Kuna wale Team Mawigi sugu hata ukiwaletea habari za google wataona kama unawazingua, labda mpaka wao wenyewe wakutane nazo wenye maombi
Mi simoacha tu wengine utakuta wanakipilipili au mapunye
Mwanamke anapendeza na kuvutia zaidi anapokuwa na nywele zake za asili wala sio mawigi. Hiyo ni FACT.
Mawigi yanaboa na yanatupunguzia hisia, mfano pale mwanaume unavyozishika au kujaribu kuzichezea halafu unajua kabisa hizi nywele sio.
Ni kama likofia fulani hivi linalovaliwa au kushonwa kichwani kwa mwanamke, ambayo pamoja na kwamba KIUHALISIA halimuongezei mwanamke mvuto (hata kama ni la Laki Moja), linatakiwa libadilishwe kila baada ya muda fulani.
Wanawake bakini na nywele zenu za asili, zipeni matunzo na usafi wala hamna haja ya kuhangaika na kubadilisha mawigi maana wanaume {99.99%} hatuzipendi. Zinaboa hata kuangalia.
Cha kushangaza, utamkuta mwanamke wa kibongo eti naye anahangaika kuweka liwigi lake vizuri kanakwamba linamzuia kuona vizuri wakati ni FAKE HAIR na yeye mwenyewe kaliweka hivyo kwa makusudi kuiga Wazungu.
Say NO to Fake Hair.
na kweliNdio ujue kuna nguvu ya ziada ktk Mawigi.
Teh teh..Yani sometimes unakuta msichana anageuka kuangalia upande mwingine ila wig limebaki straight tu..halijafwata direction ya kichwa...
kama mimiUsiseme wote, wengi tu wanaojitambua hawazivai
Wewe Sonko, Jr umeleta mjadala mzuri sana. Kwa kweli wazungu ni 'washenzi' kweli kweli. Yaani wanatuletea mawigi eti tufanane na wao. Nashukuru mke wangu havai mawigi ila mabinti zangu weeee ni shida. Sijui sisi waafrika tukoje. Nikiwaambia mabinti zangu ambao nawamudu majibu yao hunikatisha tama. Yaani utasikia wanasema wewe baba sisi tunakuheshimu na tunakupenda na umetusomesha ila tunakuomba utuache na haya mawigi kwani ndiyo mambo ya kileo...huwa nabaki nashangaa. Angalau nashukuru jambo moja. Mabinti zangu hawajagusa mikorogo. Yaani jamani mikorogo ni shida kuliko mawigi. Mimi niliwaambia mabinti zangu kuwa wakianza mikorogo nachukua panga na kuwashughulikia sitaki ujinga huo.....
Mi sipendi ila ndo hivyo nimekubali yaishe, maana mna sababu lukukiiiiiiiii
Mara nachoka kusuka, mara nakosa muda wa kwenda saluni, mara nachoka kuandaa nywele asubuhi, mara sijui nini daaah, basi bwana ntafanyaje sasa!!! make unalazimishwa kupenda usichopenda
Wamekubali, after all mawig mnavaa mtuvutie, na sis hayatuvutii Tupa Kule, kuwa simpo tu,
Hahaha my kaka bana, but wifi akinyukaga weaves zake si huwa unamsifia hata kimoyo moyo au?
Hata mumwange povu kiasi gani maweaving na wigi zitavaliwa tu na wanawake as long as wana exist on planet. Kama hamjui hata wazungu hutumia weaving
Nani kakwambia wanawake huvaa au kujiremba kwa akili ya kuvutia wanaume. Hyo perceptions yako ni wrong
Siyo kimoyo moyo namsifiaga kiwazi wazi ila ndo hivyo kinafiki, coz mnalazimisha hayo madude wanaume wengi hatuyapendi, hope umeona mwenyewe walivyotiririka humu
Mnayapenda nyie kwa nyie tu kwa kweli
Mmh basi sawa
Ila wengine tulishajiandaa kisaikolojia, so vaeni tu