Wanaume ni kama mbwa........................ wanapojihami! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaume ni kama mbwa........................ wanapojihami!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Jan 7, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kama umeshawahi kufunga mbwa au kumchunguza, utagundua kwamba, mbwa dume ana kawaida ya kutoa sauti yenye kuonesha kuumia au kuhuzunika au kuomba hasa anapokutana na mbwa mwingine ambaye anajua wazi kuwa ana nguvu kuliko yeye. Lakini mbwa huyo huyo ataunguruma kwa sauti ya chini inayotoka ndani, kama vile amekasirika sana au anajitambulisha kwamba anajimudu pale anapokutana na mbwa ambaye anajua anaweza kupambana naye. Ukiwakagua mbwa utabaini sifa hiyo ya kuunguruma kwa namna tofauti kutoka mazingira flani hadi mengine. Pale ambapo anaona atashinda pambano, huwa ana mlio mmoja na pale anapoona atashindwa mlio huwa mwingine.Lakini je, hali kama hii iko kwa mbwa tu? Hapana, watafiti wanasema binadamu naye yuko hivyohivyo. Wanasema, linapokuja suala la namna tunavyojibu hali zenye kututisha, hatuna tofauti na mbwa.

  Mbwa anashusha sauti na kuunguruma kutoka kooni kama anaamini kwamba, mbwa anayemkabili hamwezi. Mwanaume naye huwa na kawaida ya kushusha sauti yake na kuzungumza kama vile sauti yake ni mali sana, anapokuwa akizungumza na mtu ambaye anaamini anammudu kimwili. Kama ilivyo kwa mbwa, hata wanaume, hali hii hutokea bila wahusika kujua. Najua hata wewe mwanaume unayesoma hapa unaweza kutilia mashaka jambo hili, lakini kama ukianza kujiuliza sasa hivi ndipo ambapo utagundua kwamba, kwa wale watu ambao unaona kabisa unawamudu au ambao unaamini hawatishii usalama wako kimwili, utazungumza nao kwa sauti ya kutokea kooni au ndani, yenye kuonesha kujiamini.

  Kwenye akili ya mwanaume tafsiri ya sauti hufanyika bila wenyewe kujua. Mwanaume anapomsikia mwenzake akizungumza kwa sauti iliyotulia na inayotoka ndani, huhisi kwamba, mtu huyo anayo nafasi kubwa zaidi kuliko yeye. Mwanaume humchukulia mwanaume mwenzao wa namna hiyo kama aliye na nafasi kubwa ya kumudu au kudhibiti. Kama umewahi kuchunguza utakubaliana name kwamba, wanaume huwa na kawaida ya kupandisha sauti na kuwa na sauti yenye mawimbi makali, pale wanapozungumza na mtu ambaye wanajua anawazidi hasa kimwili na kinguvu. Kama ni mtu ambaye wanaamini kwamba, wanamzidi, sauti zao huwa ni za kushiba na zinazotoka ndani.

  Hii ina maana kwamba, bila wanaume wenyewe kujua, wanaposikia sauti iliyotulia, yaani inayotoka kwa wanaume wenzao huhisi kwamba, hao wenzao wanawamudu. Kumbuka hapa sizungumzii kupayuka au kuzungumza kwa kelele, bali nazungumzia utoaji wa sauti. Nikisema sauti kutoka kooni nina maana ya sauti nzito na yenye aina ya mamlaka (Vijana wa siku hizi huita Ki-besi) Lakini kwa sehemu kubwa, mamlaka au kummmudu mwanaume mwingine inapimwa zaidi kimwili kuliko madaraka au sifa nyingine. Hii ikiwa na maana kwamba, pale ambapo mwanaume anahisi kwamba, kimwili anamzidi au anaweza kumdhibiti mwingine, ndipo ambapo sauti yake huwa ni ile ya kutokea kooni. Haifahamiki ni kwa nini hasa wanaume hujikuta bila hiyari yao wakiwa na mabadiliko hayo ya sauti pale wanapokabiliana na wanaume wenzao, ambao ama wanajua kuwa wanawamudu au hawawamudu. Lakini wataalamu wanadhani, hali hiyo inatokana na maumbile ya wanaume kutaka kuoneshana tofauti zao. Bila shaka umeshawahi kuona hata kwenye sinema. Wale waigizaji ambao wanaamini kwamba, wanaweza kuwazidi nguvu adui zao, wanapozungumza nao, hutoa sauti zao kutokea kooni. Kuigiza kwa namna hii kunatokana na nadharia hii, kwamba, mwanaume mwenye nguvu hatoi sauti kali.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  ngoja nitoke nje nikamtafute mwanamme mnyonge, nione kibesi kitakuwaje.
   
 3. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Kongosho hata akiwa mnyonge uwepo wako utamfanya awe na kibesi
  Mkuu Mtambuzi nimeupata ujumbe katika uzi wako huu
  Hii yote ni katika kuonyesha kuwa hata mbele ya yule ambaye unahisi kuwa ni mbabe kuliko wewe lazima na wew eujionyeshe kuwa una sauti
  Na huwezi kuwa mnyonge hata mbele ya mwenye sauti maana dhima nzima ya uanaume wako inatoweka
  Hujawahi kuona mwanaume mnyonge ila mbele ya wenzake nae anajifanya mbabe
  Hii ni katika kuonyesha kuwa na yeye ana sauti japo mbele ya wababe sauti yake inaweza isisikike
   
 4. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ntarudi baadae kumalizia kusoma...
   
 5. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Kama ulikuw ahujamaliza kusoma haikuwa na maana ya kuweka comment yako sasa
  Ungemaliza kusoma na ktoa mawazo yako
  Au nia yako ni kuongeza post zako
   
 6. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #6
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Unajua hata mimi zamani nilikuwa nawasikia wenzangu wakisema "Usinishushie kibesi" lakini sikujua ina maana gani, lakini sasa nimeamini kama ulivyosema kwamba mtu anahisi mwenzie anamletea dharau kutokana na umbo lake (kwa wanaume lakini) ni lazima atajikakamua kujionesha kama anamudu na anauwezo wa kudhibiti, hebu jariibu kuwangalia wasimamizi wa kazi maofisini wenye miiili nyonde nyonde wanapo-react pale wanapotoa maelekezo kwa walio chini yao hasa kama miili ya hao walio chini yao imeshiba kwa siha nzuri.......... ni dhahiri hapo sauti itakuwa na mamlaka makubwa na yenye kujiamini, lakini mtu huyo akiitwa na mkubwa wake na kuulizwa juu ya jambo fulani, ni dhahiri sauti itabadilika na kuwa ya chini na yenye kutii..............
   
 7. T

  Tall JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Hata, mimi si kama mbwa.
   
 8. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #8
  Jan 7, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  mimi kama simba, mbwa kitu gani bana!!
   
 9. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #9
  Jan 7, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Broda, mbona si ndefu kihivo?

  Mkuu Mtambuzi!
  Umenifanya nianze kuwapima jamaa na marafiki zangu wote wanizungukao, ili kujua ni wangapi ninakuwa na kibesi kwao, na wangapi nawagwaya!
  Nadhani hii hali ni very hormonal controlled, na inaendeshwa na CNS, hasa baada ya macho kupeleka taarifa kwa ubongo.

  Mkuu, naamini utakubali kuwa kuna kundi la 3 la aina ya watu unaokutana nao, nao ni wale ambao unahisi mnafanana kwa namna zote, iwe nguvu au uwezo mwingineo...je kwa hapa sauti itakuwa ya namna gani?:lol:
   
 10. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #10
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Watu warefu kama wewe mara nyingi huwa ni wembamba, na hawa ndio ambao hujishusha na kunyenyekea wanapokumbana na wanaume wenzao wenye miili iliyoshiba................ wanakuwa hawana mamlaka kabisa
   
 11. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #11
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Yeah kabisa
  Na kitu kimoja ni kuwa popote pale watakapokuwa wanaume wanaongea au kuna kamjadala akiwepo mnyonge miongoni mwao ni lazima atajitahidi kutoonyesha unyonge wake na kuwa na sauti miongoni mwa wenzake
  Si kwamba anataka aonekane ila ni kwamba asije akaonekana ni mnyonge na hana sauti
  Poppote pale atakapokuwa akiwa na mwili mdogo au akiwa mnyonge ni lazima ajikakamue kuonyesha kuwa yeye ni mbabe
  Ni sawa sana kwa maeneo ya kazi wale ambao wana miili midogo au sio wababe miongoni mwa wenzake anaofanya nao kazi na akiwa ndie boss hapo ni balaa . Kwa wenzake ambao wako chini ni lazima awe na bass kubwa na sauti yenye mamlaka kuonyesha kuw ana yeye yupo
  Ila naamini hii si kwa wanawake maana huwezi wewe ukaenda kuonyesha mamlaka yako na ubabe wako kwa mkeo
  Sana sana utaonekana huna busara
   
 12. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #12
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kwa kawaida huwa tunapenda kujilinganisha, na mara nyingi tunajipima kwa kuangalia uwezo wetu kimamlaka na kudhibiti, na ndio maana ukaibuka msemo wa mafahali wawili hawakai zizi moja.......... unadhani ni kwa nini.
  Ni kwa sababu kama kimamlaka kuna kupingana kati ya wanaume wawili katika kundi, basi ni lazima mmoja ajitoe, au akubali kuwa chini ya mwingine..........
   
 13. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #13
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280


  Na kwa hapo hakuna ambaye yuko tayari kukubali kuwa chini ya mwenzake au kuonyesha unyonge wake
  Kwa maana ukikubali hayo ina maana umekubali kuwa mnyonge na heshima ya uanaume wako inapungua
  Huwa tunapenda sana kuficha madhaifu yetu haswa mbele ya wanaume wenzetu hata kama unajulikana kabisa kuwa una udhaifu fulani ila mbele ya wanaume wenzio lazima ufiche hayona uonyeshe kuwa wewe ni mwanaume kwa njia yoyote ile
   
 14. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #14
  Jan 7, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280
  asante kwa darasa!
   
 15. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #15
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe, na ndio maana tunashuhudia visa na mikasa mingi pale wanaume wanapotaka kuoneshana ubabe, hususan pale wanapomuwania mwanamke, hii ipo mitaani tunamoishi, mashuleni, vyuoni na hata makazini, pale anapojitokeza mwanamke, katika himaya ya wanaume, ni lazima kutakuwa na kuonesha na ubabe hata ule wa kichini chini........... na hii inatokana na ile nadharia kwamba wanawake hupenda wanaume wababe............. ( hili bado nalifanyia utafiti, nitakuja kuweka mada hiyo hapa ikikamilika)
   
 16. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #16
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kuna kaukweli fulani
  Ila sio ubabe wa kwenda kupigana bar au kupiga wanawake
  Ni ule ubabe kuwa mwanaume anaweza kusimamia maamuzi yake na haogopi mtu yoyote
  Na mbele ya wanaume wenzake anaweza kusimama na kutetea msimamo wake alio nao bila kujali unamuumiza nani
   
 17. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #17
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  nakusalimu tu, naona kama umenisema mimi, lakini kwa wema sio mabaya.
   
 18. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #18
  Jan 7, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  hiyo title ya thread imewafurahisha watu humu ...lol
   
 19. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #19
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mkuu karibu Kahawa hapa kwenye kibaraza cha Kahawa Kwa Msisisri Kindondoni. leo nitashinda hapa kutwa nzima......................
   
 20. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #20
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Lakini haijavuruga amani humu jamvini naamini.................. Habari za siku mkuu!
   
Loading...