Wanaume punguzeni kututesa, tunaumia jamani

Wanaume punguzeni kututesa, tunaumia jamani

Nimejifunza vitu viwili kwenye mapenzi.

1. Mahusiano ni two way. Nipe nikupe. Nakupenda nipende tupendane. Mahusiano yakiwa ni ya upande mmoja hapo pana uwalakini na Mara nyingi hiyo ni taa nyekundu.

2. Husisha akili asilimia 60 na moyo asilimia 40. Angalia practicality ya matendo na maneno. Kuna mambo mengine yanatokea kwenye mahusiano na unaona kabisa hili hapana ila unasema " nampenda" ahhh wewe tumia akili yako zaidi.
 
Uyo jamaa still yuko na ww ili akitaka sex kutoka kwa mwanamke asisumbuke kuipata.. The Donchop
Hapana. Toka siku aliyoniacha hakuwahi kuniambia lolote juu ya hilo. Sasa nimejitahidi sana kukaa nae mbali, simu simpigii ila mpaka sasa yeye anaendelea kunipigia na hata kunifata nyumbani. Simuelewi huyu mtu ana pepo gani. Hatuna tena maswala ya mapenzi lakini kila inapoingia msg ya msichana lazima ajitete kuwa huyo sio mtu wake mpya. Muda mwingine ananiachia simu yake.
 
Hayo ndio mambo ambayo.sitaki ishu zetu binafsi kuzileta jf
 
bado tu unamaumivu yanakukamua utakufa umuache anaendelea kukamua vidosho weuwee kwani ulizaliwa naye huyu mwanamke woyiii tupa kulee mapenzi siku hizi hakuna ya kuumizana hivyo big nooooo... halaa kwa lipi haswa
 
Pole sana dada..Ngoja nikupe ushuhuda wangu..Uenda utaambulia kitu

Niliondoka kwenda Iraq kutafuta kula..Huku nyuma nikawa nimemuacha mpnz wangu ambaye tulikuwa tumetimiza mwaka na nusu kwenye mahusiano yetu mpaka dakika hiyo...Na kwa kipindi chote cha mahusiano dem alikuwa ananisaidia sana..Mana yeye alianza kushika pesa mapema kabla yangu..

Kabla ya kuondoka nikaamua nimtambulishe home..Nikamtambulisha kwa Sista na mdogo wangu wa kiume..Lengo,nia na dhumuni la kumtambulisha ilikuwa nataka ndugu wamfahamu ili wanisaidie kumtupia macho kidogo..

Kumbe kipindi mi niko kule sista pamoja na dogorasi walitokea kupatana sana na yule binti..Wakawa wanashirikiana kwenye matukio mengi..Kitu kilichopelekea hata ndugu wengi kumfahamu..

Basi baada ya miaka minne ya kozi yangu ya kukwepa mabomu nikarudi home..Nilivyorudi tukaendelea na mahusiano kama kawa..Ila kipindi naendelea nae kuna kamchepuko kalikuwa kanadoea penzi la huyo dada..Sijui hata nn kilitokea..Kidogo kidogo nikaanza kumchukia mpnz wangu..Visa vikawa haviishi..Mapenzi yakahamia kwa mchepuko..

Kifupi mwisho wa siku nilimwacha mpnz wangu nikaendelea na hili balaa jingine..Binti alilia sana aisee..Sista na Dogorasi walikuwa wakinishauri lakini sikushika hata moja..Mwisho wa siku yule binti akawaambia mwacheni tu aendelee na maisha yake..
Huo ndo ukawa mwisho wa mahusiano yetu..Ila dada wa watu hakukata mawasiliano na sista wala dogorasi..Na bado kwenye matukio mbalimbali ya kifamilia kama harusi,misiba alikuwa anakuja kama kawa kitu kilichopelekea kuonana nae mara kwa mara..
Basi miaka ikazidi kusonga..Ila Kilichokuwa kinanishangaza kila tukikutana nae namuona anazidi kupendeza tu..Anabadilisha magari deile..Nikajua labda ananifanyia maigizo..Ikabidi nifanye uchunguzi..Ndo kuja kugundua kuwa mambo yake ni super ile mbaya..Nikabaki najicheka tu
Now kuna biashara wanafanya na sista..Mambo yanawaendea poa..Uwa tukikaa wananitania sana..Wananiita EP(enemy of progress)..Ananiambia Kaboom uenda ningeendelea na ww nisingefika hapa nilipo..

Ukirudi kwa huyu niliyenae ni balaaaa..Ndoa ni chungu...shubiri naiona asali..Unatamani hata Yesu arudi kesho....

Mawazo chanya:Ukiona unamuomba Mungu gari na hakupatii,Basi jua pengine anakuepusha na ajari..Usilazimishe vitu


Very touching story na inajenga pia.

tuchukue tu hatua aisee hakuna namna
 
Wanaume wengi wako hivyo akishapata anaona wewe si kifano chake.usiuzunike sana mungu atakufuta machozi
 
Hapana. Toka siku aliyoniacha hakuwahi kuniambia lolote juu ya hilo. Sasa nimejitahidi sana kukaa nae mbali, simu simpigii ila mpaka sasa yeye anaendelea kunipigia na hata kunifata nyumbani. Simuelewi huyu mtu ana pepo gani. Hatuna tena maswala ya mapenzi lakini kila inapoingia msg ya msichana lazima ajitete kuwa huyo sio mtu wake mpya. Muda mwingine ananiachia simu yake.
Nyie bado mwapendana ila mna mambo ya kitoto.
 
Yaani,.nikujitafutia laana wakati mwingine jamani,.[emoji57]
Watu udhani laana ni mpaka kwa mzazi tu kumbe hata yale unayoyafanya yanakuletea madeni makubwa katika maisha, mwishowe unashindwa kulipa. Na madeni si lazima pesa ivo.
 
Watu udhani laana ni mpaka kwa mzazi tu kumbe hata yale unayoyafanya yanakuletea madeni makubwa katika maisha, mwishowe unashindwa kulipa. Na madeni si lazima pesa ivo.
Kweli mpenzi watu wanakariri kuwa laana mpka baba au mama akuvulie Nguo,.me naona ktk mahusiano/mapenzi mtu binafsi unaweza kuepuka laana kama unajielewa na Mungu akakupigania ukawa na Amani tuu...
 
Haya mapenzi yangekuwa kwenye waliii nisingeulaaa, ningeuacha ulale nikiamka umechacha niumwage kabisaaaa!!!!!
 
Umekosea kutoka na mkaka? Halafu unalalamikia wanaume.
Hahaha!!mkaka ni kiswahili tu cha kisasa jamani. Sio kwamba amenanisha mkaka kweli.
1456325445316.jpg
 
Kweli mpenzi watu wanakariri kuwa laana mpka baba au mama akuvulie Nguo,.me naona ktk mahusiano/mapenzi mtu binafsi unaweza kuepuka laana kama unajielewa na Mungu akakupigania ukawa na Amani tuu...
kama mimi hapa mtaani naona kuna manzi ananikubali vibayavibaya ila mimi sina mpango naye, yaani najisemea huyu binti nikae mbali naye sababu najua nitamuumiza tu lakini pia ile hulka ya kiume inanijia yaani namwangaliaga simpatii picha
 
Back
Top Bottom