Wanaume Wameshindwa, Wanawake Tumeweza ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaume Wameshindwa, Wanawake Tumeweza !

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Muke Ya Muzungu, Feb 9, 2012.

 1. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Wanaume wameshindwa, Wakina mama Wameonyesha njia. Picha inajieleza !
  [​IMG]
   
 2. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Ukisoma historia ya nchi hii vizuri, ni wanawake ndio walikuwa nguzo kubwa wakati wa kupigania uhuru wa Tanzania. Yani FFU wangethubutu kuwamwagia maji ya kuwasha na kuwapiga mama zetu hao virungu, cha moto wangekiona. Wengi tungeenda kufia pale pale, kuokoa mama zetu.
   
 3. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  kweli kabisa, leo nilipoona kwnye tv hii picha ilinuma sana. nipo tayari na mimi kuongoza maandamano
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Wanawake wa Kenya waliiokoa bustani ya Uhuru isiuzwe kwa mafisadi baada ya kukusanyika hapo bustanini. Polisi walipoenda na virungu vyao ili kuwapiga, akina mama wakavua nguo wakabaki kama walivyozaliwa; polisi wakakimbia na Uhuru Park ikabaki hadi leo.
   
 5. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa mipolisi yetu ya bongo mmh! Naona ndio itawakodolea macho na kuwashika makalio, Sijui hawazionagi kwa wake zao?
   
 6. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  wanawake tunaweza kasoro Anne makinda
   
 7. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Shikamooni wanawake wote wenye moyo wa ushujaa kama hawa...
   
 8. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,094
  Likes Received: 10,451
  Trophy Points: 280
  shikamoo wakina mama kama hawa.
   
 9. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Shkamoo kwao, wamekamatwa na wasomi wa JF wakanyamaza bila kuwatetea
   
 10. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #10
  Feb 10, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wengi humu tumekuwa tukijigamba, eti tunahitaji mtu wa kutuanzishia tu ili tufanye "demonstration". Akina mama wakaonesha moyo wa ujasiri....na hapo ndipo wana-jf walipoonesha ujasiri wao wa kuandamana kwa kutumia keyboard.

  Ama kweli sisi ni mabingwa wa kuandamana kupitia barabara za keyboard, monitor, mouse, na keypads na hatimaye kuingia jf kwa ajili ya kumng'oa rahisi.

  Tuna Safari Ndefu....
   
 11. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #11
  Feb 10, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Kijo bisimba na nkya tu,except bi kiroboto
   
 12. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #12
  Feb 10, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,887
  Likes Received: 6,072
  Trophy Points: 280
  kuna watu wanaoamini kuwa 'watanzania ni waoga' ila wakisema hivi wana-exclude watawala na majeshi yao. Endapo itathibitisha kweli tu waoga basi mimi naamini hata hao pia ni waoga kama Watanzania wengineo na ndio maana wanaogopana wenyewe kwa wenyewe.

  Tumezoea kuwaona na kuwasikia kwenye tv na redio akina Ananieli Nkya, Bi Kijo Bisimba nk, lakini juzi kwa kuwa FRONT wameonyesha kweli kuwa mabadiliko (hasa kwa wale wasio yaamini) ndio yamefika tayari na naamini utokeaji wao pale Slender Bridge umechangia kwa kiasi kikubwa maamuzi ambayo serikali imetoa.

  Fikiria endapo PM asingetokea na wakaamua kama walivyokuwa tayari wamejiandaa kurudi pale hiyo jana (Alhamisi) ina maana tungelienda wengi zaidi kuwaunga mkono na kama ingelifikia Jumamosi, wimbo wa 'Tahirih Square' labda ungehamia Dar es Salaam.

  Lakini Watanzania tusijisahau, wametuonyesha njia na matokeo yake waliosimamishwa kazi (sio kufukuzwa) ni wawili tu. Bado Mh. Mponda na Naibu wake. Kwa hiyo ni budi kujipangia muda ili ikifika hapo kabla na hao hawajaachia hizo ofisi za umma tuangalie pa kuanzia. Hii ina maana wameondoka 'nyoka' wawili tu (tena wadogo) na bado wamo wengi hivyo anayeamini nguvu ya umma (na hasa hawa WAMAMA) imesaidia haya ni bora kuiunganisha. Huu uwe mwanzo, tukilala hali itarudia ileile.

  Hongera Akina Mama
   
 13. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #13
  Feb 10, 2012
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,642
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Hongereni akina Mama kwa Ujasiri ulioufanya.:poa
  Kwa mtazamo wangu,
  Huu ni mkakati uliopangwa huko huko ndani ya serikali kuvunja ukimya baada ya kuona mkuu wa nchi amekaa kimya na hatoi tamko.
  Ndo ikaamuliwa wanawake ndo watakuwa mistari wa mbele na ulinzi mkali utakuwepo kuwalinda ili wafikishe ujumbe kwa mkuu wa kaya( Huoni PT iko pembeni ina wahakikishia usalama? hata wao polisi walichoshwa na ukimya wa mkulu.

  KWANINI SERIKALI ISUBIRI MAANDAMO NDIO WAWAJIBIKE NA KUWAJIBISHWA KWA WAHUSIKA? :smash:
  JE WASINGEANDANAMA HII HALI INGEDUMA MPAKA LINI?:photo:
  AU WALIKUWA WANAONEANA AIBU KUWAJIBISHANA
  MPAKA PINDA ALIPOAMUA KUVAA BOMU
   
 14. Desteo

  Desteo JF-Expert Member

  #14
  Feb 10, 2012
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 446
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  tatizo hawachelewi kusema, mkitupiga mnatuonea, mkituacha mnatuogopa'. Ukweli mwingine ni kuwa ffu wanaangalia waanze vipi kupambana na hao wanawake? Kila cha kinguvu utakachomfanya unamdhalilisha. Hivyo kusema wanawake wameweza ni kupotosha
   
 15. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #15
  Feb 10, 2012
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Doctor hawa inabidi muwe mnawapatia matibabu extra

   
 16. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #16
  Feb 10, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  hawa wakina mama ni mashujaa....yes we can do it.hapo nakubali kuwa wakina mama wametuzidi kete.
   
Loading...