Wanaume warefu tuko kwenye 'extinction' hatari ya kutoweka kabisa Duniani

Wanaume warefu tuko kwenye 'extinction' hatari ya kutoweka kabisa Duniani

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2014
Posts
4,050
Reaction score
12,968
Naposema wanaume warefu nazungumzia mtu mwenye urefu au kimo cha kuanzia futi 6 na kuendelea.

Historia inaonyesha miaka ya nyuma watu walikua wenye miili mikubwa na maumbo makubwa, sio wanawake wala wanaume. Miaka inazidi kwenda na kizazi cha watu wenye maumbile au miili mikubwa kinazidi kutoweka, kimekuja kizazi ambacho kiko contaminated and diluted, watu wana miili midogo na wafupi ajabu. Leo watu warefu ni wa kuhesabu. Ukiwa futi 5.8 unaitwa tall, unajiuliza tall?

Mimi naomba kusema, katika vitu vinavyotoweka Duniani kwa kasi, ukiachia wanyama kama tembo au twiga au kifaru, wanaume warefu au watu warefu kuto kwenye hatari ya kutoweka kabisa Duniani. Miaka 100 ijayo hizi mbegu hazitakuwepo kabisa. Dunia iyakua imejaa andunje kama kina Pierre Liquid, itakuja kua historia kua kulikua na watu wana kimo cha futi 6 au 7 huku majority wakiwa na futi 4 hadi 5.

Ni wakati muafaka sasa tuhalikishe tunahifadhi hizi mbegu kubwa maana hakuna namna mtu utakua mrefu, kua mrefu ni natural gift, sio hela kua utatafta na kuzipata.

Miaka flani kikiwa mdogo, kuna mzee mmoja kijijini kwetu alikua anamwambia bro wangu ambae sasa ni marehemu (6.7ft) kua akiwashika ugoni bro wangu na mke wake, atawasamehe maana anajua hata kama mtoto atakaezaliwa hatakua wake angalau atakua na umbile kama lake, hivyo hata watu hawatahoji sana maana watasema ana mwili wa baba yake ila akimkuta mwanaume mfupi na mkewe atawaua wote maana watacontaminate mbegu yake. Hata mimi sasa naungana na yule mzee, ili kuhifadhi mbegu yangu, nikimkuta mke wangu na mchepuko mfupi namuacha, akiwa mrefu naweza kumfikiria kumsamehe.

Kwa niaba ya watu warefu wote, naomba serikali ianzishe jitihada za maksudi kuhifadhi hizi mbegu zetu, tutapotea itakuja kua hadithi huko mbele. Iaka 100 ijayo Dunia itakua ya ajabu sana, itakua na watu majority nika Pierre, mtu analingana na vits urefu.

Naomba ieleweke wazi kua haya ni maoni yangu binafsi na sina nia ya kukashfu umbile au kimo cha mtu.
20190202_182202.jpg
 
urefu wa juu au chini maana sikuizi urefu wote ni shida haupatiani yaani wa juu na chini
 
Duh hilo guu ni shida

Repent *4 cause we're two steps away from a real disaster, think there is a boss but a who are the master?life set a pace, everything's much faster need to slow down and pray, forgive them
 
Duh hilo guu ni shida

Repent *4 cause we're two steps away from a real disaster, think there is a boss but a who are the master?life set a pace, everything's much faster need to slow down and pray, forgive them
Ka goliathii😂
 
Back
Top Bottom