Lizarazu
JF-Expert Member
- Aug 23, 2015
- 6,331
- 7,885
Wanavyosema wao eti ile ni ishara ya appreciation for being accepted kumuoa binti, lakini ile ina maana nzito sana na haishii pale tu, kwa taratibu za kimila za jamii zingine kupiga goti inatoa tafsiri ya kwamba kwenye jambo zito/kubwa uko tayari kupisha na kukaa kando huku yule uliyempigia goti ukimuona ndio anastahili kuongoza kimaamuzi.Yaani mkuu ni aibu mno. Zamani mwanamke ndiye aliyekuwa analia machozi kwa kutoamini kama kweli kavishwa pete!! Mpaka wakati wa ndoa ilikuwa ni kilio kwa binti, sasa siku hizi sijui wanaume ndio wanakuwa hawaamini kama wamekubaliwa kuoa hawa mabinti!!?
Maana yake hapa ni kuwa kijana ndiyo anakuwa amebahatika ku,woa binti, ila huyu mke wala hana pressure na jamas. Hivyo kudumu kwa ndoa za aina hii kwa kiasi kikubwa kunategemea utii wa mwanamume kwa mkewe. Mke ni kama hana cha kupoteza isipokuwa mume, na hivyo mwenye ndoa hapa ni mke. Huu ni upuuzi wa hali ya juu na mwanamume wa aina hii keshaikana asili yake.
Nachoshukuru kuna jamii huu upuuzi wa kupiga goti kwa mwanamke haupo kabisa ikiwemo ya kwangu mimi.
