Wanawake na umbea wa saluni

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
14,893
2,000
Kwenye Saluni nyingi za wanawake, mazungumzo mengi yanahusu maisha ya watu na hasa kuhusu mapenzi na kipato, kashfa na saikolojia zisizo rasmi kuhusu ndoa na uhusiano.

Kuna mazungumzo ya kukatishana tamaa na kuumizana zaidi, kwa sababu kila mmoja anajaribu kuonyesha kwamba ana nafuu fulani.

Lakini mbaya zaidi ni kwamba, saluni za wanawake hutumiwa na wanawake hao kama maeneo ya kusemea hisia zao chungu na kutoa jumuisho kuhusu wanaume na uhusiano.

Huko saluni hakuna wataalamu, bali kuna wazungumzaji ambao wanaamini wao ni wataalamu, na wengine kwa sababu ya kuzidiwa na mzigo wa matatizo hasa ya uhusiano na pengine ya kipato, huwaaamini hao wataalamu wasio rasmi.

Huko saluni ndiko ambako wanawake wanaambiana`kwamba, mwanaume akiacha kufanya tendo la ndoa kwa wiki moja na mpenzi wake, ni lazima mwanaume huyo atakuwa na ‘nyumba ndogo.’ Ndiko ambako wanafundishana kwamba, ukipata Mganga wa nguvu unaweza kumshika mwanaume.

Ndiko huko ambako hutajwa orodha ya wanawake ambao wamewashika waume zao kupitia kwa waganga. Ndiko huko ambako majina ya waganga maarufu hutajwa.

Lakini ndiko huko saluni ambako, wanawake hutaja orodha ya wanawake wenzao waliopata mali kupitia ‘mabuzi,’ ambao huwapa mitaji ya biashara inayowawezesha kusafiri hadi Uchina.

Pia hutajwa majina ya wanaume wanaohonga sana. Ni saluni ambako wataalamu wasio rasmi hutoa suluhu ya matatizo ya ndoa.

Ndiko ambako wataalamu hao huwaambia wanawake wenzao kwamba, ukimuonyesha mwanaume kwamba unampenda sana, atakudharau na kukuacha. Kwa hiyo mwanamke akitoka saluni anakuwa ametoka shule anayoiamini. Ambapo huacha kumwonesha mumewe kwamba, anampenda. Ni wazi shule hii ya saluni haijui kwamba, unapoonesha kutokupenda, nawe utaoneshwa kutokupendwa.

Kwani unachopanda ndicho unachovuna. Wakati mwingine shule hii inajua jambo hilo, isipokuwa inataka waliopotea na kuharibikiwa wawe wengi.

Ni huko saluni ambako utasikia wanawake wakifundishana namna ya kuwadanganya wanaume zao.

Hufundishana namna ya kujenga nyumba bila kunaswa na mume, kwani wanaume hawaaminiki, huwezi kuacha kujiandaa. Lakini shule hii haijui kuwa, hiyo ni sumu kubwa kuliko sumu nyingine kwenye ndoa, kutafuta mali na kujenga msingi wa kipato kwa siri.

Ni hukohuko saluni ambako wanawake huambiana uongo kuhusu wakwe, watoto wa kambo, na mawifi.

Hufundishana kwamba, kumpenda mama mkwe au wifi ama mtoto wa kambo ni kutafuta muhali. Haiishii hapo huendelea kufundishana hata namna ya kuwachukia watu hao.

Mwanaume, kama ukiona mwenzi wako anakwenda saluni na akitoka huko amekuwa mtu mwingine kabisa, unapaswa kujua kwamba, huenda amepata ‘dozi’ ya wataalamu hao.

Wanawake, nawashauri jihadharini sana na maneno ya saluni. Kwani katika kila maneno mia moja, ni moja tu linalokaribia ukweli.

Kumbuka, linalokaribia ukweli sio kuwa ni la kweli……
 

feitty

JF-Expert Member
Jul 10, 2015
2,021
2,000
Bila kusahau ukienda pale utachangia mada na kujiunga nao katika stories ila ukitoka tu unageuzwa main topic.
Ndio mana kukaa kimya na kusikiliza ndio naona bora.
Labda kama saluni umeizoea na watu wake umewazoea.
Saluni umbea hautokaa uishe.
Kuna habari ukizisikia unabaki mdomo wazi mana mwingine anasemwa mtu halafu unajikuta unamjua.
Wakati mwingine wanasemana wao kwa wao hasa mmoja wao akiwa hayupo.
Tabu tupu
 

cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
24,812
2,000
Ha ha haaaaa

Wanaongelea mabwana zao ovyo ovyo kwa watu wowote hawafai kabisa.

Ndio maana wengi wanashangaa wanaachwa na kutokumbuka midomo yao walipooachia, waliowasikia walisaka bwana na kubeba.

Esp tabia ya kuponda mwanaume ndio eeeeh, lazima abebwe kwa maswali ya mpindo huku huji unatoa taarifa za wapi anaweza kupatikana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom