Wanaume wanaonyaswa na wake zao. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaume wanaonyaswa na wake zao.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mfamaji, Jul 2, 2009.

 1. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Nilisikia kwenye vyombo vya habari hivi majuzi kuwa kuna mwanaume huko Kenya aliamua kuvunja ukimya kwa kumshtaki mkewe baada ya mkewe huyo kumpiga mzee na kumpa majeraha.

  Wanaume wengi wamekuwa wakivumilia manayanyaso ya aina mbalimbali toka kwa wake zao. Wako wanawake wanaoanzisha matatizo kwa waume zao wakiwa na malengo ya kuachana halafu baadae adai mali kama sheria ya ndoa invyodai, na kwa haraka haraka naona kama hili linachukua sura ya kisasa zaidi likiambatana na idiology ya usawa pamoja na kuigana . Utakuta baaadhi ya waliokwishaachika wana maisha fulani ya kirahisi , kama wanavyodhani wengine- kwamba fulani angalia baada ya kuachika maisha yake fresh,ana gari,biashara etc.

  Wako wazee wanaopigwa , wanaonyimwa chakula , ndoa , kufungiwa nje n.k
  Hakuna mahali pa kuongelea haya maana wanaume aibu kuzungumza hivi. Mimi naona JF itumike pia kuwakomboa wenzetu wanaonyanyasika kindani ndani bila mahali pa kupata msaada. Wenye shida zao waweke hapa tuwachangie mawazo. Au mnasemaje wakuu? We dare talk openly.
   
 2. M

  Malila JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,413
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Hata hapa jf hawatajitokeza,angalia hiyo highlit point ktk maelezo yako. Cha kufanya toa majibu/suluhisho la tatizo hilo moja kwa moja ili mwenye kuguswa nalo aweze kupata majibu moja kwa moja.
   
 3. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Nafahamu kuwa hili ndilo tatizo. Kuzungumzia tatizo ni njia ya kulitatua. Kuna njia nyingi tu za kujitokeza .After all hatujuaini mkuu.
   
  Last edited: Jul 3, 2009
 4. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  makubwa haya. Eti niseme hadharani mke wangu jana kanipiga sana. Aibu aibu aibu.

  Lakini kuna umuhimu wa watu kuwa wawazi sana.
   
 5. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ndio maana utapigwa kila siku mpaka mwisho dunia afadhali useme JF ikusaidie mbinu?
   
 6. B

  Bibi Kizee JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2009
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 213
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kweli mmenichekesha, its good one step forward mkianzia hapa JF - NGO-etc;

  inabidi mfikirie pakwenda kudai haki zenu wenzenu tulianzia Beijing, ila watani kenya nadhani wanayo NGO ya kutetea wanaume wanaonyanyaswa 'MAENDELEO YA WANAUME' ,
   
 7. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #7
  Jul 5, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Ni afadhali upigwe utaumia then kwisha. Wanawake psychology yao ya utendaji mambo katika relationship hususan ndoa inaumiza sana na majeraha yasopona ukichunguza kwa makini. Hapa inasaidia akili. Pale mwanaume unapogundua kuwa mke wako anataka tu kukufanyia kitu mbaya itakayokufadhaisha, akili unageuza mashambulizi, yaani vita ya akili na ya kimya kimya. Ukizubaa utapiga hadi utakuja ua. Ishi kwa akili. Mfano: Mme atanunua say mosquito net kwa ajili ya mtoto. Na ni baada ya request kutoka kwa mkewe. Then mke hataitumia kisa alitaka ushindwe kuinunua ili akulaumu. Mtoto atapata malaria then mme atakataa kutoa tena pesa ya kutibu kabla ya kuhoji why net haitumiki. See it may end up somewhere very unattractive in a relationship. Hii ndio utendaji kazi wa kikeni na jinsi wanaume wanavyonyanyaswa kimya kimya. Afadhali akupige kiishe kuliko jeraha la akili na moyo. Halifutiki na hufadhaisha.
   
 8. Wayne

  Wayne JF-Expert Member

  #8
  Jul 6, 2009
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 663
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mimi nafikiri hii mada ni ya msingi kuijadili kwa kina.
  Unyanyaswaji upo sana na hasa pale inapotokea kuwa Mume ameyumba au kipato chake ni kidogo kuweza kukidhi mahitaji ya familia.

  Kuna swali najiuliza kwa nini WAJANE NI WENGI KULIKO WAGANE?
   
 9. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #9
  Jul 6, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Wayne nakushukuru maana unaanza kuona maana halisi ya hii thread. Kama alivyoeleza Mshiiri hapo juu kuna mambo ambayo yanasumbua wanaume psychologically na kukosa raha. Yawezekana high blood pressure, heart attacks na immotional suffererings vinachangia asilimia kubwa kwa vifo vya wanaume kutokana na manyanyaso ya akina waife wao. Na tufanye utafiti tuone nani anaishi zaidi kati ya wanume wasiooa na wale waliooa. assuming everthing is equal .

  Movement against mfume dume unaendelea kuwasupress wanaume kama vile wao ndio waliopanga iwe hivyo. Mwanadamu wa kwanza alikuwa dume , na ndiye alipewa mamlaka ya kuongoza dunia akiwemo jike . Sasa wanaume tufanyeje? Tubadilishe mfumo huu halafu ubaki upi ? What is the alternative ya mfumo dume ambao ndio theme ya sasa duniani kote kutaka kuuondoa? In the process wanume wanaisha ?.

  Enyi wanawake , eleweni vita haichi kuwa na madhara, na madhara ndio sisi madume wenu .Halafu tukiisha mtabaki wenyewe?

  Ni muhimu wanaume tuanze harakati za kujitetea haraka iwezekanavyo la ivyo mambo yetu ni mbaya kabisa.
   
  Last edited: Jul 6, 2009
Loading...