Wanawake Arusha wanasikitisha, vipi mikoa Mingine?

Wanawake Arusha wanasikitisha, vipi mikoa Mingine?

Kakende

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2012
Posts
2,741
Reaction score
1,233
Wadau ukifika Arusha mjini utaona hali ya kusikitisha, wanawake na baadhi ya vijana wamejaa mji mzima, kila kona ya mitaa wanauza Nyanya na mbogamboga mbalimbali katika maeneo ambayo uwezi kudhania kuwa mtu anaweza kuuza mboga za majani.

Kibaya zaidi ukifika pale friends corner(opposite to CRDB bank) utakuta baadhi yao wanauza nyama mbichi ya kuku, yaani kuku anakatwa vipande. Nyama hizo ni fresh kabisa, hazifunikwi, nzi wanarukia, vumbi, watu wanapita nk, bibi afya wamelala.

Kuuza nyanya ni sehemu ya maisha, ni kujishughulisha, lakini inatakiwa iwe katika sehemu iliyo rasmi, lakini hapa utaona wametandika vigunia chini kila eneo. Kuijishghulisha ni muhimu sana, mimi ningeona wako kwenye mashamba ya uzalishaji wa mbogamboga, wanazalisha na kufungasha kupeleka hata kwenye soko la nje hapo sawa, lakini kinachofanyika hapa ni indicator ya umasikini

Anyway, ukifikiria utagundua kuwa watu hawa wamekata tamaa, wanatafuta angalau cha kuingia kinywani, wanatafutia watoto wao. Hakuna viwanda, hawana elimu watafanyaje!. Maisha ya Mtanzania yamekuwa magumu, Mtanzania sasa anaona umaskini ni sehemu ya maisha yake ndiyo maana ukija uchaguzi anapigia chama kilekile kilichojigawia nyumba za umma, kuua viwanda, sasa ni zamu ya meno ya Tembo.



Vipi mikoa mingine, hali ikoje?

Concept yangu iko hivi. Nchi yoyote ambayo umaskini umekithiri utaona mji mzima vijana ni machinga, watu wanauza utumbo wa kuku, wengine wanauza karanga, kila kijana ni dereva pikipiki ili mradi apate jinsi ya kuishi siku hiyo. Lakini kama kungekuwa na mpango mzuri, tungeona wanawake na vijana wamewezeshwa, mfano wangekuwa wanashona nguo kwa wingi na ku export nje. Kwa taarifa yenu hizi nguo tunazoagiza kutoka nje zote zinatengenezwa kwa mikono ya watu waliopewa mafunzo ya hali ya juu. Ninachomanisha ni hiki hapa chini

Hawa wanashona nguo kwa mikono na ku export
clothing 2.jpg

clothing 3.jpg

Tazama wa huku kwetu Arusha city center, hapa si sokoni kabisa, ni nje ya maduka

mboga2.jpg
 
Ni Arusha mjin au village

Arusha mjini, yaani utakuta nje kwenye duka lenye kiwango cha kimataifa, nje ya Bank wao wako nje. Kuanzia posta hadi stand, kwenye njia kuu zenye round about kote wamefurika. Inasikitisha
 
Ni tz nzima hali ni mbaya....wakati huo kila mtu anadaiwa na wazungu laki sita...zilizonunulia mashangingi na kutibu
wakubwa... check up wao us...india uk..nyumba ndogo nk

sisi hata panadol ni tatizo
 
Wadau ukifika Arusha kuna hali ya kusikitisha, wanawake na baadhi ya vijana wamejaa mji mzima, kila kona ya mitaa wanauza Nyanya na mbogamboga mbalimbali katika maeneo ambayo uwezi kudhania kuwa mtu anaweza kuuza mboga za majani.

Kibaya zaidi ukifika pale friends corner(opposite to CRDB bank) utakuta baadhi yao wanauza nyama mbichi ya kuku, yaani kuku anakatwa vipande. Nyama hizo ni fresh kabisa, hazifunikwi, nzi wanarukia, vumbi, watu wanapita nk, bibi afya wamelala. Anyway, ukifikiria utagundua kuwa watu hawa wamekata tamaa, wanatafuta angalau cha kuingia kinywani, wanatafutia watoto wao. Hakuna viwanda, hawana elimu watafanyaje!. Maisha ya Mtanzania yamekuwa magumu, Mtanzania sasa anaona umaskini ni sehemu ya maisha yake ndiyo maana ukija uchaguzi anapigia chama kilekile kilichojigawia nyumba za umma, kuua viwanda, sasa ni zamu ya meno ya Tembo

Vipi mikoa mingine, hali ikoje?

Pole sana mkuu, naweza kuhisi unavyo umia rohoni juu ya Watanganyika hao. Nakubali maneno yako, kua hao wamekata tamaa. Najua serekali badala ya kuwajengea fursa, hapo wataahidiwa tena ten more years ya Maisha bora.
 
Si walisemaga kwamba wamechaguaga Mbunge na Madiwani ambao ni MAJEMBE...!!!!
 
Arusha mjini, yaani utakuta nje kwenye duka lenye kiwango cha kimataifa, nje ya Bank wao wako nje. Kuanzia posta hadi stand, kwenye njia kuu zenye round about kote wamefurika. Inasikitisha
Nafikiri hii ni shida kubwa kuliko wauza mchicha.
Kuuza mchicha sio kihashiria cha shida, ni kiashiria cha aina ya watu watafutaji.

9k=
 
wakinamama wa arusha wamekata tamaa kabisa, wamemchagua lema wakifikiri hali zao duni zitapungua kumbe ndio zinaongezeka, lema na wahuni wenzake wanaandaa maandamano kila siku ili wawapore wanawake wafanyabiashara ndogo ndogo bidhaa zao. hasira zao tutaziona kwenye uchaguzi mwakani watahakikisha wanainyima kura chadema uliyowasababishia umasikini wa kutisha
 
Kina mama wa Arusha wako juu. njoo huku kwenye migodi uone dada zetu wanavyonyanyasika. au pale ohio wanavyodhalilishwa na wageni wa ccm hasa wahindi. utatamani ubakie Arusha milele
 
Kina mama wa Arusha wako juu. njoo huku kwenye migodi uone dada zetu wanavyonyanyasika. au pale ohio wanavyodhalilishwa na wageni wa ccm hasa wahindi. utatamani ubakie Arusha milele

mkuu, pitia pale maeneo ya mrina na shiverz uone wanawake wanavyodhalilishwa na machalii wa chadema, utatamani usikanyage tena arusha
 
Hali ni mbaya si Arusha tu bali nchini kote.Tunahangaika na katiba kwa sehemu kubwa kwa ajili ya madaraka lakini kama taifa hatuna kipaumbele wala uelekeo.Tunajiendea endea tu kwa wananchi walio wengi.
 
Ingefaa baada ya suala la katiba tukae kama taifa na kujiwekea vipaumbele na adhabu kwa watakaokiuka. Mfano hawa watu waliotajwa wanafanya uchuuzi tu. Kuwepo na uzalishaji na masoko, kuwe na viwanda vya umma na uteuzi usiwe wa raisi ili atakayeshindwa atolewe mara moja.Tutake tusitake kama tunataka maendeleo ya watu turudi kwenye sera za ujamaa ulioboreshwa.
 
Tatizo si wanawake,vijana wala wananchi!

tatizo ni huyu shehe tuliyempa nchi!

Amesoma economics lakini anaendesha mambo kama vile amesoma taarabu!

Mipasho mipasho tu!
 
Back
Top Bottom