Wanawake pitieni hapa

Wanawake pitieni hapa

Dam55

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2015
Posts
5,669
Reaction score
12,044
Kwanza kabisa nawasalimu wapendwa, kila mmoja apokee heshima yake.

Leo naomba niwashirikishe jambo hususani ni dadazetu, mnajua tunawapenda sana na tunawaheshimu na kuwapa nafasi kubwa katika jamii japo mnaonekana ni viumbe duni lakini si kweli ninyi mnanguvu sana kuliko sisi na kuanzia sasa nawataka usijidharau.

Haya ni mambo machache sana yanayoshusha heshima yenu nakuonekana si lolote nifuateni kwa makini kisha mchukue hatua.

1; UTEGEMEZI.
wanawake mmekuwa na tabia ya utegemezi kwa wanaume katika maswala ya kiuchumi. Wengi wenu hamtaki kuwajibika bali mnategemea matunzo kutoka kwa wanaume
ni ukweli ulio wazi wanaume usipo toa matunzo kwa mwanamke hamta fika mabili, ni jukumu la wanaume lakini mnapo liendekeza linapelekea kushuka kwa thamani yenu na kuuendeleza mfumo dume.( usitake mwanaume akuoe ili akutunze.) kwa wale wasio wawajibikaji wabadike watayaona matokeo chanya mke mwenye kipato chake mume hawezi kumdharau.

2; JIWEZESHENI.
kuna ile kauli " mwanamke akiwezeshwa anaweza" msemo huu wengi mmeukalili lakini unakulemazeni. Sio lazima mafanikio yako yawe na mkono wa mwanaume, mnao uwezo wa kusimama wenyewe na mkafanikiwa kama elimu ni ruhusa kwa wote, tumia elimu yako uliyo nayo kujiwezesha.

3; MWANAMKE NI KICHWA PIA.
Sio kweli kwamba wanaume tunawazidi akili, hakuna kitu kama hicho hata ninyi mnaakili vilevile.
Unaposema mwanaume ni kichwa je mwanamke ni shingo?? na kama mwanamke ni shingo je kichwa bila shingo kitakaa?? kwa maana hiyo hata mwanamke anafaa kuwa kuchwa.(kuwa kiongozi wa familia, biashara na utawala)..

4;MSIWE NA TAMAA NA MALINGO;
Tabia ya tamaa inapelekea matumizi mabaya ya muda wako wa kujituma, malingo yanapelekea kupoteza fulsa mbalimbali. wanaume wameigundua siri hii ndio maana wanafanikiwa.
Usiwe na tamaa ya kupata vitu haraka bali unatakiwa kupambana tena kwa mateso huku ukitumia vizuri fulsa unazozipata. wanaume wakaja na msemo "fanya kazi kama mtumwa uishi kama mfalme" mwanamke usikimbie mateso bali kabiliana nayo.

5;MATUMIZI MABAYA YA UJANA WENU.
Ni wanawake wachache sana wanaotumia vizuri kipindi cha ujana wao kutengeneza maisha yao ya badae.
wengi wanadanganywa na uzuri na urembo wa ujanani na masifa wanayomwagiwa na wanaume.
mwanamke anapokuwa na umri wa 20yrs ukimuuliza unataka mume wa namna gani atakwambia mwenye gari,nyumba,pesa n.k. akifikisha miaka 30 ukimuuliza tena atakwambia anataka mume muaminifu na mchamungu. Akifika miaka 45 ukimuuliza hapo atakwambia yeyote tu ili mladi mume.
Hii yote ni kwamba mnadanganywa na uzuri wa ujanani bila ya kujiwekea malengo ya mbeleni. Usisubiri uwe na umri mkubwa ndo uanze kuhangaiaka tumieni vizuri ujana wenu.

6; MSIWE DHAIFU WA MAPENZI.
kwanini unakubali kuolewa kuwa mke wa pili au wa tatu?? huoni kama unajishuaha thamani ndio maana wanaume wanajigamba kuwa wao ni vidume na hawawezi kuwa na mke mmoja. Kwasababu ninyi wenyewe mnakubali kulundikwa kama mbuzi zizini.Mbaya zaidi mnatupiana maneno "utaachika" "tutabanana hapahapa" huku lidume lipo ndani linawasikiliza na kuzidi kujipandisha chati tu.
hebu amkeni kwenye huo usingizi wanawake.

Ninyi si viumbe duni mnanguvu sana tena kutuzida ukitumia akili vizuri mwanaume hana neno mbele ya mwanamke ila mnajiporomosha wenyewe.

Yapo mengi ya kuwaambia ila kwa leo naishia hapa.

MFUMO DUME MTAUONDOA NYINYI WENYEWE KWA MAAMUZI YENU YENYE MAANA ILA MKIJIBWETEKA MTAENDELEA KUWA CHINI YETU DAIMA.
(WANAWAKE NI JESHI KUBWA MKIAMUA VITA MNAIWEZA)
 
1478490877852.jpg
 
; UTEGEMEZI.
wanawake mmekuwa na tabia ya utegemezi kwa wanaume katika maswala ya kiuchumi


Tumeagizwa kuzaa sio kula kwa jasho
Ni kweli mkuu ila hali ilivyo kwasasa watu hawakumbuki hilo bali wanatumia nafasi hiyo kuwadharau.
Atakuheshimu vipi ikiwa wewe ni mtu wa kula kulala?
 
Duu! Punguza ukali wa maneno basi! Halafu tafakari upya nafasi yako as man
 
Hawatakuelewa. Watakimbilia kusema waliagizwa kuzaa kwa uchungu. Ilihali wengine wapagani
mkuu, sasa kama ni hivyo basi wasilalamike kutawaliwa na wanaume kwa sababu Imeandikwa pia HUYO MWANAUME ATAKUTAWALA NA TAMAA YAKO ITAKUWA KWA MUMEO.
Njia pekee ya kuwatoa hapo ni wao kujitegemea
 
Nakubaliana Na wewe kasoro tu hapo kwenye 'malingo'
Mwanamke ameumbiwa kuringa bwana. Kuringa kunatuponya Na mambo mengi. Mwanamke anaeringa ni nadra sana kutapeliwa, sio tu mapenzi hata pesa pia.
Sawa ila uwe makini maringo hayo yasipunguze uwajibikaji wako.
Alafu kumbuka maringo ni chanzo cha kukosa umakini
 
mkuu, sasa kama ni hivyo basi wasilalamike kutawaliwa na wanaume kwa sababu Imeandikwa pia HUYO MWANAUME ATAKUTAWALA NA TAMAA YAKO ITAKUWA KWA MUMEO.
Njia pekee ya kuwatoa hapo ni wao kujitegemea
Kulalamika wameletewa [emoji23]. Ingekuwa sio presha ya nje wasingelalamika.

Wewe huoni wanalalamikia nje kwenye mikutano ya TAMWA ila Mkiwa ndani wawili ndani ya nyumba ni kimya.
 
Back
Top Bottom