Ushamtamani House girl hapo unatafuta sababu tuKwa hali hii hamasa itakuwepo? Hakika yatabakia mazoea tu
Kuna wanawake ni warembo sana wakiwa hawana make up, yani toto limesuka twende kilioni lakini roho yako inasuuzika.
Asante mama D kama nimekugusa. Huu ujumbe nitamfikishia hakikaNchi Kavu naomba umfikishie wife huu ujumbe kama ulivyo. Inawezekana anadhani akipendeza huwa huoni au huvutiwi
Mapenzi ili yawe matamu na kudumu hayataki mazoea... yanataka kufanyiwa kazi kila muda na pande zote mbili
Umeniamsha usingizini sasa ngoja na mimi niondokane na mazoea nianze kujipodoa hata jioni😃😃😃
Ukiona hivyo jamaa hajachangia hela ya Saluni.
Asante BAK kwa ushuhuda huu. Tena bahati mbaya huwa hawawasikilizi wenzi wao. Atabadilika kwa kuambiwa na mtu wa pembeni, kama ulivyofanyaNiliwahi kumchana rafiki yangu KE aliyewahi kuwa office mate. Huyu dada tulikuwa ni marafiki wakubwa sana hadi ndugu zake wote na wazazi wake walinifahamu na kuniheshimu kama ambavyo mimi niliwaheshimu. Nikaacha kazi pale naye akawa ameacha lakini urafiki wetu haukufa. Akasikia nimetoka zangu bush niko MUJINI hivyo akanialika kwa lunch. Mumewe tunafahamiana sana na tunaheshimiana sana tu.
Basi nikafika pale nikamkuta na mama yake mzazi tukapiga story kisha msosi ukawekwa mezani tukajichana. Baada ya kula nikaaga na yule dada kunishindikiza. Basi ile tuko wawili nikaanza “umepatwa na kitu gani mbona umejiachia hivi?” “Kwanini nyumbani kwako unakuwa nyuku nyuku kama house girl?” “Wewe ni mtu unayejipenda sana lakini kwako umevaaa kisempele kimechoka sana Nywele zako nzuri umezifunga na kilemba kilichochoka sana” “Hivi unadhani mumeo akirudi kutoka kazini akikukuta hivi atakuwa na hamu hata ya kukugusa?” “Si bora tu awe na mchepuko wake anayevutia na havai visempele kama wewe na kuficha uzuri wale?”
Akainamisha kichwa kama dakika tano hivi. Ule ukimya nikajua nimeshapoteza rafiki yangu wa miaka mingi.
Akasema ahsante sana nashukuru sana. Tumegombana sana na hubby kuhusu issue hii kuliko issue nyingine yeyote ile. Naona kuna kila sababu ya kujirekebisha.
Ukweli ni kwamba KE wengi waliokuwa kwenye ndoa wanajisahau sana kuhusu kupendeza na kuwa maridadi wanapokuwa majumbani mwao na hii husababisha ME wengi kwenye ndoa kuanza kuangaza angaza huku na kule kutafuta warembo.
Hakika hili nalo neno. Ila ni ubinafsi uliopitiliza hasa ukifikiria ni vingapi unachangiaUkiona hivyo jamaa hajachangia hela ya Saluni.
Kwa hiyo shoo ambayo haujalipia haiwezi kukuburudisha.
Sisi wanawake ni zaidi ya mtujuavyo.
🤣🤣🤣