Unastahili pongezi mama, wewe ni wachache kati ya wengi akina Cynthia Chriss...Umenikumbusha wakati nasoma driving school somo la riverse ilikuwa mtihani ila now days naweza rudi nyuma kwa kuendesha barabara yote ile ya samora niko fit God knows.
we ni mrembo kuzidi hawa?
View attachment 183687
wanawake wenye mawazo finyu kama wako ni wale wasio active, kwa ligha nyingine tunawaita "nyenyenye", hata akikaa jikonni anapika kila kitu anamtuma dada wa kazi, kuchukula mwiko tu.."halima nipe mwiko, halima nifungie hilo bomba, halima nifanyie nivue soksi"! wapo wanawake wa shoka ninawafahamu wengi sana, na hizo pesa wanazo na wanachapa kazi ukimkuta hana mchezo yuko mstari wa mbele kuonesha mfano, dereva wa basi lake akimzingua ananyang'anya funguo anapiga gia mwenyewe, lakini asilimia kubwa ni nyenyenye tu..eti kubadili taili ya gari atachafuka, wanaume hatuchafuki?..au wanaume hatuna pesa?! mwanamke wa kweli ni mwenye kujiamini, kujiamini ni pamoja na kukataa unyenyenye!
Unastahili pongezi mama, wewe ni wachache kati ya wengi akina Cynthia Chriss...
1. tie rod end/ball joint etc ikikatika sio mwanamke tu hata mwanaume huna ujanja,utapaki pembeni utaita wenye kazi yao....fundi labda wewe mwenyewe uwe fundi magari.
2.pancha inahitaji uzoefu,kuna wanaume wanapata pancha nao hawajui mpaka unamshtua kwahio unahitaji kauzoefu fulani kuhisi mabadiliko kwenye gari yako na si kila mtu ana uwezo huo.
kuna wanaume wengi tu hawawezi kubadili tairi,wakipata pancha utawaonea huruma wanavyohangaika wakikosa mtu wa kuwatolea....
Hahahah ushachelewa sana....
umeongea muzuri sana, kula 5
Hainihusu coz gari lenyewe sina
siyo lazima uwe nalo, siku ndugu yako yuko hoi anahtaji kupelekwa hospital na gari iko flat utashindwa kubadili tairi umpeleke hospital nduguyo kisa utachafua kucha?!!
Wanawake wengine wanachefua sana dada, utakuta yeye kila kitu anachechemea tu, mtoto kakojoa anavyonyanyua dekio utafikiri kashika mkia wa nyoka, kufuta anatumia mguu, kisa una pesa, unapesa za kumzidi oprah wewe?!! kujitegemea ni kujiamini, kujiamini ni pamoja na kuwa active, unapiga starter asubuhi haijibu unashindwa hata kufungua bonnet mpaka usubiri saa nzima mtu aje kukuchekia?!!! napenda sana wanawake active.
Mkuu uko sahihi ila wanawake wengi hawajishughulishi kufahamu vitu vidogo vidogo kuhusiana na magari.
Nafahamu wengi tu hata kucheki kiwango cha engine oil, au maji hawajui!
Wengine hawaelewi kila taa ya tahadhari kwenye dashboard inahusiana na nini. Anaweza akawa anaendesha bila wasi wasi wakati taa inaonyesha joto la ongine liko juu!
Wanahitaji kubadili attitudes na kijifunza mambo ya msingi kuhusiana na magari!
I am here dear... watu8 ni ndugu yangu so nlimruhusu kuja kukusalimu tu baasi.. kwani alisema mengine?