Possibly, kuna wanawake wanatamani kuwa wanaume...lakini kuwa mwanaume haimaanishi kuwa stiff all the time to what you're doing, ndio maana kuna jokes za apa na pale, hivyo mahali kama hapa ndio watu wanaona ni sehemu ya ku relax. Sio vyema kumlazimisha mtu awe kama unavyotaka, kila mtu ana life style yake na ana approach yake ya ku handle mambo yake. Otherwise, huyo bado binti na hawaelewi vyema wanaume walivyo.
Dah..si bure Kuna kitu wanaume wamekufanya....[emoji2960] https://www.jamiiforums.com/index.php?threads/1610844/Nimekuwa mfuatiliaji wa huu mtandao not so long, mwanzoni sikuweza kujiunga kwasababu sikujua namna ya kufanya hivyo. Baadae nikikutana na mtu ambae pia ni mtumiaji wa huu mtandao ndio akanipa ABC's za namna ya kujiunga.
Nilikuwa naiona kwenye suggestions ninapogoogle jambo, nikavutiwa nao sana. Ila nikajikuta nakuwa msomaji tu na nilitamani sana kuwa mmoja wa members humu. Hatimae nikafanikiwa.
Nilijiunga na nikaendelea kuwa msomaji tu hadi hapo nilipoamua kuwa mchangiaji pia. Ila nilivutiwa sana na jukwaa la MMU na CC.
Kwa muda wote nimekuwa nikishindwa kuwaelewa members wa kiume wa humu ndani. Ni wako na tatizo gani? Ni malezi mabovu,stress,kukata tamaa,elimu duni(nieleweke sio ya darasani tu) au tatizo ni nini haswa?
Wengi wao sio wastaarabu kabisa, mtu aweza kuleta mada yake badala wachangie kwa hoja wao ni matusi tu na hii ni hata jukwaa la siasa ambapo ningetegemea kuwakuta wenye weledi na hoja madhubuti kama ilivyo sifa ya mtandao huu(home of great thinkers)
Kuna siku nilileta uzi nikashambuliwa sana kwa matusi, nasikitika niliwajibu kulingana na level yao ya thinking ila i was not proud of it at all.
Hivi nyie binadamu wenye kuitwa wanaume haswa wa humu ni kwasababu gani hamna maadili na hamjielewi?
Hii inatupatia picha wazazi watarajiwa kuwa makini sana na watu tunaotaka wawe baba wa watoto wetu, hivi kama baba wa familia anakosa maadili na upeo namna hii ataiongoza vipi familia yake?
Kuna wakati nikiona mwanaume ana app ya jf kwa simu yake namtafakari sana, namchukulia kitofauti kidogo. Nashukuru mdogo wangu sio member humu.
Wapo wachache atlest ukisoma unafarijika kuona kuwa angalau bado tuna akina baba bora kwenye jamii zetu. Tambueni nyie ni wachache kwa idadi duniani, kwahiyo mnapaswa mjitafakari sana je mnastahili kuitwa wanaume au ni viumbe wenye uume tu?
Kuitwa mwanaume tayari ni jukumu, hivyo tangu ukiwa mdogo unapaswa kukuzwa hivyo. Sasa kama mlipitia malezi mabovu kutoka kwa wazazi its about time dunia iwafunze.
Acheni kujisifia mambo ya kipumbavu, mna jukumu kubwa sana hapa duniani, kumbukeni mlipoteleza kisha mchukue hatua.
Ipeni JF heshima yake kama ilivyo kauli mbiu yake.
UPDATES:
Ukitaka uamini kuwa nililoandika ni kweli tupu bila ya chenga basi soma comments za kwenye huu uzi.
Keshageuzwa geuzwa huyu ndomana analia na jfhuyu Uvelia haijui JF ndo kwanzaa ametumbukiamo humu juzu tu. wacha achemke ndo ataijua vizuri. huu mchezo hautaki mihasira yeye anadhani ni sawa na kule INSTA au TWIT alikojifunzia mitandao
Soma uelewe, wangekuwa wawili watatu maybe tungesema tatizo ni dogo. Ila wengi wenu hamjielewi. Wapo wachache sana wanaojielewa.Umekosea heshima wanaume wa JF
Ku generalize inaonesha na wewe pia hujielewi, kukoseana na wanaume wawili watatu humu isiwe sababu ya kuwasema wanaume vibaya
Pia elewa kwamba wanaume waliopo umu ndio wanaume waliopo mtaani, pengine hata baba yako pia yupo humu
Mwisho ombi lako linaendelea kufanyiwa kazi (umegusia swala la kupata na baba watarajiwa wa watoto wako), be patient utapata hitaji la moyo wako.
Ukute ndo clas mate wako uliemtegemea na leo unamualiko wake jioni utamtembelea ha ha haaaKwani wewe shida yako nini?
Malezi yako mabovu peleka stendi.
Oohh kwahiyo kwa wanaume tu huwa ndiyo iko hivyo ila kwa wanawake huwa mnalazimisha kuwa tuna stress kutokana na hizi hizi comments zetu za humu siyo?
kweli kabisa kuna mjinga mmoja jana kakurupuka huko kaleta uzi huu
Ndege iliyobeba wachezaji wa YANGA imekutwa imeibwa keki, soda na sabuni za chooni!
UTANI: Ndege iliyowabeba Wachezaji wa Yanga SC leo kumekutwa kumeibiwa Headphones, Mikate, Keki, Soda, Bia na Sabuni za Chooni
Utani tu huu vyura 🐸🐸 🐸 msipanikiwww.jamiiforums.com
Tena nawasiwasi hao unaowazungumzia ni MBUMBUMBU FC
kwani kina evelyn salt na Money Penny ni wanaume hao?? wapo kifungoni ebu jiulize wamefata nini huko rumande? endelea tu kudhani wanaume tu ndio wenye shombo..
Kuna wanawake physicaly nawajua na wana ID za kiume..wanashombo hata za samaki zina afadhali..we kaa ukituhukumu wanaume tuliojiweka wazi kua ni wanaume..Kuna watu humu wana jinsi mbili mbili,tukisemwa wanaume Anakaa kwa wanawake,wakisemwa wanawake anarudi kiumeni..
Asee member wa JF sio kama wa Insta au badooo...Lawama zako ziweke kwa wote usitaje JINSIA kabisa maana ukiweka jinsia basi usi include wote Mtaje muhusika wako unae mlenga ila kusema "wanaume wa jf" unakosea.
ukitaka kujua unakosea
Nitajie ID 10 ambazo huwajui kwa kuwaona Live(physicaly) ila umewajulia huku JF ambao wewe unasema ni WANAUME...ukiweza taja ID 10 za wanaume nakupa vocha ya 10,000.
Nataka tu ufahamu kuwa JF member wachache sana walio amua kujiweka live kuwa ni ME au KE...wengi wao wanacheza nafasi zote KE na ME.
mimi na wanaharakati kama wewe ni quite different, I can learn nothing from youUkifundishwa fundishika, kuwa mwanaume.
Wanawake wengi wanawapiga wanaume kwenye kudanga, huwezi kuona sana JF.
Kuna msemo wa Kiingereza "All is fair in love and war".
Wengine JF bila drama ni kama chipsi bila kachumbari.
Ukitaka kubadilisha JF ni vigumu kuliko kuchunga paka kama ng'ombe.
Pia, ni vizuri uka address specific examples, maana hapa bila specific examples utaweka mtego wa panya unaoshika mpaka panzi.
Naona umeshahukumu wanaume wote wenye app ya JF.
Wakati unaweza kukuta hata wahashamu na wahadhiri wenye staha zao wamo.
Ukiongelea mtu specific, kwa ushahidi specific, hata mimi naweza kukuunga mkono nikijiridhisha.
Ukitoa shutuma za jumla haisaidii, inatengeneza vita zaidi kati ya wanaume na wanawake, unakuwa kama unataka kuzima moto kwa kuumwagia petroli.