Wanaume punguzeni kututesa, tunaumia jamani

Wanaume punguzeni kututesa, tunaumia jamani

Wana JF, sina raha kabisa. Nimejaribu kulala lakini imeshindikana. Vidonge vyangu vya usingizi vimeniishia kabisa.

Niliwahi kuleta mada juu ya mpenzi aliyeniacha ingawa muda wote ameniganda. Tunashinda nae, tunakula nae, tunasaidiana kwa kila kitu.

Wiki hii mwenzangu amebadilika tena. Ameninunia ghafla kisa nimemuuliza kipi kinamfanya aendelee kuwa nami wakati hanipendi. Hilo swali limeibua ugomvi mkubwa. Hataki hata kunisikia kisa nimeuliza hilo swali.
Wanajamii forum, naandika hapa pengine nitajisikia vema. Ila kiukweli, nimejisikia vibaya sana.

Mtu niliyesimama kidete kipindi akiwa na shida, leo shida imeisha ananiona mkosi!! Mtu niliyejinyima kuvaa kwaajili yake ili yeye apate nauli ya kwenda kutafuta maisha, leo hii nimekua chanzo cha yeye kufail maisha!

This is too much wanaume. Msipende kutuumiza namna hii. Ingawa tuna uwezo wa kuvumilia lakini kuna muda mnazidisha na mnapaswa kujua kuwa nasi ni banadamu kama nyinyi.

Mnashindwa kumwambia mtu kama mko kwa muda tu ili usolve matatizo yako mpaka mnatudanganya kuwa mnatupenda na tunawakabidhi mioyo yetu!

Mnashindwa kuthamini upendo wa mtu mpaka mtuumize mioyo yetu? Msitufanyie hivyo tafadhali. Hapa moyo wangu naona umebadilika. Kila mkaka namwona ni walewale. Kila ninapojaribu kusahau nashindwa. Chuki. hasira, huzuni ndivyo vilivojaa moyoni mwangu. Sababu ya mpuuzi mmoja tu.
Leo nalivua hili pendo la kihuni.

Samahanini wana jf, nimependa kuwashirikisha ili mjue ni jinsi gani tunavyoumia na wadada ambao hawajafikwa na hili wakae tayari.
Uliwezaje kuish na mtu ambaye hata ww unajua hakupendi halaf tena ww umuuliza wkt unajua hakupend ulitegemea akujibu mini?
 
Nimekuelewa Sana Sana ila Kuna mambo inapaswa akubali Tu kila siku uumie kila siku unalia till when??

Well my understanding ni kwamba kila break up INA utofauti wake isipokuwa tuko sawa kwa kusema we broke up.. Tofauti it depends two people wameichukuliaje .. Na muda pia waliokuwa pamoja, mangapi walifanyiana, nakadhalika . Kwa Mmoja inaweza kuwa easy na kwa mwingine ikawa hard to accept it .. So let's try to put ourselves in her shoes , halafu vile ambavyo tungependa tujibiwe basi nasi tutumie chance hii to do the same to her .. I do feel her pain ,for not accepted it the reality but the last thing she does not need is another stress from us.. We need to get easy on her so she can get pass this difficult time, she is going through right now . Remember tuko tofauti from different experience. Probably this it was her first love or second relationship..in this case huwezi kufananisha na MTU mwenye too much experiences ya more than 5 relationships ambazo zote zilivunjika na yuko normal.. What she needs now is to learn to accept it that its over with that man.. But it won't come easily, itachukua muda kwake . I wish angekuwa na rafiki WA kweli who can be with her without judging her , just to be there and praying with her and lean on her as her shoulders.. Dear I had a friend who went through the same break up kama huyu Dada .. Everybody who surrounded her judged her . Beside of other advice niliyowahi kummpa mojawapo ilikuwa ni kuchange number and it worked with her maana the guy abused her feelings .. Kila Siku ilikuwa ni kulia tuu na kukata tamaa ya maisha ... I wasn't there to judge her but I was there to be her best friend na kujaribu kufanya vitu ambavyo Mimi ningependa kufanyiwa na mwingine .. Well she survived Thank you Jesus now she is happily married with another awesome guy .. Na wale wote waliokuwa waki mjudge now kutwa kummsifia kwa kupata mume mwema.. ( ambaye si yule ex mchumba ) .. So tumtie moyo huyu Dada na kumuombea ili avuke salama kipindi hichi kigumu .. Thanks..
 
Binadam ni mtu sana anapozaliwa na hata kabla ya kukutana na binadam mwengine, ila baada ya kukutana na binadam mwenzake hubadilika na kuwa na roho mbaya zaid ya mnyama, pale anapotendewa mabaya huweka roho ya kisasa na hata anapomkosa mtu sahih wa kumlipiza kisas hulipa kwa yeyote ambaye hupita mbele yake na huo ndo mwanzo wa ubaya, kila vuno baya unaloliona limetokn na zao baya lililopandwa, sitashangaa akajitoke mwanaume nae akalalamika umemtenda..nadhan sasa umeanza kunielewa
 
Everything happens for a reason!! Baya na zuri kaumbiwa mwanadamu,, ishatokea move on!!
 
Pole sana dada..Ngoja nikupe ushuhuda wangu..Uenda utaambulia kitu

Niliondoka kwenda Iraq kutafuta kula..Huku nyuma nikawa nimemuacha mpnz wangu ambaye tulikuwa tumetimiza mwaka na nusu kwenye mahusiano yetu mpaka dakika hiyo...Na kwa kipindi chote cha mahusiano dem alikuwa ananisaidia sana..Mana yeye alianza kushika pesa mapema kabla yangu..

Kabla ya kuondoka nikaamua nimtambulishe home..Nikamtambulisha kwa Sista na mdogo wangu wa kiume..Lengo,nia na dhumuni la kumtambulisha ilikuwa nataka ndugu wamfahamu ili wanisaidie kumtupia macho kidogo..

Kumbe kipindi mi niko kule sista pamoja na dogorasi walitokea kupatana sana na yule binti..Wakawa wanashirikiana kwenye matukio mengi..Kitu kilichopelekea hata ndugu wengi kumfahamu..

Basi baada ya miaka minne ya kozi yangu ya kukwepa mabomu nikarudi home..Nilivyorudi tukaendelea na mahusiano kama kawa..Ila kipindi naendelea nae kuna kamchepuko kalikuwa kanadoea penzi la huyo dada..Sijui hata nn kilitokea..Kidogo kidogo nikaanza kumchukia mpnz wangu..Visa vikawa haviishi..Mapenzi yakahamia kwa mchepuko..

Kifupi mwisho wa siku nilimwacha mpnz wangu nikaendelea na hili balaa jingine..Binti alilia sana aisee..Sista na Dogorasi walikuwa wakinishauri lakini sikushika hata moja..Mwisho wa siku yule binti akawaambia mwacheni tu aendelee na maisha yake..
Huo ndo ukawa mwisho wa mahusiano yetu..Ila dada wa watu hakukata mawasiliano na sista wala dogorasi..Na bado kwenye matukio mbalimbali ya kifamilia kama harusi,misiba alikuwa anakuja kama kawa kitu kilichopelekea kuonana nae mara kwa mara..
Basi miaka ikazidi kusonga..Ila Kilichokuwa kinanishangaza kila tukikutana nae namuona anazidi kupendeza tu..Anabadilisha magari deile..Nikajua labda ananifanyia maigizo..Ikabidi nifanye uchunguzi..Ndo kuja kugundua kuwa mambo yake ni super ile mbaya..Nikabaki najicheka tu
Now kuna biashara wanafanya na sista..Mambo yanawaendea poa..Uwa tukikaa wananitania sana..Wananiita EP(enemy of progress)..Ananiambia Kaboom uenda ningeendelea na ww nisingefika hapa nilipo..

Ukirudi kwa huyu niliyenae ni balaaaa..Ndoa ni chungu...shubiri naiona asali..Unatamani hata Yesu arudi kesho....

Mawazo chanya:Ukiona unamuomba Mungu gari na hakupatii,Basi jua pengine anakuepusha na ajari..Usilazimishe vitu
Nimependa ushuhuda wako
 
maumivu ya hii kitu yasikie tu kwa wengine... Nishawahi kuwa mlevi mpaka nilikuwa nikishindwa hata kubadili nguo. Kila niliyokuwa nikivaa basi nilihakikisha wiki nzima Ipo mwilini... Siku Alipokuja kuzaliwa Mwanangu Yaseer ndio Siku ya Mwisho niliyoiacha Pombe.

Licha ya kuumizwa na Kutendwa na mwanamke niliyezaa nae lakini Daima mwanangu alinifanya nijione nimezaliwa Upya na Majukumu mengine.

Usilie kwa sababu ya Mtu Asiyejali wala Kuuthamini Moyo Wako.

Mtu ambaye haumizwi na Kilio chako..

Bali umia na Kunyenyekea Mbele ya Mungu kwa Kuwa ndio mtu pekee mwenye huruma na Upendo kwa Viumbe Vyake Wote bila Kujali Utofauti wa Kipato, kimaisha na Mengineyo.

Usilie Ukajiona Huna thamani bali simama na Kufuta machozi Huku Ukijiona Wewe ni Shujaa kwa Kuwa wapo wanawake wanaoteseka na kuteswa kuliko wewe lakini kamwe hawalii sababu ya kutendwa na Binadamu Wenzao bali hupiga goti na Kusujudu sababu ya Kuhitaji Amani na Uhuru kutoka kwa Mungu Baba..
 
Pole sister angu ila usipende kutumia vidonge vya usingizi popote pale cuz ni aina ya dawa za kulevya na inamadhara makubwa baadae especially addictions na insomnia...

Kuhusu huyo jamaa just leave him...your king is out there..u wil find him usife moyo althought i know how it hurts..be a strong woman my sstr and alwayz be blessed..
 
hizi tungo tata wanaume tunalalamika wanawake mmezidi nanyi pia mnalalamika WANAUME TUKIPENDA HATUPANGUI hata utoe mzigo mara mia kabla ya ndoa kama umependa hatuachi tatizo lipo kwenu huenda kuna kitu umemfanyia maana kwa maelezo yako jamaa alikuwa karibu nawe ila kuna kitu zaidi ya hapo ALWAYS MEN DONT LIE LIKE GIRLS
 
MMU raha sana maswali na majibu vipo hapa hapa, matatizo na ufumbuzi tunavyo humuhumu.
 
Wana JF,

Sina raha kabisa. Nimejaribu kulala lakini imeshindikana. Vidonge vyangu vya usingizi vimeniishia kabisa.

Niliwahi kuleta mada juu ya mpenzi aliyeniacha ingawa muda wote ameniganda. Tunashinda nae, tunakula nae, tunasaidiana kwa kila kitu.

Wiki hii mwenzangu amebadilika tena. Ameninunia ghafla kisa nimemuuliza kipi kinamfanya aendelee kuwa nami wakati hanipendi. Hilo swali limeibua ugomvi mkubwa. Hataki hata kunisikia kisa nimeuliza hilo swali.
Wana JamiForum, naandika hapa pengine nitajisikia vema. Ila kiukweli, nimejisikia vibaya sana.

Mtu niliyesimama kidelete kipindi akiwa na shida, leo shida imeisha ananiona mkosi! Mtu niliyejinyima kuvaa kwaajili yake ili yeye apate nauli ya kwenda kutafuta maisha, leo hii nimekua chanzo cha yeye kufail maisha!

This is too much wanaume. Msipende kutuumiza namna hii. Ingawa tuna uwezo wa kuvumilia lakini kuna muda mnazidisha na mnapaswa kujua kuwa nasi ni banadamu kama nyinyi.

Mnashindwa kumwambia mtu kama mko kwa muda tu ili usolve matatizo yako mpaka mnatudanganya kuwa mnatupenda na tunawakabidhi mioyo yetu!

Mnashindwa kuthamini upendo wa mtu mpaka mtuumize mioyo yetu? Msitufanyie hivyo tafadhali. Hapa moyo wangu naona umebadilika. Kila mkaka namwona ni walewale. Kila ninapojaribu kusahau nashindwa. Chuki. hasira, huzuni ndivyo vilivojaa moyoni mwangu. Sababu ya mpuuzi mmoja tu.
Leo nalivua hili pendo la kihuni.

Samahanini wana JF, nimependa kuwashirikisha ili mjue ni jinsi gani tunavyoumia na wadada ambao hawajafikwa na hili wakae tayari.
Achana kabisa na hayo mavidonge ya usingizi yatakuharibu.
 
Hahah mapenzi hayanaga guarantee. Ww umeyapa guarantee yamekutia hasara.nxt time ujifunze kuwa mapenz yana nafas yake lakin syo kila kitu.fanya mambo yako hayo mambo yapo tu na yatakuwa upande wako at the right time.
 
mkuu kwani swala kumkabidhi moyo mtu katika nyanja ya mahusiano/mapenzi we unalielewaje?

Kwenye nyanya hiyo hakuna kukabidhi moyo. Kwa wanawake cha kukabidhi ni huduma ya papachu tu. Ukikabishi moyo haukawii kuharibiwa.
 
Demu mmoja aliamsha guts zake na kujitongizesha kwa mshikaji, mshikaji nae akasema ngoja nijilie tu hivi vyakula visivyo na mlaji, baada ya wiki demu akamuuliza mshikaji eti hivi baby umenipendea nini??

Sasa niambie kama ni wewe umeulizwa hilo swali utajibu nini?
 
Pole sana mrembo ila na nyie wadada mcpende kuforce lv muda mwngne mjtajd kusoma alama za nyakat

Em jarbu kujiwekea vgezo ambavyo vtakufanya ugundue km mwenzi mtarajiwa amerdhka naww au yuko as party time??


Na nyie wanaume mcpende kupenda mdada et ksa ana'maisha mazur

Et ksa unasoma unahtaj hfadh kwa muda ila ukpata kaz unaanza kutafuta type yako
 
Back
Top Bottom