Wanaume wanaotelekeza watoto ni janga kubwa nchini kwa sasa

thanks again and have you

JF-Expert Member
May 11, 2023
230
423
Habari!? Kumekuwepo na ongezeko la wadada wengi ambao hawako kwenye ndoa ila tayari wana watoto, wengine wanaishi nao na wengine wamewapeleka vijijini kwa wazazi, unakuta anayehusika kwa malezi ya mtoto ni Dada peke yake (single mom) unakuta mdada hana kipato Cha maana Matokeo yake anaamua kujikita kwenye biashara mbalimbali haramu Kama ukahaba ili aweze kukidhi mahitaji ya mtoto.

"Wanaume wenzangu hii tabia sio nzuri tumewafanya wanawake waishi mazingira Magumu na unajua mtu Mpaka anaamua kukuzalia amekuheshimu na kukupenda Sana kwa hyo suala la kumtelekeza si Jambo jema hata Kama alikukosea lakini mtoto anakua hana hatia unatakiwa umpe huduma zote. Ukikutana na wanawake waliotelekezwa hawatamaniki, kucha kwa waganga, kwenye maombi nk lengo kutafuta unafuu wa Maisha then anatokea mwanaume anasema "Tusioe single mother" wakati sisi ndio Main cause!

Na badae tuseme wadogo zetu hawaolewi na bra bra! Malipo duniani ndugu zangu! Naumiaga sana nikiona Mama anahangaika na mtoto kwenye hali ya uduni wakati muhusika wa mtoto yupo. Tubadilike.
 
Awali, nilikuwa na huruma kama wewe lakini baada ya kuufahamu uhalisia wa asilimia kubwa ya hawa dada zetu(single moms) nimejikuta nafurahia kutangatanga kwao
Wanaangaika Sana Mpaka najisikia vibaya wamekua wadangaji ,wanauzaa miili sababu unakuta ana watoto wawili Sasa imagine kwa Maisha ya Dar es salaam umetelekezewa watoto wawili? Unalipa Kodi, wale na uhakikishe wanapata mahitaji ya shule na nyumbani wanakutegemea utaweza!!? Si utaingia majaribuni tu
 
Best option ni kumnyang'anya. Maana ukisema utume hela ya matumizi utajikuta zaidi ya 50% unamtunza mwanamke na Siyo watoto
Hii ndio mimi niliifanya kwa watoto wangu wote 5 wa mama tofauti. Niligoma kutoa matumizi, lakini nilikubali kuwalea na mwisho wa siku wanangu wote 5 niliwachukua na kuwalea mwenyewe, kabla sijaoa na tukapata watoto wengine 3😊😊
 
Mwanaume kazi yako hudumia mwanamke malezi Sana Sana ! Wewe toa huduma za mtoto
Hii kitu hua napingana nayo siku zote (usimpe mwanamke pesa akutunzie mwanao). Maana mwanao akilelewa na mtu mwingine, siku akikua mkubwa atakuja kwako akiwa mtu mwingine, mwenye fikra tofauti na zakwako pia atakuja na tabia za watu wengine kabisa tofauti na ulivyo tamani wewe awe.

Unapo toa pesa kwa mama wa mtoto amtunze, unauhakika gani kama zinatumika kama ulivyo taka?? Na jeunapo toa pesa kwa mama wa mtoto wako amtunze mwanau, unauhakika na maneno anayo ambiwa ni mema juu yako kama baba anae wajibika??
 
Back
Top Bottom