Wanaume punguzeni kututesa, tunaumia jamani

Wanaume punguzeni kututesa, tunaumia jamani

Pole sana dada..Ngoja nikupe ushuhuda wangu..Uenda utaambulia kitu

Niliondoka kwenda Iraq kutafuta kula..Huku nyuma nikawa nimemuacha mpnz wangu ambaye tulikuwa tumetimiza mwaka na nusu kwenye mahusiano yetu mpaka dakika hiyo...Na kwa kipindi chote cha mahusiano dem alikuwa ananisaidia sana..Mana yeye alianza kushika pesa mapema kabla yangu..

Kabla ya kuondoka nikaamua nimtambulishe home..Nikamtambulisha kwa Sista na mdogo wangu wa kiume..Lengo,nia na dhumuni la kumtambulisha ilikuwa nataka ndugu wamfahamu ili wanisaidie kumtupia macho kidogo..

Kumbe kipindi mi niko kule sista pamoja na dogorasi walitokea kupatana sana na yule binti..Wakawa wanashirikiana kwenye matukio mengi..Kitu kilichopelekea hata ndugu wengi kumfahamu..

Basi baada ya miaka minne ya kozi yangu ya kukwepa mabomu nikarudi home..Nilivyorudi tukaendelea na mahusiano kama kawa..Ila kipindi naendelea nae kuna kamchepuko kalikuwa kanadoea penzi la huyo dada..Sijui hata nn kilitokea..Kidogo kidogo nikaanza kumchukia mpnz wangu..Visa vikawa haviishi..Mapenzi yakahamia kwa mchepuko..

Kifupi mwisho wa siku nilimwacha mpnz wangu nikaendelea na hili balaa jingine..Binti alilia sana aisee..Sista na Dogorasi walikuwa wakinishauri lakini sikushika hata moja..Mwisho wa siku yule binti akawaambia mwacheni tu aendelee na maisha yake..
Huo ndo ukawa mwisho wa mahusiano yetu..Ila dada wa watu hakukata mawasiliano na sista wala dogorasi..Na bado kwenye matukio mbalimbali ya kifamilia kama harusi,misiba alikuwa anakuja kama kawa kitu kilichopelekea kuonana nae mara kwa mara..
Basi miaka ikazidi kusonga..Ila Kilichokuwa kinanishangaza kila tukikutana nae namuona anazidi kupendeza tu..Anabadilisha magari deile..Nikajua labda ananifanyia maigizo..Ikabidi nifanye uchunguzi..Ndo kuja kugundua kuwa mambo yake ni super ile mbaya..Nikabaki najicheka tu
Now kuna biashara wanafanya na sista..Mambo yanawaendea poa..Uwa tukikaa wananitania sana..Wananiita EP(enemy of progress)..Ananiambia Kaboom uenda ningeendelea na ww nisingefika hapa nilipo..

Ukirudi kwa huyu niliyenae ni balaaaa..Ndoa ni chungu...shubiri naiona asali..Unatamani hata Yesu arudi kesho....

Mawazo chanya:Ukiona unamuomba Mungu gari na hakupatii,Basi jua pengine anakuepusha na ajari..Usilazimishe vitu
Sitaki kuamini majicho yangu, naomba hii iwe tu ni story au niwe ninaota tu kwakweli.
 
Duh! Pole sana. Its a one step back but its not a total failure. You can collect your self and move on. There are good looking nice young men looking for some one like you out there. Some one else will see you and value you for who you are... Move on plz...
 
Punguza kujikabidhi mzima mzima kwa mtu uliyekutana naye ukubwani.

Halafu moyo ni kitu cha kulinda sana kuliko chochote, iweje umkabidhi mtu kiiivyo
 
Mie tena wa kukupelekesha!! Na hiyo ni iraq ya wapi uliyokwenda mume wangu? Hivi mbona hivi jamani? Haya njoo tuyamalize mpenzi.
Teh teh..Nilienda kusomea kujilipua..Sasa ww endelea kuzurula tu..Dawa wako ipo jikoni
 
Back
Top Bottom