Wanaume wa Ukweli karibuni.

Wanaume wa Ukweli karibuni.

Mzalendowadamu

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2016
Posts
218
Reaction score
319
Nimeamua kutoa ushauri wangu kwa wanaume wenzangu juu ya namna ya kujiongezea ufahamu juu ya mambo mbalimbali ya ulimwengu na walimwengu, hasa wale viumbe tata waitwao wanawake. Mwenzenu ninapenda kujipatia ufahamu kupitia nyimbo za kale zenye ujumba ambao kwa kiasi kikubwa unakinzana na upotoshaji wa nyimbo za vijana wenzangu wa kisasa. Mfano:-
Masheji wangapi... naota nadanganywa Vs Hainaga ushemeji tunakulaga!!
Pombe sio chai (marijani) Vs Mitungi Mikasi !!
Wosia wa baba (jiepushani na anasa) Vs Nakula ujana ... wananita popo nakeshaaaa!!
Hii ni mifano michache ambayo nimeitoa ili kufahamu jinsigani ujumbe unakinzana katika nyimbo hizi. Ushauri kwa wanaume wenzangu mbao tumepangiwa kula kwa jasho, tujitahidi kusikiliza nyimbo hizi za dunia ya analog na manual kuliko hizi za dital na auto , ili kujiongezea busara.
Tafadhali kama unajua nyimbo zingine zinazo kinzana ujumbe, weka hapa ili tujuzane.
 
Back
Top Bottom