Wanaume 'msio na pesa' hapa tu ndo mnapokosea

Wanaume 'msio na pesa' hapa tu ndo mnapokosea

Upendo ndo wa muhimu, pesa zinatafutwa tu na sio adimu kama upendo. Umuache mtu anakupenda kisa pochi?
Yaani wanawake mngekuwa hivyo..halafu mkaondoa manywele ya marehemu na mikatani kichwani...mkabaki na nywele zenu asilia...mkabaki na ngozi yenu asilia...sisi wanaume tungeiona dunia nusu pepo.
 
<<< ina TV ndaniiii ?????? >>ukisikia hivyo mdada sepaaaa hakuna hela hapo>>somo limeniingia kijana mm>>
 
Nimekuelewa. Niliwahi kuwa na mtu wa hivyo, nilikuwa nafanya ninachoweza vingine namuachia. Yanini kuitesa nafsi?
 
Kama nimemwelewa mtoa mada vile!

Kwenye chemistry kuna theory moja ya heat inasema unapochanganya kitu cha moto na cha baridi pamoja, kile cha moto kitapoteza joto lake kwa kiwango sawa na kile cha baridi kitakavyogain joto

When two or more objects at different temperatures are brought together in an isolated environment, they eventually reach the same temperature by the process of heat exchange. That is, warmer materials transfer heat to colder materials until their temperatures are the same.

Ndo maana unakuta watu wanasema chemistry haijakubali, ina maana mwenye joto kagoma kugawa joto lake, au mwenye baridi kagoma kupokea joto.
Hii ni physics mkuu labda kama ulisoma physics with chemistry enzi za Mungai (RIP)
 
Stashed-Presents-Behind-The-Meme-Crying-MJ-1050x654.jpg
Mbona unalia [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]mweeeh
 
Hii ni physics mkuu labda kama ulisoma physics with chemistry enzi za Mungai (RIP)

Sikusoma kipindi cha Mungai, labda tu nimechanganya madesa.

Okay, mi kumbukumbu zangu za topic ya Heat ni Chemistry Form 3.

Asante kwa kunisahihisha mkuu.
 
Wanaume wengi, hasa wa JF wanalalamika sana kuwa wanawake tunataka wanaume 'wenye pesa' au waliofanikiwa tu. Pia kuonesha hii (kukubalika bila kuwa na pesa au kuhonga) ndio concern kwa wanaume wengi ni pale nyimbo nyingi za Kitanzania message ni hiyo hiyo, mfano: "Japo sina kitu,......", "Ukawaacha wenye pesa......" Tukilala njaa......"

Nikirudi kwenye mada, Kukosa pesa sio tatizo!!!!!

Mimi ni mtu ninayependa finer things in life. Napenda vitu vizuri na sisubirii mtu anipe. Kwenye kujipa raha sinaga subira wala uoga, najigharamia. Halafu kingine ni kuwa I am generous, sio mchoyo kabisa. Kuwa na mimi na utaexperience kila ninachoexperience. Ukiwa mtu wangu automatically ntakuinclude nikienda shopping, movies, nikipanga safari ya bata nakujumuisha na kila kitu.

Sasa unakuta uko kwenye mahusiano na mtu, akishajua jinsi unaendesha maisha yako anataka kujitutumua kukuimpress. Anataka kukupa huduma zile zile unazojipa mwenyewe au hata zaidi kwa pesa ambazo hana ili tu umuone bora zaidi. Inatia huruma!

Unakuta unamuinvite mtu out anataka kulipa wakati unajua kabisa hawezi kuafford, kwanini mnajitesa wanaume. Mtu ukishapendwa usiwe na hofu, ujue umekubalika ulivyo. Matokeo yake inabidi nishushe hadhi ya starehe zangu ili mpenzi aweze kuafford, ni kuikatili nafsi huko!!!!

Na mwanaume wa hivi atake kulipia kitu halafu umwambie hapana Weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee....mnuno wake hauishi leo. Atakuaccuse vitu kibao. Baada ya siku kadhaa unamkuta anakula karanga na kijoti, kisa kulipa Ankara zisizo zake.

Ndio maana wadada wanaishia kwa wenye nazo ili kuondokana na hali ya kuona huruma kila siku.
Mjirekebishe!!!!!!!!
Ninachokiona hapa, unajipigia debe maji yameanza kuonesha dalili za kuzidi unga!

Wanawake mpo wa aina nyingi km wewe labda uwe mchepuko tu kuhusu ndoa siwezi kuoa mwanamke anayependa yeye ndiyo aonekane simply tu sina pesa kumzidi.
 
Nimekuelewa sana,lakini na uwe wazi tangu tunakutana ,nieleze kuwa una uwezo wa kujitoa na kunitoa,nieleze kuwa mali si kila kitu leo.
Nieleze kuwa kesho tutaijenga wote,pia niondolee mazingira yenye kutia wasiwasi(suspicious environment),kama kutopokea simu yangu kila nikipiga,kunieleza ulipo kila tukiongea,kutonuna unapokuwa na shida ambayo huwezi kuitatua mwenyewe na wala kuniambia leo una mtoto na wadada wenzio tu bila mimi kuwa meza ya tatu.
 
"Halafu kingine ni kuwa I am generous, sio mchoyo kabisa. Kuwa na mimi na utaexperience kila ninachoexperience. Ukiwa mtu wangu automatically ntakuinclude nikienda shopping, movies, nikipanga safari ya bata nakujumuisha na kila kitu."

For Promotional Use Only.
Asante kwa kunisaidia kutangaza zaidi. Sijui nikulipee
 
Ninachokiona hapa, unajipigia debe maji yameanza kuonesha dalili za kuzidi unga!

Wanawake mpo wa aina nyingi km wewe labda uwe mchepuko tu kuhusu ndoa siwezi kuoa mwanamke anayependa yeye ndiyo aonekane simply tu sina pesa kumzidi.
Hahahahaha....maji yakizidi unga si nakoroga tu uji. Tatizo liko wapi? Wewe kwanza kwa ulivyo mwanamke kama mimi utanisoma tu JF. Roho mbaya haijengi!
 
Back
Top Bottom