Simplicity.
JF-Expert Member
- Dec 19, 2013
- 2,636
- 1,661
Wakuu, nafuata ule msemo kuwa kama una silaha, hata bomu la maangamizi na adui anakusumbua, wewe tumia tu, kwa hiyo ni ujinga kuwa na ulimbo lakini ndege wanakusumbua na wewe unawaangalia.
Sasa naona wanawake wamepanda tena daraja, hasa hawa wa mjini Dar, kuna vigari vyetu hivi kama corolla, vits, etc., naona siku hizi wanaviona kama maguta tu, nani kawafundisha, sijui! Duh, hali ni mbaya.
Mwezi uliopita nilikuwa sehemu mjini kwenye mkutano, sasa ikawa mida ya jioni mkutano umeisha ndio tunatawanyika. Kuna mdada mmoja, nikaona anahaha namna gani ataenda nyumbani, mie nikawa msamaria mwema kwa kumwambia, si tunaenda njia moja, twende nikupe lift, duh, akajibu "kwa usafiri gani, aku", huyo akawa ameishia, mara akaenda kupanda gari ya jamaa mwingine! Kwa sababu nilipata kizunguzungu kutokana na jibu lake hata sikujua alipanda gari ya aina gani.
Sasa wanawake wa mjini naona kila siku mnapanda bei, mnapenda gari gani? Ili nami ninunue tuheshimiane.