Nami nasema hivi, hata msiyapende, kuna baadhi yetu hatufanyi kwa ajili yenu, kuna wanawake wengi sana wako local (natural) go and opt for them. Yanini kujipa pressure kwa vitu visivyokuhusu?
Inasemekana ndivyo ilivyo, ndo maana mwanamke mwenzie akimshauri usimkubalie fulani basi atapokea ushauri haraka zaidi. ..akisifiwa na mwanamke mwenzie anaamini, akisifiwa na mwanaume atahisi ni kwa sababu tu kuna kitu mwanaume anataka.
So vingi wanawake wanataka waonekane bora kwa wenzao wakiamini ndio ukweli wamekuwa bora
Hahaha babu hii ni "fair game". Na wewe hupendi weaves?
Kwenye hii sayari mnaishi na sisi, 99.99% hatuzipendi, wewe kama unazipenda jua ni ulimbukeni uliopitiliza??
Kwahiyo unavyoigaiga kuwa Mzungu kwa kuvaa Fake Hair ndo unakuwa international? Ndo unavyojidanganya
Tunataka kurudisha wanawake katika misingi ya urembo na mvuto, misingi ambayo mnaacha kwa kasi
Bwana weee! Mwanamke wa nani umrudishe kwenye hiyo unayoiita misingi ya urembo? Ikiwa sisi wenyewe hatuamini katika unaloamini wewe? Why can't you deal with your wife anyway! ?
Ikiwa sisi ni malimbukeni tunakuathiri vipi labda? Kuiga uzungu! Naomba tuanze kuchambua moja moja tuliloiga kwa wazungu halafu tuyaache, ikiwezekana basi na mimi ntaacha kujiremba na kuweka fake hairs!
Naomba tuwe wakweli kabisa ķwa joto la Dar na jinsi watu tulivyo busy na maisha, muda ni mdogo sana, sana sana mtu ataenda weekend kusafisha wigi lake hebu tujadili mijasho ya siku mfano 3 tuu huko kichwani kweli kaharufu kana kwepeka?
Team Mawigi inabidi muelewe kuwa wanaume 99.99% hatupendi na hatuvutiwi na Fake Hair.
Wanawake wakifanya kila wanaloweza kufanya na nywele zao za asili wanapendeza na kuvutia zaidi, Full Stop
Kama huamini hizo principles ndo kutokujitambua kwenyewe, upo??
Mkiwa malimbukeni mnatusababishia tuvute hewa chafu tukiwa kwenye meeting yoyote mliomo
Kama hukupewa nywele ndefu kama Wazungu au wahindi ya nini uhangaike kuweka za bandia ili ufanane nao? Kwanini usijikubali, ya nini ushindwe kujiamini?
Nilitaka tu kuthibitisha kuwa wanawake ndio tunaoelewa stuffs zetu mara nyingi sio wanaume. Na mwanamke akikusifia basi jua she is real.
Teh teh..Mnatutisha..Acheni banaHahahahaha umenifanya nicheke kwa sauti,
Utani wako wa ngumi ujue.
Absolutely right! Ikitokea mwanamke amekusifia basi ujue yamemfika hapaaaa, ameshindwa kuvumilia. Men wanasifia ili kutengeneza njia ya kile wanachotaka kuomba.
Ngoja nikupe mfano, chuo nilisoma mkoani miaka hiyoooo mi pia wamkoani lakini nina exposure yakutosha maana nimezurura sana, kwahiyo nilikuwa mjanja wao yaani nawakimbiza ile mbaya, ikatokea kila nikiwa naenda lecture njiani wadada watanisimamisha (nilikuwa natembea mwenyewe mwenyewe mara nyingi) basi wale wanaopenda vya kijanja wataniuliza hiki nimenunua wapi hiki wapi, nimesuka saluni gani na vitu kibao, as time goes nikatengeneza marafiki kwa mtindo huo, basi nikaona why nisianze biashara? wakati kila kitu changu inatokea kinapendwa na wadada wengi? Since there nikawa mjasiriamali, hadi leo hii nafanya biashara zangu na wanawake, chuomates wengi washaolewa wameshamove sehemu nyingine lakini akiona hata dp yako atasema na mi nataka hicho kitu, namtumia kiroho safi.
Kwanini nimeyasema hayo yote? Nilitaka tu kuthibitisha kuwa wanawake ndio tunaoelewa stuffs zetu mara nyingi sio wanaume. Na mwanamke akikusifia basi jua she is real.
Huo ni mtazamo wake siwezi mlazimisha kila mtu akawa na mtazamo kama wangu but mimi kukaa hata siku mbili na mijasho ya Dar siwezi hapa ntaambiwa mambo ya fashion ila kwa fashion hii nilikwisha kubali inipite.
Unajielezea au unafanyaje? mickuelewi naona uko nnje ya post kabisa tunachozungumzia ni mawigi cjui chuo ulichosoma ni chakutega samaki hueleweki
Wenzako wajanja huwa wanawauliza wanaume walio nao kwenye mahusiano, wawaambie kama wamependeza au wamebugi maana jibu watakalopata hapo ni la ukweli na linawaongezea confidence 1000%
Kama mwanaume hana nia ya kumuoa mtu hata utoe wigi hakuoi, usitudanganye hapa. Hao wanaume wengi mbona wanawaacha dada zao wavae/wasuke ni kwamba hawataki dada zao waolewe! ! Nadhani muanze kuwashauri mnao onana nao, huku mtandaoni hatujali.
Naona Engine yako inahitaji kupumzishwa, mi niko na V8, sijui utanikutia wapi