Wanaume punguzeni kututesa, tunaumia jamani

Hapo ndio unakomaa sista, hlf usisahau kwamba siku huwa hazigandi(hata kwenye ndoa kuna milima na mabonde) kwahiyo hata ukiolewa kukwaruzana kwa hapa na pale kupo tuu, jambo la msingi ni kujitambua, punguza hasira zitakutesa ww mwenyewe, hasira hasara
 
Wana JF,

Sina raha kabisa. Nimejaribu kulala lakini imeshindikana. Vidonge vyangu vya usingizi vimeniishia kabisa.

Niliwahi kuleta mada juu ya mpenzi aliyeniacha ingawa muda wote ameniganda. Tunashinda nae, tunakula nae, tunasaidiana kwa kila kitu.

Wiki hii mwenzangu amebadilika tena. Ameninunia ghafla kisa nimemuuliza kipi kinamfanya aendelee kuwa nami wakati hanipendi. Hilo swali limeibua ugomvi mkubwa. Hataki hata kunisikia kisa nimeuliza hilo swali.
Wana JamiForum, naandika hapa pengine nitajisikia vema. Ila kiukweli, nimejisikia vibaya sana.

Mtu niliyesimama kidelete kipindi akiwa na shida, leo shida imeisha ananiona mkosi! Mtu niliyejinyima kuvaa kwaajili yake ili yeye apate nauli ya kwenda kutafuta maisha, leo hii nimekua chanzo cha yeye kufail maisha!

This is too much wanaume. Msipende kutuumiza namna hii. Ingawa tuna uwezo wa kuvumilia lakini kuna muda mnazidisha na mnapaswa kujua kuwa nasi ni banadamu kama nyinyi.

Mnashindwa kumwambia mtu kama mko kwa muda tu ili usolve matatizo yako mpaka mnatudanganya kuwa mnatupenda na tunawakabidhi mioyo yetu!

Mnashindwa kuthamini upendo wa mtu mpaka mtuumize mioyo yetu? Msitufanyie hivyo tafadhali. Hapa moyo wangu naona umebadilika. Kila mkaka namwona ni walewale. Kila ninapojaribu kusahau nashindwa. Chuki. hasira, huzuni ndivyo vilivojaa moyoni mwangu. Sababu ya mpuuzi mmoja tu.
Leo nalivua hili pendo la kihuni.

Samahanini wana JF, nimependa kuwashirikisha ili mjue ni jinsi gani tunavyoumia na wadada ambao hawajafikwa na hili wakae tayari.
Wanawake ni wahanga sn ktk mahusiano ila kitu kimoja mnashindwa kujielewa na kujitambua kwamba una maamuzi yako na kuna haki zako zinalindwa .sometyms inatokea unaogopa kumwacha mwanaume kwmba anaweza kukudhuru au akakuaribia au kukuabiisha mbele y watu futa hapo piga nyama chini.bora kufa mara 1 kuliko kufa mara 1000 yaan we kila cku sononeko u a dying slowly very painful
 
even marriage is not love it is ----------Marriage means the voluntary union of a man and a woman, intended to last for their joint lives.
 
Mpige limbwata tu...huko kwenye vidonge vya usingizi unapoteza muda...
 
Wana JF,

Sina raha kabisa. Nimejaribu kulala lakini imeshindikana. Vidonge vyangu vya usingizi vimeniishia kabisa.

Niliwahi kuleta mada juu ya mpenzi aliyeniacha ingawa muda wote ameniganda. Tunashinda nae, tunakula nae, tunasaidiana kwa kila kitu.

Wiki hii mwenzangu amebadilika tena. Ameninunia ghafla kisa nimemuuliza kipi kinamfanya aendelee kuwa nami wakati hanipendi. Hilo swali limeibua ugomvi mkubwa. Hataki hata kunisikia kisa nimeuliza hilo swali.
Wana JamiForum, naandika hapa pengine nitajisikia vema. Ila kiukweli, nimejisikia vibaya sana.

Mtu niliyesimama kidelete kipindi akiwa na shida, leo shida imeisha ananiona mkosi! Mtu niliyejinyima kuvaa kwaajili yake ili yeye apate nauli ya kwenda kutafuta maisha, leo hii nimekua chanzo cha yeye kufail maisha!

This is too much wanaume. Msipende kutuumiza namna hii. Ingawa tuna uwezo wa kuvumilia lakini kuna muda mnazidisha na mnapaswa kujua kuwa nasi ni banadamu kama nyinyi.

Mnashindwa kumwambia mtu kama mko kwa muda tu ili usolve matatizo yako mpaka mnatudanganya kuwa mnatupenda na tunawakabidhi mioyo yetu!

Mnashindwa kuthamini upendo wa mtu mpaka mtuumize mioyo yetu? Msitufanyie hivyo tafadhali. Hapa moyo wangu naona umebadilika. Kila mkaka namwona ni walewale. Kila ninapojaribu kusahau nashindwa. Chuki. hasira, huzuni ndivyo vilivojaa moyoni mwangu. Sababu ya mpuuzi mmoja tu.
Leo nalivua hili pendo la kihuni.

Samahanini wana JF, nimependa kuwashirikisha ili mjue ni jinsi gani tunavyoumia na wadada ambao hawajafikwa na hili wakae tayari.
Huwezi kubadilisha nyekundu kua njano.mnaingia kwenye mapenzi bila muongozo wa kweli kutoka kwa huyo mwanaume,unampenda na kuanza kusex nae na hajakuoa,mmekutana ukubwani,mna hulka na malezi tofauti lakini unataka aendane na fikra zako.ni ngumu sana,msiwe mnalalamika ilihali ni matokeo ya dhambi,kama hukumgawia mpaka ukafunga nae ndoa na akaja kubadilika hapo ukija hapa kulalamika hata mimi ntakuelewa,sasa mmekutana JIMWAGE MTU NA MTU GUEST HOUSE kabla hata ya ndoa,mnavyoachana asubuhi ndivyo mtakavyoachana siku zijazo,tatizo wanawake mna mbinu mbovu za kutafuta ndoa,masuluale mepesi ya kuonyesha viungo vyenu,kujibebesha mimba bila matarajio sahihi,na siku hz mnahonga kijanjajanja pale unapojua boy wako ana shida unajifanya kumsaidia kumbe unalenga mbeleni asije kukukimbia kutokana na misaada yako,you're wrong.acheni kulalamika pamoja na kwamba ninajua vijana wako na shida zao lakini ninyi wanawake wa town mmekua hamfai kwa tabia zenu.usichukie coz nimeongea yaliyopo ndani yenu kwa karne hii
 
Pole sista ila biblia unasema Linda sana moyo wako,mana ndio chemichemi ya uzima itokapo...usimpe mwanadamu moyo wako tena Hata siku moja atakuua.mpe Mungu peke yake.pole jipe moyo this too shall pass
True that.
 
Tatizo mnaingiza kichwa na miguu kwa mtu hata hamjaoana wala hajaenda kwenu. Unampenda mtu kama ulizaliwa nae?

Lala ukiamka yameisha, time is the best healer, mwanaume kama hataki mwache aende zake, kwani ulizaliwa nae? Si umemkuta ukubwani tu huyo? Sasa tatizo nn, kwani lazima uolewe kwenye matatizo ndio ijulikane unakipimo cha uvumilivu?

Alafu acha zako unajuta kupoteza nauli ulizo msaidia wakati anatafuta maisha? Ha ha nauli kitu gani bana, hata kama ulitoa kila kitu, watu wanapoteza billions ya pesa na wana sahau wanaanza upya, watu wanalala anaamka kaunguliwa nyumba ndani mke na watoto wamefia huko, na maisha yanaendelea, wewe unalilia nauli? Sasa komalia nauli ufe na machungu ya mapenzi "eti unapenda" walipendana Adam na hawa mwisho wakatengana wa kwanza utakuwa wewe?

Kwani ukimuacha huyo mwanaume hupati mwingine? Utasikia mwanaume wote ni sawa, sawa? hao walio katika ndoa na wanafuraha wao wanaishi na wanawake wenzao? Jibu ni la!

Anyway pole nimeandika kama maudhi hivi ila jua cha muhimu katika maisha ni uhai na uzima wa viungo tu, vingine vyote utafutwa na kupatikana.

Mutangulize Mungu, kuwa mtulivu, usiwe na papara ya ndoa wala kulazimisha ndoa, tafta maisha na acha mwanaume aingie yeye wewe uwe kama half half hata kama umekufa na kuoza.
Umemaliza yote na makavu live juu.. khaa
 
Sasa inakuuma nini wakati unajua hakupendi? Alikua hajanuna ila ulipomuuliza hilo swali akaanza kununa. Huoni kuna tofauti kati ya wakati kabla hujauliza na baada ya kuuliza
 
Tatizo mnaingiza kichwa na miguu kwa mtu hata hamjaoana wala hajaenda kwenu. Unampenda mtu kama ulizaliwa nae?

Lala ukiamka yameisha, time is the best healer, mwanaume kama hataki mwache aende zake, kwani ulizaliwa nae? Si umemkuta ukubwani tu huyo? Sasa tatizo nn, kwani lazima uolewe kwenye matatizo ndio ijulikane unakipimo cha uvumilivu?

Alafu acha zako unajuta kupoteza nauli ulizo msaidia wakati anatafuta maisha? Ha ha nauli kitu gani bana, hata kama ulitoa kila kitu, watu wanapoteza billions ya pesa na wana sahau wanaanza upya, watu wanalala anaamka kaunguliwa nyumba ndani mke na watoto wamefia huko, na maisha yanaendelea, wewe unalilia nauli? Sasa komalia nauli ufe na machungu ya mapenzi "eti unapenda" walipendana Adam na hawa mwisho wakatengana wa kwanza utakuwa wewe?

Kwani ukimuacha huyo mwanaume hupati mwingine? Utasikia mwanaume wote ni sawa, sawa? hao walio katika ndoa na wanafuraha wao wanaishi na wanawake wenzao? Jibu ni la!

Anyway pole nimeandika kama maudhi hivi ila jua cha muhimu katika maisha ni uhai na uzima wa viungo tu, vingine vyote utafutwa na kupatikana.

Mutangulize Mungu, kuwa mtulivu, usiwe na papara ya ndoa wala kulazimisha ndoa, tafta maisha na acha mwanaume aingie yeye wewe uwe kama half half hata kama umekufa na kuoza.
You fail to copy $ paste
 
Jinsi unavyolalamika wewe hata na sisi wanaume huwa tunalalamika vilevile, kila mtu humfika ya tofauti na mwingine.
Ila pole pia kwa majanga uliyokutana nayo, hizo ndo changamoto katika mahusiano.
 
Back
Top Bottom