Wanaume tunarogwa sana na hawa wanawake

Wanaume tunarogwa sana na hawa wanawake

Hapo ndipo ilipo sababu ya kukuloga.........na nitakuloga mpaka ukae sawa..........

Wakati mwingine hii siyo sababu ila ni wanawake kutojiamini. Baadhi wamekutwa na mauaji ya waume zao na kutengwa na jamii. Maana hujui chemical contents ya dawa anakupa mganga. sijui kwanini mnaweka imani kwa waganga na kuwapa nguvu wasizositahili. Wengine mnaishia kuingiliwa kimwili na waganga wa kienyeji mkiwa bado mnaamini ndo dawa inavyofanya kazi. kumbe hata hapi nawe ushachepuka, kitu unachopigania kwa mwenzi wako.
 
Mngekuwa mnalogwa sana wengi wenu mngekuwa mmetulia na wake/wapenzi wenu bila mbwembwe za nyumba ndogo na michepuko kila mahali.

Hivyo vitu mnaweza mkawa mnalishwa kweli ila vitakuwa havifanyi kazi,au pengine mmekomaa kiasi kwamba hamlogeki tena. Maana mtu hawezi kuwa na mke aliyemloga bado akamtafutia nyumba ndogo, nyumba ndogo nae amloge na bado akatafuta na mchepuko mwingine.

Umenifanya nicheke siku nzima leo.
 
Mwamini Mungu kwa Imani yako utakuwa salama. Lakini usione haya pia kumpenda mke wako eti utaambiwa umerogwa, hakuna kitu kama hicho.
 
ahahahah jamani niulize na hao waganga wapo manake sikuizi kila kona mpaka kwenye maguzo ya umeme unakuta matangazo mganga,anatibu,kumtuliza mume hasharati,kunyanyua nyota,kumvuta mpenzi alokua mbali,kupanda cheo kazini,kurejesha heshima ya ndoa,kumuinamisha mume/mchuchu.. yani matangazo mpaka unacheka..
 
Kwa vitu nisivyopenda ni kuwa na ukaribu na mtu mshirikina achilia mbali mke wangu. Nikijua tu hakika tutaachana. Washirikina wana itikadi flani za kipumbavu, kila awazacho huwa ni ushirikina tu.
 
Kuna jirani yangu juzi kanichekesha sana, yeye ameoa na mm bado, sasa mke wake akamtengea chai kwa vitumbua, mme wake akaniita, mimi nikadhani kuwa ananikaribisha chai, kumbe aliniita amseme mke wake mbele yangu, akasema hivi "Mke wangu njoo, akaja, bwana ...nimekuita hapa nilisema hili swala mbele yako, mke wangu amekuwa akiniwekea dawa kwenye chai na mboga, mizimu ya kwetu ina nguvu sana na huwa nagundua na sijui nia yake ni nn!!!!
 
Wewe usiwe na shaka.......nimekuweka kwenye chungu muda mrefu........huna neno.......relax...........

Ila sina shaka, najua umeniloga kwa nia njema! Ninachohitaji kwako ni mapenzi ya dhati, kama hilo ninalipata I don't care kuhusu ulozi wako
 
Uchawi na nguvu zidaiwazo unao, haupo!

Yaitwayo matendo ya kichawi ni matokeo ya ujinga tu.

Bila shaka ndo maana ukaitwa 'imani'.
 
Na tuwaloge tuuu..... Ha ha hivi kuna uchawi wa mapenzi kweli au ndio kuweka majani ya mipera kwenye chai unadhani dawa??
 
ahahahah jamani niulize na hao waganga wapo manake sikuizi kila kona mpaka kwenye maguzo ya umeme unakuta matangazo mganga,anatibu,kumtuliza mume hasharati,kunyanyua nyota,kumvuta mpenzi alokua mbali,kupanda cheo kazini,kurejesha heshima ya ndoa,kumuinamisha mume/mchuchu.. yani matangazo mpaka unacheka..

He! Kuna njia ya kumvuta mpenzi kwa karibu zaidi ya hii ya dot com?
 
Katika nchi nyingi za DUNIA ya 3 hasa kusini mwa jangwa la Sahara suala la mtu kwenda kwa mganga ni utamaduni, na kuna tofauti kubwa ya mtu kurogwa na mtu kukuendea kwa mganga.
Wanaume kwa wanawake ni wateja wazuri wa waganga si tu ktk masuala ya MAHABA bali hata ktk masuala ya SIASA, uchumi n.k. Katika kila watu 10, watu 8 wanaenda na kuamini tiba zitolewazo na waganga. 60% ya watz wanatumia huduma za waganga hii ni kwa sababu huduma za afya zimezorota.
 
Back
Top Bottom