Wanaume wa Dar buana...!

Daladala imejaa, unapanda huku ukijua una nguvu na uwezo wa kusimama. Kwanini nikupishe?
Mimi huwa napisha wazee tuu. Basi kwa huruma tuu.
 
Mimi ndio mana nimeanza kuweka kibubu
mke wangu asije pata adha kama izi.

na akiwa ana mimba ama timu ya watoto
Kuanzia wawili basi ntajitahidi asipande
dala dala atumie bajaji nk.
 
Huruma yake anailazimishia kwa mtu mwingine, na mara nyingine wakina mama wenye watoto huwa wanawatumia watoto kama ngao ya kutaka kupishwa gari zinaweza kuwepo nyingi tu ila anajua mtampisha tu hivyoanaamua kujitoa ufahamu ila kibinadamu hakuna mwenye jukumu la kumpisha ila wote tunapaswa kuwa na huruma sio awe mwanamke tu au mtu fulani tu, tukio lako linafanana na safari moja natokea dodoma enzi hizo akapanda mtu mwenye ulemavu mzee akampisha halafu akaanza kumsema kijana ambaye alikuwa amelala kuwa vijana hampendani, tena mwenzio mlemavu...ni kukosea kufikiri maana kama umejitolea kusimama maneno ya nini? watakuona umesimama watakupisha pia maana hata kama anaamini kuna mungu na kuna baraka kwa mapovu hayo sidhani kama alipata hizo thawabu kwa kweli!
 
Uko sawa kabisa boss, kama hujisikii kupisha kaa tu sio unapisha huku unasema fulani ndio alitakiwa kupisha
 
Mimi ndio mana nimeanza kuweka kibubu
mke wangu asije pata adha kama izi.

na akiwa ana mimba ama timu ya watoto
Kuanzia wawili basi ntajitahidi asipande
dala dala atumie bajaji nk.
Ni kweli ila si unajua riziki anagawa muumba
 
Sina kawaida ya kumpisha siti mtu mzima na akili zake aliyeamua bila kushurutishwa na mtu kupanda daladala iliyojaa akati mji una daladala nyingi tuu!
 
"Kinamama waheshimiwe kote duniani"
 
Sina kawaida ya kumpisha siti mtu mzima na akili zake aliyeamua bila kushurutishwa na mtu kupanda daladala iliyojaa akati mji una daladala nyingi tuu!
Haha kuna baadhi ya maeneo huwezi kupata siti hata iweje
 
Labda huko Dar..ila huku niliko mimi inawezekana kabisa, kama ukishindwa kabisa panda bajaji.
Juzi nimepanda daladala tukafika kituo kimoja kikubwa kuna daladala nyingi hatari, ile nlopanda mim ikawa imejaa..kuna mzee mmoja akapanda af tall kimtindo kwahyo ilikua lazima ainame, akaja kusimama jiran yangu akijua ntampisha haikuwa ivo.!
Watu wakawa wananiangaliaa nikaona mengi ya mengi nakavaa zangu earphones nakula mziki taratiibu!!
Haha kuna baadhi ya maeneo huwezi kupata siti hata iweje
 
Nonsense kabisa.......aliyemdogo humpisha mkubwa.....mwanaume yuko juu ya mwanamke kiafrika hivyo mwanamke kukalia kiti huku mwanaume kasimama ni utovu wa nidhamu..ni sawa na mtoto kukaa kitini half mkubwa asimame....
Mwanaume ni kichwa cha mwanamke, kichwa cha mwanaume ni Mungu....
 
Aiseeee....
 
Usinikumbushe mimi mambo ya kusaidia siti au kusaidia mtoto kwenye daladala.

Niliwahi msaidia mdada kubeba mtoto kufika mbele sikumuona. (Alishukia njiani halafu kuna wenzake walimuona sasa)
Nikampeleka mtoto polisi, nikaambiwa inabidi ukakae nae uache mawasiliano tutoe tangazo mamake akipatikana umlete.
Nikawaaga polisi naenda kununua vocha.
Sikurudi tena!!

Siku nyingine nikamsaidia mjamzito siti, katika kuinuka kumpisha simu ikadondoka kwenye siti akaificha kifuani, (hakuwahi kuizima).
mara ikapigiwa...sasa mlio wa simu naujua nikaanza kujisachi ....sioni simu!!! Kuskiliza vizuri inaitia katikati ya manyonyo ya mjamzito...khaaa!! Nikamuuliza vipi imekuwaje!? Eti nisameheee.

Kuanzia hapo nikajiona msaada wangu unakuwaga na gundu tu BORA MPEANE WENYEWE (WANAWAKE/WANAWAKE) msaada.
 
Kwa hali hii tutatoka kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…