Hongera binti, kazana usikate tamaa. Nakutia moyo uendelee na msimamo wako maana nahisi wako waliotema mate pembeni kwa kusoma huu uzi wako tuu na wapo waliosonya na wapo pia waliokung'ong;a japo hawakuoni usishangae wakapatikana pia waliokutizama kwa jicho la husda kwa kukupandisha na kukushusha bila hata kukuona kwa macho ya nyama.
Kama udhui na lengo la uzi wako basi wataojitokeza muendelee kutiana moyo na kusimamia msimamo wenu hadi siko mtakapofunga pingu za maisha. Baada ya kusema hayo naomba nitoe ushuhuda wangu kuhusu bikira....
Kasie wakati nasoma mama yangu aliniasa kuwa shati la shule nnalolivaa (jeupe) lina maana ya usafi hivo nihakikishe usafi huo nakua nao hadi namaliza shule na wakati huo nilikuwa nasoma shule ya msingi. Wakati huo huo wakati napokea kipaimara nikiwa sekondari mama alinikumbusha huu usemi kuwa nguo nyeupe maana yake ni usafi hivyo nikivaa gaunu jeupe nihakikishe na mie ni msafi. Namshukuru Mungu nilimaliza kidato cha sita nikiwa bikira na kipindi chote hicho nilipata misuko suko ya kila namna na aina kutoka kwa wavulana, vijana na wababa. Ila baada tuu ya kumaliza kidato cha sita laah nakumbuka ilikuwa mwezi wa Tano/Sita sikufika mwezi wa 12 tayari walishaniondoa kwenye kundi la mabikira. Hivo lengo langu na adhma ya kuolewa nikiwa bikira ilifutika na hii ni moja ya sababu zilizonifanya niachane na kufikiria masuala ya ndoa hadi leo hii.
Kila la kheri msichana kigori.
Kasie.