The Donchop
JF-Expert Member
- Jan 10, 2014
- 294
- 378
Wana JF,
Sina raha kabisa. Nimejaribu kulala lakini imeshindikana. Vidonge vyangu vya usingizi vimeniishia kabisa.
Niliwahi kuleta mada juu ya mpenzi aliyeniacha ingawa muda wote ameniganda. Tunashinda nae, tunakula nae, tunasaidiana kwa kila kitu.
Wiki hii mwenzangu amebadilika tena. Ameninunia ghafla kisa nimemuuliza kipi kinamfanya aendelee kuwa nami wakati hanipendi. Hilo swali limeibua ugomvi mkubwa. Hataki hata kunisikia kisa nimeuliza hilo swali.
Wana JamiForum, naandika hapa pengine nitajisikia vema. Ila kiukweli, nimejisikia vibaya sana.
Mtu niliyesimama kidelete kipindi akiwa na shida, leo shida imeisha ananiona mkosi! Mtu niliyejinyima kuvaa kwaajili yake ili yeye apate nauli ya kwenda kutafuta maisha, leo hii nimekua chanzo cha yeye kufail maisha!
This is too much wanaume. Msipende kutuumiza namna hii. Ingawa tuna uwezo wa kuvumilia lakini kuna muda mnazidisha na mnapaswa kujua kuwa nasi ni banadamu kama nyinyi.
Mnashindwa kumwambia mtu kama mko kwa muda tu ili usolve matatizo yako mpaka mnatudanganya kuwa mnatupenda na tunawakabidhi mioyo yetu!
Mnashindwa kuthamini upendo wa mtu mpaka mtuumize mioyo yetu? Msitufanyie hivyo tafadhali. Hapa moyo wangu naona umebadilika. Kila mkaka namwona ni walewale. Kila ninapojaribu kusahau nashindwa. Chuki. hasira, huzuni ndivyo vilivojaa moyoni mwangu. Sababu ya mpuuzi mmoja tu.
Leo nalivua hili pendo la kihuni.
Samahanini wana JF, nimependa kuwashirikisha ili mjue ni jinsi gani tunavyoumia na wadada ambao hawajafikwa na hili wakae tayari.