Wanaume tuoneeni huruma dada/mama zenu

Wanaume tuoneeni huruma dada/mama zenu

haijalishi kama alikubali au kukataa,ila main poin ni jinsi gani mwanamke anaweza kua kigeugeu kwa kitu alichokitaka mwenyewe
Hivi nawe inakuingia akilini kabisaa hiyo kauli hadi uamue kuwa sperm donor???
 
Hili swala huwa linaniumiza sana kichwa, huwa najaribu kuvaa uhusika wa waliotelekezwa najikuta najenga chuki na wanaume wanaotelekeza mimba au mtoto akizaliwa, nimekua mshauri sana kwa marafiki zangu pale wanapowapa mimba wasichana ambao hawakua machaguo yao; kati ya mambo yanayosababisha hiyo hali ni;
  1. Kutojadiliana na mwenza wako juu ya swala la mimba endapo litatokea nini itakua hatma ya hiyo mimba. Wenza wengi hawajadili hili jambo kabla ya kushiriki tendo la ndoa, na baada ya kutokea kila mtu anakua na mtizamo tofauti, kuna wengine hadi wameingia kwenye uadui mkubwa baada ya kutokea kwa mimba.
  2. Kutokuweka wazi kwa wazazi/walezi, hii hufanya watu kuwa na uoga endapo itajulikana kwa yule mtu asiyependa ajue kuhusu mimba hiyo. Mfano mke/mme.
  3. msichana kubeba mimba kwa kufikiri ndiyo njia ya kummiliki mwanaume moja kwa moja, hiii inatokea mara nyingi sana hasa inapotokea kama mwanaume ana msichana wake na ana malengo ya kumuoa sasa akinzisha mchepuko anataka amuovertake njia kuu kwa kubeba mimba, na mara nyingine wanafikiri ukibeba mimba ndo utapata upendo wa mwanaume.
 
ha

hahaha mkuu unanivunja mbavu,tena anakwambia kabisa kwamba kama sio damu yangu jaribu kutoa,utanitafuta
Noma sana aisee..Halafu anaenda kujitapa mbele ya watu,flani ana mimba yangu..Wakati hata mia ya matunzo hatoi
 
single parent Mara nyingi sana inaleta migogoro, na mama anakuwaga muhanga wa hili but hujitoa muhanga kuhakikishaa mtoto wake anapata mahitaji yote muhimu

√√ single parent ya baba Mara nyingi huwa haitokei sababu mama vigumu kuacha mtoto na hapa utamkuta baba anampeleka mtoto kwa ndugu zake akalelewe huku anachkua vimada wengine


√√ wanaume kama jogoo anampanda temba ,kazi ya kulea vifaranga ni Juu yke kuku jike
 
Pole sister! ila kuna kitu watu huwa hawatambui,wanaume huwa si wepesi wa kuongea yanayowasibu kwenye mahusiano ila wanaume wanateswa sana na wanawake japo siungi mkono tabia ya kukimbia familia ila kuna wanawake pasua kichwa aisee,nina jamaa yangu yeye toka ameoa ana miaka mitatu,mke hata wakizinguana kidogo anasepa kwao miezi 6 mpaka karibia mwaka.sasa saa hizi ana ujauzito huyo mdada baada ya kua akibeba unaaribika,alafu makosa yenyewe yanamtoa hom kwake ni makosa ya kawaida tu,kuna muda jamaa huwa anatamani hata amuache kabisa sasa hali hyo ikiendelea si ipo hatar ya jamaa kutelekeza mke na mtoto? sema wengi huwa mnatumia watoto kama mwavuli,ukisha kua na familia inabidi ujifunze kukaa vizuri na mwenzio kwa ajili ya ustawi wa familia,wanaume sio watu wa ku take action kirahisi ila akichukua hua aangalii side effect ya uamuzi anaochukua.Maudhi yakizidi familia huwa haina uzito sana hasa katika kuchukua uamuzi mgumu
umwsema vema kaka,,,, hakuna anaeunga mkono kumuachia watoto mwanamke..... ila kiuhalisia wanaume huwa tunaumizwa sana na hatupendi kupiga makelele ovyo... unakomaa till ukiona hii sasa taabu ....kimya kimya unachukua maamuzi magumu... tena magumu kweli.... na wanawake huwatumia watoto kama ngao na kuwalisha sumu ......mjiangalie na nyie msilaumu wanaume tuuu......kama kichwa cha familia,,,,, unaweza chukua uamuzi bila kujali what next,,, na maisha yakasonga kama kawaida....
 
umwsema vema kaka,,,, hakuna anaeunga mkono kumuachia watoto mwanamke..... ila kiuhalisia wanaume huwa tunaumizwa sana na hatupendi kupiga makelele ovyo... unakomaa till ukiona hii sasa taabu ....kimya kimya unachukua maamuzi magumu... tena magumu kweli.... na wanawake huwatumia watoto kama ngao na kuwalisha sumu ......mjiangalie na nyie msilaumu wanaume tuuu......kama kichwa cha familia,,,,, unaweza chukua uamuzi bila kujali what next,,, na maisha yakasonga kama kawaida....
ndio maana usije ukamsikiliza mwanamke au upande mmoja tuu katika kusuluhisha,anaweza kuja jamaa hapa akafunguka hadi ukashangaa
 
madada wakati mwengine huwabambikia wanaume watoto sio wao!! mkiambiwa suala la DNA mnaruka mita 100, ufanano wa sura si kigezo cha mtoto kuwa wako kwa maana inawezekana hilo njemba jengine pia limefanana na hiki kidume!!! msibebeshe watu mizigo sio yao kwani nanyi pia mnakuwa na majukumu! na pengine unakuta mwanamme wako amekufumania upo na njemba nyengine ndiyo akakuacha kisha unadai wakati anakuacha alikuwa na ujauzito wako
 
ndio maana usije ukamsikiliza mwanamke au upande mmoja tuu katika kusuluhisha,anaweza kuja jamaa hapa akafunguka hadi ukashangaa
silaha yao kubwa ni midomo yao.......wanaume yetu maamuzi kimya kimya.... na mwisho wa siku suluhu ni ya watu wawili tuuuu.... sijui vikao vya usuluhishi ni umbea tuu...
 
Back
Top Bottom