 
Nashukuru wewe umenielewa wengine wanang'ang'ania kuwa naleta ushindani na wanaume yaani hivyo ni vitu viwili tofauti wao wanadhani kuwa mwanaume ni kuwa kinyume na mke wako kwenye kila kitu na kumkosea mke makusudi ili umpime uwezo wake wa kusamehe na kuvumilia
Hapo ndo wanapokosea, maisha hayapimwi kabisa, maisha unaishi. Usichopenda kufanyiwa nawe usimfanyie mwenzako.
 
Hapo ndo wanapokosea, maisha hayapimwi kabisa, maisha unaishi. Usichopenda kufanyiwa nawe usimfanyie mwenzako.
Hakika yaani kumbe wanaume kama wewe bado mpo dunia hii? Nilishaanza kukata tamaa kutokana na comments za baadhi ya wanaume humu Extrovert Meraki Nyalotsi Relief Mirzska njooni msikie nilichokuwa namaanisha siyo nyie mlichokuwa mnang'ang'ania oohh kushindana kushindana
 
Sijawai fanya hayo mambo.Yani mwanaume ata akitaka akaongelee nje kabisa sitamuuliza alikua anaongea na nani.Huwa na assume hakutaka niskie mazungumzo yao so siwezi muuliza.
 
Mmekaa sitting room mnaangalia taarifa ya habari, simu ya mr inaita, anaamka anachukua simu, ameamua kuongelea chumbani. Baada ya maongezi anarudi anakukuta mwanamke umeumuka kama umetiwa hamira, aliyepiga simu ni nani?

Kama ungetakiwa kumjua au kujua wanayoongea asingeenda chumbani, yeye ni mtu mzima anahitaji privacy yake. Kama anataka kukopa hela je?

Mimi ninaamini kama katika wote amenichagua mimi, hata akitoka wala sina wasiwasi ninajua atarudi. Simu ikipigwa ninampelekea kama yuko mbali, hata kama caller’s name ni Joyce siulizi kwani mwenye pete ya ndoa ni mimi.

Uache kulala usingizi wako mzuri unamsubiri mtu ambae yuko kwenye bata lake huko au ndiyo anashughulikia ada za watoto. Mradi tu awe na adabu ya kunijulisha kuwa atachelewa.
Nilikua nasoma kama guest ila hapa nimelazimika ku log in.....
Kama wanawake wote wangekua na mtazamo kama huu wallah dunia ingekua mahala salama sana pa kuishi.Halafu msichokijua nyie mkiacha kufuatilia fuatilia huwa tunaingia wenge flani,kuna hali mtu anajjistukia.
Aisee,kuna watu wana bahati sana
 
Hakika yaani kumbe wanaume kama wewe bado mpo dunia hii? Nilishaanza kukata tamaa kutokana na comments za baadhi ya wanaume humu Extrovert Meraki Nyalotsi Relief Mirzska njooni msikie nilichokuwa namaanisha siyo nyie mlichokuwa mnang'ang'ania oohh kushindana kushindana
Kwani unadhani mimi sikuelewi?? Nakuelewa vizuri tu ila kuna namna flani nashindwa kuanza kuzozana nawe
 
Back
Top Bottom