Wanaume wengi, hasa wa JF wanalalamika sana kuwa wanawake tunataka wanaume 'wenye pesa' au waliofanikiwa tu. Pia kuonesha hii (kukubalika bila kuwa na pesa au kuhonga) ndio concern kwa wanaume wengi ni pale nyimbo nyingi za Kitanzania message ni hiyo hiyo, mfano: "Japo sina kitu,......", "Ukawaacha wenye pesa......" Tukilala njaa......"
Nikirudi kwenye mada, Kukosa pesa sio tatizo!!!!!
Mimi ni mtu ninayependa finer things in life. Napenda vitu vizuri na sisubirii mtu anipe. Kwenye kujipa raha sinaga subira wala uoga, najigharamia. Halafu kingine ni kuwa I am generous, sio mchoyo kabisa. Kuwa na mimi na utaexperience kila ninachoexperience. Ukiwa mtu wangu automatically ntakuinclude nikienda shopping, movies, nikipanga safari ya bata nakujumuisha na kila kitu.
Sasa unakuta uko kwenye mahusiano na mtu, akishajua jinsi unaendesha maisha yako anataka kujitutumua kukuimpress. Anataka kukupa huduma zile zile unazojipa mwenyewe au hata zaidi kwa pesa ambazo hana ili tu umuone bora zaidi. Inatia huruma!
Unakuta unamuinvite mtu out anataka kulipa wakati unajua kabisa hawezi kuafford, kwanini mnajitesa wanaume. Mtu ukishapendwa usiwe na hofu, ujue umekubalika ulivyo. Matokeo yake inabidi nishushe hadhi ya starehe zangu ili mpenzi aweze kuafford, ni kuikatili nafsi huko!!!!
Na mwanaume wa hivi atake kulipia kitu halafu umwambie hapana Weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee....mnuno wake hauishi leo. Atakuaccuse vitu kibao. Baada ya siku kadhaa unamkuta anakula karanga na kijoti, kisa kulipa Ankara zisizo zake.
Ndio maana wadada wanaishia kwa wenye nazo ili kuondokana na hali ya kuona huruma kila siku.
Mjirekebishe!!!!!!!!