Lanlady
JF-Expert Member
- Feb 27, 2019
- 1,913
- 6,524
Habari! Ni matumaini yangu mu wazima wa afya, kama kuna wagonjwa poleni sana; nawaombea mpate afya haraka kwa uwezo wa Mola!
Sasa, leo naomba tuzungumze kidogo kuhusu tabia za baadhi ya wanaume. Kama tujuavyo wengi, kwa mila na desturi za kiafrika; mwanaume ndiye huanza kutafuta au kutaka mahusiano na mwanamke. Mwanamke anaweza asiwe tayari kutokana na sababu mbalimbali lakini mwanaume anaweza kutumia mbinu za ushawishi ili awe na huyo mwanamke.
Baada ya muda mwanamke anaamua kukubalia kuwa na mahusiano na huyo mwanaume. Ni jambo la kawaida kwasababu za kimaumbile, si rahisi kuishi peke yako siku zote.
Cha ajabu ni kwamba baada ya muda kupita, mwanaume yule yule aliyetumia kila aina ya ushawishi kumpata mwanamke aliyemhitaji, anaanza kumdharau, kumtesa na pengine hata kumsimanga kwa yale aliyomfanyia. Mfano pesa, mtaji wa biashara nk. Huu ni ukatili.
Mwanaume unapoamua kumshawishi mtu kwa namna yoyote ile, inabidi ujiandae kwa matokeo utakayoyapata! Usianze kulalamikia pesa au mali ulizotumia kwa ajili yake. Huo ni ukatili wa kihisia!