barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Kumekuwa na wimbi kubwa sana la wanaume kuhangaikia kuwa na six packs,yaani kwa sasa ukitembea kwenye saloon zenye kutengeneza kucha na yale maeneo ya gym wamejaa sana wanaume wenye miili mikubwa na wanavizia wamama wanaokwenda kutengeneza kucha na wale wanaokwenda kupunguza matumbo yao gym
Kwa sasa vijana wengi mjini wanajichubua sana mpaka inakuwa hakuna tofauti na dada zao.Vijana mpaka wanaiba makopo ya mikorogo ya dada zao.Unakuta mtu mnyakyusa wa Mbeya tena Tukuyu ndani ndani kwa kina Mwakalindile na kina Mwakajanga lkn mweupe usoni kama anatoka ukoo mmoja na Shy Rose Bhanji.Mpaka imefikia mwanaume anashindana kwa makopo ya mikorogo na dada zake
Jamani wakaka wa mjinj na hasa Dsm hebu achaneni na mambo ya mikorogo sijui mambo ya six packs,kuna namna nyingi za kuonekana mwanaume "wa haja" si lazima upendwe kwa mkorogo na six packs.Hizi ni salamu kwa wanaume wa Dsm maskani yao na warumi na dada yangu Nifah