Leo naomba niongee na wanaume wenzangu.
Kwanini sisi wanaume hatupendani?
Tunawalaumu wanawake kuwa hawapendani ilihali na sisi pia hatupendani. Nitaeleza kwanini nasema hivi.
Unakuta mtu kwa makusudi anafahamu kuwa huyu mwanamke ni mke wa mtu. Mwanaume mwenzangu kamtolea mahari, kajipiga piga kufanya sherehe na anafanya kazi kwa bidii ili kumtunza mkewe(japo maisha yana changamoto nyingi sana) lakini bado atamtongoza (mke wa mtu) na atalala nae.
Kwani mbona kuna watu hawana huruma na wanaume wenzao namna hii? Ina maana hawafahamu kuwa wanachokifanya ni kuharibu ndoa na nyumba ya mwanaume mwenzake?
Au ndio tumekosa upendo kiasi hicho? Ndugu zangu kama sisi wanaume tungekuwa tunapendana kusingekuwa na visa vya kufumaniana na wake za watu.
Tufikie hatua za kuwatakia heri wenzetu waliooa, tusiwe sehemu ya kuvuruga ndoa zao. Sikatai kuna baadhi ya wanawake ukiwa unamtongoza ukimuuliza ikiwa ameolewa anakataa, lakini mara nyingi wanawake huwa wawazi kuwa wameolewa.
Wanaume tupendane, tusiharibiane ndoa.
NB: Hakuna lolote lililonisibu, nimeandika kwa kuzingatia jinsi mambo yalivyo katika jamii.