MwanaHaki
R I P
- Oct 17, 2006
- 2,401
- 710
Nadhani mtoa mada angetumia Waefeso 5:25-33 mada yake ingekidhi zaidi hoja zake. Hebu tazameni kwanza hapa.
Wanaume tunaamrishwa kuwapenda wake zetu kama Kristo alivyolipenda Kanisa; yaani tuwapende kama tunavyozipenda nafsi zetu.
Wanawake wameamrishwa kuwatii waume zao kwa kuwa mume ndiye kichwa cha familia, kama Kristo alivyo kichwa cha Kanisa.
Ukweli ni kwamba, siku hizi, familia nyingi za Kikristo wamesahau misingi hii. Utakuta mke anajiamulia atakavyo, licha ya kwamba mafundisho yote ya dini aliyapitia, na alipokea Kipaimara na Komunyo ya Kwanza (nawazungumzia Wakatoliki). Bado anaenda kanisani na anapokea Ekaristi Takatifu. Lakini nyumbani kwake, mambo ni tofauti. Je, kuna ulazima wa kuendelea kuwa Mkristo iwapo unashindwa kuifuata misingi imara iliyowekwa na Kristo?
Ukiangalia, kwa upande mwingine, Kanisa Katoliki halitofautiani sana na mila na tamaduni za Kiafrika. Wanaume ndio waliokuwa watawala wa familia, na waliwapenda wake zao kwa dhati, na wake zao waliwatii. Hivyo hata malezi nayo yalikuwa yenye baraka, japokuwa Ukristo haukuwapo.
Misingi iliyoletwa kwenye Ukristo si migeni; ni jinsi na namna ya kuishi kwa upendo, kwa amani. Leo hii utakuta nyumba nyingi, baba akitoka kazini anapitia kwenye baa, anakutana na washkaji zake, wanajimwaga kwa pombe na nyama choma. Hajui nyumbani kama kuna chakula au la. Hajui kama watoto wanadaiwa ada za shule au la. Akirudi nyumbani, saa tano au sita usiku, amechoka, anataka huduma kwa mkewe. Na kwa kuwa ni haki yake, mke atampa tu hiyo huduma.
Hayo mapenzi gani? Sasa kwa nini mke asichoke na kutafuta wa kumfariji nje ya ndoa? Huyo mke atakustahi vipi wewe mume usiyejali?
Matatizo mengi wanaoyasababisha ni wanaume, tusiwalaumu wanawake, kwani wao ndio wanaoshawishiwa. Ukiona mkeo ana dalili za kutoka na mpango wa nje, jua ya kwamba wewe ndiye chanzo. Jichunguze.
Sina zaidi ya hapa. Natumai ujumbe umefika.
25 Nanyi waume, wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipenda kanisa, akajitoa mwenyewe sadaka kwa ajili yake. 26 Alifanya hivyo, ili kwa neno lake, aliweke wakfu kwa Mungu, baada ya kulifanya safi kwa kuliosha katika maji, 27 kusudi ajipatie kanisa lililo takatifu na safu kabisa, kanisa lisilo na doa, kasoro au chochote cha namna hiyo. 28 Basi, waume wanapaswa kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. 29 (Hakuna mtu yeyote auchukiaye mwili wake; badala ya kuuchukia, huulisha na kuuvika. Ndivyo naye Kristo anavyolitunza kanisa, 30 maana sisi ni viungo vya mwili wake.) 31 Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Kwa hiyo, mwanamume atawaacha baba na mama yake, ataungana na mkewe, nao wawili watakuwa mwili mmoja." 32 Kuna ukweli uliofichika katika maneno haya, nami naona kwamba yamhusu Kristo na kanisa lake. 33 Lakini yanawahusu ninyi pia: kila mume lazima ampende mkewe kama nafsi yake mwenyewe, naye mke anapaswa kumstahi mumewe.