Kama kichwa cha habari kinavyojieleza
Nawaalika mabikra wote tuliopo MMU tukutane hapa tupeane uzoefu, lengo kubadirishana mbinu zilizotusaidia kuutunza usichana wetu mpaka Leo hii.
Binafsi nilifanikiwa kuutunza usichana wangu kwa kuzingatia maagizo ya wazazi wangu, pamoja na hilo pia nili nia kuto kumkubalia mwanaume yoyote atakaye nitaka kimapenzi.
Changamoto nilizokutana nazo kwa uamuzi huo ni nyingi sana , wasichana wenzangu walinicheka na kuniambia nakosa raha duniani.
wavulana walifka mahali wakawa wana niogopa sana kutokana na majibu yangu.
Nilitengwa ktk mambo kadhaa na walio kuwa rafiki zangu.
Nilionekana kama mwanamke asiye na hisia ...na mengine mengi tu lkn hayakuni yumbisha.
Nafurahia maamuzi yangu sijawahi kuyajutia kamwe.
Na nitaendelea na msimamo wangu mpaka nitakapo funga ndoa...
Karibuni