Wanaume walioharibika akili

Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
14,770
10,650
Leo tuangalie upande wa pili kidogo. Tujadili kwa kujenga ili tuone wapi tumekosea ili tujirekebishe, lengo likiwa ni kufunguana mawazo. Mada hii inaweza kuwa msaada mkubwa kwa vijana ambao hawajawa na wake bado kama wataifuata kwa kujenga na si ushindani. Twende kazi:

Mwanamume aliumbwa kwa ukamilifu wake toka mavumbini. Hakuwa na upungufu wowote na hata Mungu mwenyewe aliona kila alichokiumba na tazama "ni chema." Mwanamke alitoholewa kutoka ubavuni mwa mwanamume, baada ya Mungu kuona jamaa amekosa kampani ya sampuli yake, kwani alikuwa kati ya wanyama na wadudu na ndege etc. Hivyo mwanamke ni companion wa mwanamume na hawezi kamwe kuwa mbadala. Ndio maana hata tamaduni za kale zilitaka mwanamke arithiwe pale mume anapofariki, lakini mke akifariki mume harithiwi.

Ukitazama kizazi cha kisasa kimeondoa kabisa mipaka kati ya mwanamume na mwanamke. Vijana wengi sasa wanajisikia wako level moja na wanawake, kifikra, kiutendaji, kifamilia n.k. Sio kosa lao, ni ukosefu wa msingi wa maadili kutoka kwa wazazi na jamii kwa ujumla wake. Zamani jamii ilihusika kuwalea watoto, kiasi kwamba hata kama uko mtaani kucheza na rafiki zako, akapita mtu mzima akawakuta mnafanya michezo isiyo na maadili, alikuwa na uhuru wa kuwatandika bakora na kisha kwenda nyumbani kutoa taarifa. Lakini leo watoto wanajilea automatic, wazazi wako bize, mtaani hakuna maonyo, ni shida tu.

Kufuatia hayo vijana wengi wamejiona wamezibuka kwa kuiga mambo ya kijinga kabisa toka vyanzo mbalimbali kama TV, filamu za ulaya, magazeti ya udaku, mitandao ya kijamii, mafundisho mashuleni n.k. Vijana wanafunzi wa shule badala ya kujadili bunsen burner au parking orbit, wanabishana nani ana shepu kali kati ya wolper na Wema Sepetu!! Wanabishana kati ya mavazi ya kampuni za mashoga za Lee na Calvin Klain nani mkali!!

Hawa vijana hawana fikra za kujenga familia siku zijazo, wengi wameingia kwenye ushabiki wa mambo ambayo kimsingi yamewazidi umri. Siku wakifika umri wa kuwa na familia wanajikuta hawajaweka msingi wowote vichwani mwao, wamejaza magalasa tupu, ndio hawa hawa wanaanza kubet, "mimi mke wangu lazima awe na kipato ili tuchangie huduma." Mwanaume wa namna hii ameharibika akili tayari, hana ukamilifu wa kiume, badala yake amegeuka opportunist. Sisemi tusioe wenye vipato, bali ni kwamba hilo linapaswa kuja naturally sio planned, na huo ndio upendo halisi.

Halafu kuna vijana kutokana na kukumbwa na tabia ya kuiga kila kivutiacho machoni, unakuta hata uvaaji wao, unyoaji, utembeaji, namna ya kutamka maneno n.k. vimebadilika kabisa. Unakuata mwanamume anaongea kwa kubana pua au mwanamume anavaa vinguo vya kubana kana kwamba anataka watu waone "alivyoumbika!" Lol, dunia inakwenda kasi kweli kweli. Fashion industry imetawaliwa na mashoga duniani kote, yaani kuanzia ma-designer, sorry to say this, lakini ndio ukweli mchungu. Sasa fikiria kina Calvin Klein (huyu ni shoga aliyekubuhu kwa msiojua) wanabuni mavazi kumvutia nani? Hii ndio sababu hasa ya wanaume kuhama kutoka kwenye mavazi yetu ya kibabe na sasa tunavaa nguo za kuvutia macho kiasi tunaonekana warembo. Swali je, kuwa tunamvutia nani?

Dunia ya leo ni kawaida kumuona mwanamume anatinda nyusi, anaweka mkorogo, anakalikiti nywele, anaremba kucha, ananyoa "malaika," kiufupi anarekebisha sura ili awe mrembo. Hivi tunakwama wapi lakini? Dr Shika alipotangazia dunia kwamba ni multi billionaire ghafla alizungukwa na mabinti warembo lukuki, wala sura yake haikuhesabiwa kitu. Sasa wanaume tunaotafuta kuwa na mvuto wa baby face, vijana soft mayai, huu ni uanaume kweli? Mtu wa aina hii atamudu dhoruba za familia? Ndio maana ziko familia ambazo mke anaogopwa kuliko mume, yaani mke ni kama ndiye baba wa mji!!

Unakuta kijana anashindana mapozi na wanawake, halafu muda mwingi yuko na makundi ya wanawake tu. Kijana kajiweka soft kama mwanamke ambaye yeye anatumia mwanya huo kuwakamata vijana walioharibika akili!! Sijui lengo hasa ni kumvutia mwanamke? Kwamba siku hizi vijana wanatafuta kupendwa na wanawake wakati mwanamke sio jukumu lake hilo kwani mwanamume ndiye hupaswa kumpenda mwanamke. Kutafuta kupendwa na wanawake ni kujishusha hadhi na kuwa level moja na wanawake kwani wao ndio hutafuta kupendwa. Ndio maana watu wa namna hii kwa kiasi kikubwa kampani zao ni wanawake, wanajipodoa kama wanawake, wanaitwa effeminate. Wako tayari kufanya lolote kutetea makosa ya wanawake hata kama yako wazi kwa kutafuta kupendwa. Ni lini basi watafikiri jinsi ya kuhudumia familia zao siku za usoni? Wanapata wapi mawazo ya wanaume wenzako kama watu wao wa karibu ni wanawake? Tena unakuta wengine wametoga masikio na pua, wanavaa hereni, wenyewe wanaita vipuri, ama kweli maajabu hayaishi. Wanawake wanavaa mavazi ya kiume wakati wanaume nao wanajipamba kike, wanatengeneza neutral gender. Huku ni kuharibika akili.

Tena wako vijana wengi wameingia kwenye ndoa kwa mtazamo usio sawa kabisa. Unakuta mwanamke anavaa vinguo vya kuonyesha maungo, amekwenda kwa mchina kuongeza tako, ni mtumiaji pombe, ni mtu wa kujirusha viwanja n.k. eti unaamua kumchumbia na kumuoa ilhali dalili zote za kutofaa kuwa mke ziko wazi kabisa. Unajidanganya eti utamwekea masharti abadilike, huu ni ujinga uliotukuka, akili yako imeshaharibika wewe!! Unatekwa na mwonekano wa nje ukidhani mke ni kama kahaba ambaye ukishalala naye nafsi inaridhika. Mwanamke atabadilishwa tabia na watu wa kwao akiwa hajavunja ungo, lakini kwa sababu na wewe ushaharibika akili, unaona nyeupe kuwa nyeusi. Akiingia ndani huyo ataendelea na maisha yake kama kawaida, vinginevyo jiandae kupambana na madai ya haki sawa. Mwanamke wa namna hiyo ameshajitoa kwenye fungu la wanaothamini ndoa, amekuwa ni liwazo la wenye mahitaji. Ni mwanamke wa jamii na hakika wewe unayeoa mwanamke wa namna hii kichwa chako kimenoki!!

Unakuta mwanamke ana boyfriend wake ambaye keshamfanya kipozeo chake, afu unajidai wewe ni kidume kumnyang'anya ili umuoe, naye huyo mwanamke kwa kukuona ulivyo lofa anakuapia, "nimeshamwacha kabisa na namba yake nimefuta." Afu na wewe unajisifia kwa jinsi mchumba wako alivyotulia baada ya kukutana na wewe, usijue kuwa amekuzidi mahesabu nawe umekiri ulofa wako. Kawaida ni kama mazoea, jiandae kwa ugonjwa wa moyo. Huwezi kuoa mwanamke wa jumuiya, atakuzuga tu ili aingie ndani kwa sababu umemwahidi jambo kubwa maishani mwake ambalo "mtu wake" hajamwahidi.

Hoja ya mwisho kwa sasa ni tamaduni za kuiga. Unakuta mtu ni mwanamume kwa mwonekano lakini akili yake na matendo yake ameyaweka level moja na wanawake, hajioni kama tofauti, amegeuka mwanaharakati wa "ukombozi" wa mwanamke. Haijulikani mwanamume huyu anataka mwanamke akombolewe kutoka utumwa upi hasa, ikizingatiwa maisha ya kifamilia yalikuwa bora tangu zama za wazazi wake. Huu ni upuuzi wa kimagharibi ambao sasa umepandikizwa mpaka mashuleni. Mwanamke hatokuja kuwa sawa na mwanamke hata siku moja, hata kama ubadilishaji wa jinsia utaendelea. Hivi wewe mwanamume unayepigania usichokijua unaona uko sawa? Huoni hata maumbile, namna ya kufanya maamuzi hasa under stress, pressure n.k. kuwa ni tofauti? Mwanamume ni kiongozi kwa kuzaliwa, mwanamke ni kiongozi kwa kufanywa!! Wewe unayeshabikia mambo ambayo ndiyo yamepelekea kuua umoja wa familia umeharibika akili kwa kunakili mambo usiyoyajua. What a shame!! Wewe unayeiga umekuwa mtumwa wa fikra za kimagharibi. Umedharau vya kwenu, umekataa maadili ya msingi, umekuwa msukule unayeendeshwa na kila uvumi upitao. Umeharibik akili kweli kweli. Mwanamume wa namna hii huzaa mapooza, watoto wakiwa hawaeleweki yupi wa kike yupi wa kiume. Niishie hapo kwa sasa



Wavulana wanashindana kuwa wasichana, na wanawake ktk ndoa wanakazana kuwa wanaume! Painful



Yaani mkuu ni aibu mno. Zamani mwanamke ndiye aliyekuwa analia machozi kwa kutoamini kama kweli kavishwa pete!! Mpaka wakati wa ndoa ilikuwa ni kilio kwa binti, sasa siku hizi sijui wanaume ndio wanakuwa hawaamini kama wamekubaliwa kuoa hawa mabinti!!?

Maana yake hapa ni kuwa kijana ndiyo anakuwa amebahatika ku,woa binti, ila huyu mke wala hana pressure na jamas. Hivyo kudumu kwa ndoa za aina hii kwa kiasi kikubwa kunategemea utii wa mwanamume kwa mkewe. Mke ni kama hana cha kupoteza isipokuwa mume, na hivyo mwenye ndoa hapa ni mke. Huu ni upuuzi wa hali ya juu na mwanamume wa aina hii keshaikana asili yake.



Wanavyosema wao eti ile ni ishara ya appreciation for being accepted kumuoa binti, lakini ile ina maana nzito sana na haishii pale tu, kwa taratibu za kimila za jamii zingine kupiga goti inatoa tafsiri ya kwamba kwenye jambo zito/kubwa uko tayari kupisha na kukaa kando huku yule uliyempigia goti ukimuona ndio anastahili kuongoza kimaamuzi.

Nachoshukuru kuna jamii huu upuuzi wa kupiga goti kwa mwanamke haupo kabisa ikiwemo ya kwangu mimi.
 
Maelezo yamebeba hoja za msingi sana. Mwanaume ni kiongozi tangu kuzaliwa. Mwanaume amebeba kusudi la Mungu. Mwanaume akibadilika na kuacha misingi ambayo Mungu aliiweka, hapo ndipo anapoanza kuangamia. Hawezi kubaki salama.
Dunia inamuheshimu mwanaume, endapo ameishika misingi ya Mungu. Ila dunia inamdharau mwanamke (inamwona amepitwa na wakati), endapo ameishika misingi ya Mungu.
 
Back
Top Bottom