Wanaume: Tuacheni tuolewe basi

Wanaume: Tuacheni tuolewe basi

Hakuna kitu kibaya kama kutaabikia mambo ambayo aliyeyaumba yupo!.Inawagharimu wengi sana!
 
Habarini za usiku humu ndani bila shaka mko vizuri.

Kumekuwa na malalamiko mengi humu ndani kutoka kwenu wanaume, sijui niziite lawama ama nini hata sielewi lakini hamuishi kutuongelea, ati wanawake tunalazimisha kuolewa huku mkijua fika kuwa mwanamke na kuolewa ni muhimu.

Sasa jamani hamtaki tuolewe ama? maana tusipoolewa pia hamtokosa neno la kutuambia (binadamu haishiwi maneno).

Wakati mwingine unakuta mwanaume umri umekwenda kweli kweli, hapo kasugua gaga kupata walau mpenzi ajenge naye mahusiano baadae ndoa, lakini naye pia analalama ati mwanamke anawaza kuolewa mwezi mmoja tu wa mahusiano anaulizia ndoa, wakati hapo alitakiwa ashukuru mungu kakutana na mwanamke mwenye kutaka kuolewa naye anaacha kushukuru Mungu kamwonesha nyota njema asubuh yeye anashangaa kwani kuolewa ni jambo la ajabu? Eti nauliza jamni mbona kama kututupia lawama zisizokuwa na mashiko???

Hili suala la kuharakisha kuolewa sio kwetu tu hata nyie wanaume mnaharaka sana ya kuoa lakini hapa mnaficha uhalisia, wapo wanaume katoka huko ana stress zake sijui anakutongoza kwa gia ya kutaka kuoa mbona hatuwaongelei hapa? mwingne mko kwenye mahusiano miezi mitatu ati anataka akajitambulishe kwenu wakati hata wewe mwenyewe hujamjua vizuri bado... watu kama hawa sijui wanawaza nini vichwani mwao.

NB: Mtuache jamani kama mtu aliset goal aolewe ni lazima liachieve, tafadhali wanaume msiwaharibie watu mipango yao.

Miye nakiri kabisa kwamba ni mimi niliyempigia mama Ngina magoti kutaka kumuoa na hakukubali kirahisi kwa hiyo ni mimi niliyekuwa na mshawasha wa kuoa wa si yeye.....
 
Mo mumooo malafyale hahahahaha

Jina hilo linanikumbusha mbali sana,mwaka 1995 Rungwe Sec School,alikuwepo mwanafunzi wa kike wa Day kwa jina hilo!Kwa kweli nikisikia jina hilo nakumbuka mbaaali mm!
Filomena ole nnyakyusa?
 
Last edited by a moderator:

Hapana malafyale nalipenda tu kabila huwa wananifurahisha sanaaaa
 
Last edited by a moderator:
Hivi nikabila gani wanaongoza kuwataliki wake zao hapa Tanzania?
 
kusubiri mtu unasubiri,yani hata huo msamiati ndoa unaukwepa kabisaaa in his presence...tatizo ni uongo umezidiii banaa,ye ndo unakuta anaisema ndoa afu hana mpango wowote,ukija kugundua ts too late keshakufunua au ulimpa willingly coz unampenda,hata kama utaamua kusepa utabadilisha wanaume wangapiiiii???and mind you sio rahisi kama tunavoandika hapa unakuta mtu unampenda na falling out of love is harrrrd...kuja kupata mwingine hadi mshibane vizuri ujue intention zake unashangaa mwaka miaka miwili imekatika,umri unaenda,loooh...namuachia Mungu nimesurrender hii sekta for now

i see your pain in ya heart, umeandika kwa uchungu hiyo sentensi ya mwisho. pole endelea kumwomba Mungu atakupatia unayefanana naye,usijitangulize,mtangulize Mungu.
Dada yangu mmoja alipata mchumba , yule jamaa alikuwa na safari ya kuja dar, dada alupiga goti na kuomba kwa Mungu kwamba kama huyu mchumba ndiye uliyeniletea, naomba nimwagize salamu na kimzigo nyumbani kwa mzazi na ndugu zangu dar akifika akafikisha salamu na mzigo na asipopotea iwe ndiye. kama asipofika, na akirudi na blablah siye.
kweli jamaa alienda dar, kwa mzazi wala hakufika, akarudi na sababu kibaoooo, haukupita wiki dada akagundua jamaa ana muke imetelekeza huko tarakea
 
umivu kweli ninalo,japo linapungua polepole...ahsante,naamini wakati ukifika ntakuwa nae,
 
Miye nakiri kabisa kwamba ni mimi niliyempigia mama Ngina magoti kutaka kumuoa na hakukubali kirahisi kwa hiyo ni mimi niliyekuwa na mshawasha wa kuoa wa si yeye.....

bora yako wewe unakubali lakini wengi humu wanabisha ati sisi ndio watambuzi
 
Ngoja nikwambie yaliyonikuta. Baada ya kuachana na niliyempenda niliishia kwa Dada mmoja ili nisiwe mpweke. Huyo Dada sasa, Mara weka picha yangu kwenye profile yako fb, mara badili status, kwetu utaenda lini? Nataka unipe mimba yaaani nilijuta hata kumsemesha. Hapo ujue tuna miezi miwili tuu ya kuwa pamoja. Akisikia kuna mtu anayemfahamu anaolewa ndio itakuwa topic ya wiki nzima. Hivi kuolewa ni kuigana? Kwani tunalazimishana? Nikaamua kumpiga chini
 
ahhhh sasa hata hukumuweka hata auze uze sura wazap jmn...vibayaa hvo...lol
 
Ngoja nikwambie yaliyonikuta. Baada ya kuachana na niliyempenda niliishia kwa Dada mmoja ili nisiwe mpweke. Huyo Dada sasa, Mara weka picha yangu kwenye profile yako fb, mara badili status, kwetu utaenda lini? Nataka unipe mimba yaaani nilijuta hata kumsemesha. Hapo ujue tuna miezi miwili tuu ya kuwa pamoja. Akisikia kuna mtu anayemfahamu anaolewa ndio itakuwa topic ya wiki nzima. Hivi kuolewa ni kuigana? Kwani tunalazimishana? Nikaamua kumpiga chini

ahahahahaaa pole sana kwa yaliyokusibu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom