Wanawake sasa wakiachika wanasema walikua wananyanyaswa

Wanawake sasa wakiachika wanasema walikua wananyanyaswa

The Evil Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
6,147
Reaction score
20,085
Nashangaa sana siku hizi wanawake wengi wakiachika wanasingizia walikua wananyanyasika. Mfano ni hawa mabinti Lady JD, Frola Mbasha, Shamsa Ford nk. Siku chache kabla ya kuachika walikua wakiwasifia waume zao kwamba ni wanaume wazuri na wanaowajali, wanaowapenda.

Lakini mara tu baada ya kuachika wanaleta malalamiko kwamba walikua wananyanyasika. Siku chache kabla JD, Mbasha hawajaachika walikua wanasema kwenye vyombo vya habari kwamba wanaume wao ndio wanaume bora lakini baada ya kuachika tu wametoa tuhuma mpya kwamba walikua wanapigwa, kunyanyaswa kijinsia nk.

Wanawake kwa nini mkiachika mnatunga shutuma mpya kwa waune wenu, kwanini ni kawaida kwa mwanamke kuachika na kuanza kumsema vibaya mpenzi wake wa zamani, utasikia kwanza alikua hanifikishi, mara alikua hanijali wakati umekua nae kwa zaidi ya miaka 10.

Hii mnalionaje ndugu zangu
 
Wao ndio wanajua changamoto wanazo pitia katika familia zao, hata hvyo wanawake wengi ni wavumilivu wanapitia mambo magumu xana ktk ndoa.
 
Sasa kama walikua wananyanyasika wasiseme? Halafu huwezi rusha mawe nyumba ya vioo ukiwemo ndani
 
So vale mnasubiri mkitoka nje ndio mnasema!! Kwa nini msipiganie haki yenu mkiwa ndani?

Nikiwa ndani kwako nakua zoba,unayonifanyia yote nachkulia poa ila ninapochoka zaidi na kuamua kutoka nje ndipo mawazo mengine yanapata nafasi
 
nikiwa ndani kwako nakua zoba,unayonifanyia yote nachkulia poa ila ninapochoka zaidi na kuamua kutoka nje ndipo mawazo mengine yanapata nafasi

Zoba!! Muda huo akili mnaziweka wapi? Hii ni asili yenu vale, utamkuda mdada anapiga kelele weee baada ya muda unamkuta karudi kuomba msamaha hahahahahhh.
 
Huwa hata Mimi Inashangaza sana kwa hili....
 
Hamna huwa wanatafuta huruma na pia waonekane wanyonge. Hiyo ni inferiority complex yao kubwa ya kutafuta huruma na kujikosha. Unaweza kuta wao ndio chanzo cha mtafaruku
 
Alafu wanakuja na madai eti wame zao waliwalazimisha 713
 
The Unknown

Wanawake siyo watu wakawaida wew waache hivyohivyo hata wakilalamika achana nao
 
Last edited by a moderator:
Ukitaka ujifunze saikolojia ya wanawake hutamaliza syllabus na utafeli tu. Wewe ishi nao kwa akili tu...so does the bible say!
 
Yule wa sugu naye anasema alikuwa akipigwa na kunyimwa pesa ya matumizi. wanawake wakitoka kwenye ndoa mazuri yote wanasahau wanaanza kutangaza mabaya tu, mpaka mtu unajiuliza hivi miaka yote hakuna hata moja jema la kusema yeye anaona yote mabaya tu
 
Ukitaka ujifunze saikolojia ya wanawake hutamaliza syllabus na utafeli tu. Wewe ishi nao kwa akili tu...so does the bible say!

Na ukitaka ujifunze saikolojia ya wanaume hutamaliza syllabus na utafeli tu na ndio maana tunaishi na wanaume kwa akili NB kutokana na kusomana huku tutaendelea kunyatiana mithili ya paka mawindoni na kuendelea kupimana kama mafuta ya kibaba dukani kwa bwashee or mpemba
 
Wanawake ni natural waigizaji

wanavyoweka status za facebook na watsaap kumbe wako kwenye moto
hadi waachike tena in most cases mwanaume ndo kamuacha ndo unakuja shangaa....
kumbe yoote yalikuwa maigizo
 
Human psychology is difficult but women psychology is the most.
Ukweli uko hivi "we live in the world of no fair, mwanaume akisema mke wangu ana tabi hizi na zile huwa anaonekana anamdhalilisha mkewe/mwenza. Ila mwanamke akisema kuhusu mumewe aah ni kweli alikua ananyanyasika.
Dunia hii Wanawake ndio wangekua wanaume (in terms of responsibilities) tusingeishi.
 
Wanawake ni natural waigizaji

wanavyoweka status za facebook na watsaap kumbe wako kwenye moto
hadi waachike tena in most cases mwanaume ndo kamuacha ndo unakuja shangaa....
kumbe yoote yalikuwa maigizo

Usipime..
 
Human psychology is difficult but women psychology is the most.
Ukweli uko hivi "we live in the world of no fair, mwanaume akisema mke wangu ana tabi hizi na zile huwa anaonekana anamdhalilisha mkewe/mwenza. Ila mwanamke akisema kuhusu mumewe aah ni kweli alikua ananyanyasika.
Dunia hii Wanawake ndio wangekua wanaume (in terms of responsibilities) tusingeishi.

Ahaaaa nshajua tatizo lako rejea picha ilioweka kwenye avatar yako
 
Back
Top Bottom