Ukiacha mazingira, wanawake Arusha ni wahangaikaji/watafutaji sana. Kupitia biashara zao halali za kuuza nyanya na mchicha wanalea familia, wanalipa kodi na kusomesha watoto.
NI KWELI KABISA, WAMAMA HAWA WA ARUSHA MJINI WANAJITAHIDI JAMANI. WANASOMESHA WATOTO, WANALISHA FAMILIA, WANALIPA KODI ZA NYUMBA, WANAJENGA NYUMBA ZAO ZA KUISHI, WANATUNZA WABABA( BAADHI YA WABABA HAWAFANYI KAZI YOYOTE YA KUINGIZA KIPATO. KAZI YAO KUBWA KUSHINDA VIJIWENI WAKITEGEMEA JASHO LA WAMAMA HAWA). WAMAMA HAWA HAWALALI JAMANI. NAWAPA POLE SANA, NAWAOMBEA KWA MUNGU JASHO LAO LISIMWAGIKE BURE. Hakika wachacharikaji sana. Saa kumi na moja asubuhi utawaona barabarani, kwenye toyo na kwenye vifodi na mafurushi makubwa ya mboga za majani wanawahi soko kuu, Kilombero na Samunge(soko lililipo uwanja wa NMC) kuuza mboga kwa bei ya jumla. Wengine wana watoto mgongoni. Ukirudi mabustanini kuna wanaolima hizo mboga wanahangaika kunyweshea maji usiku na mchana na kupeleka mboga kuuza au kuwauzia wenzao wanaokwenda kuuza jumla au rejareja. Kukipambazuka ndo utawakuta wanavyochacharika na uuzaji wa mboga, nyanya, vitunguu, n,k katika maeneo hayo yasiyo rasmi. Utawaona na vigunia vyao wametandika chini, watoto migongoni wanahangaika kubembeleza wapita njia wanunue. Ghafla utaona wananyanyua mifuko na vigunia vyao na kukimbia. Kisa? Mgambo katokea anawafukuza wasiuzie bidhaa katika maeneo hayo!!!!!
Shida hii ya kufanya biashara maeneo yasiyo rasmi inatakiwa iangaliwe kwa mapana zaidi.
Sababu kubwa ni kuwa watu ni wengi wakati mji ni mdogo. Watu wamejazana sana pale eneo la kuzunguka soko kuu, NMB na CRDB bank hadi uhuru Road wakiuza vitu kwa sababu pia kuna wanunuzi wengi tu. Uwingi wa watu/walaji na mji mdogo ndilo tatizo. Kinachopaswa kufanywa ni kupanua mji na kuhamishia soko kuu na stand ya mabus makubwa nje ya mji kwenye maeneo kama vile Murieti, Moshono, Usa river, Kisongo, Korona, Lengijave, n.k. Kwa kufanya hivyo basi kutakuwa na mtawanyiko wa watafutaji na si kulundikana sehemu moja kiasi hata magari yanakosa pa kupita. Huu ni mtazamo wangu. Naomba kuwasilisha.