Samahani kwa wale mtakaokwanzika na maneno yangu japo najua sina lengo la kumkwanza mtu. Humu ndani memba wote naamini ni watu wazima na wenye heshima za kutosha, lakini mtu akileta Uzi wake kama huwezi kuchangia bora unyamaze kuliko kutoa matusi, binafsi nachukizwa sana na matusi na huwa sipendelei kunyamaza pale ninapohisi natakiwa kusema jambo linaloniumiza.
Nimekuwa nafuatilia sana namna tunavyochangia mawazo na ushauri kwa mwenzetu anaehitaji mchango wetu kimawazo. Nashukuru Mungu kuna watu humu wana busara na siku zote hutoa majibu yenye staha njema kabisa na kwa moyo wangu wote huwa napenda kuwapongeza.
Swali hivi matusi kwa jamii yetu ni sehemu ya maadili au malezi mabovu? Lakini pia tukisema malezi bado tutawakosea wazazi wetu maana huenda wazazi waliwajibika ipasavyo ila pear group au bangi na madawa ya kuvuruga akili ndio sababisho? Naomba tubadilike wana JF na kama huwezi kuchangia kwa maneno ya busara sio lazima uchangie. Samahani kama ntakuwa nimewakwaza ila nimeongea kwa nafasi yangu.